Ni mama au balaa ya familia…………………? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mama au balaa ya familia…………………?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 1, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba hata Polisi walipofika katika eneo la tukio waliamini kwamba yule mama alikuwa ameuawa na majambazi. Kwani wakati mauaji yale yanafanyika mume wa yule mama alikuwa baa ya jirani na wenzake akicheza Darts, na watoto wake wawili Glenn aliyekuwa na umri wa miaka 15 na John aliyekuwa na umri wa miaka 14 walikuwa wametumwa na mama yao huyo kumtembeza mbwa wao.

  Kwa mujibu wa maelezo yao wakati wakihojiwa na polisi walisema kuwa walimkuta mama yao akiwa sakafuni amefariki huku damu ikivuja kichwani kwani alikuwa amepigwa na kitu kizito. Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kwenye eneo la tukio askari wa upelelezi aliyejulikana kwa jina la Heigh, alisema kwamba, mwizi yule angeweza kuchukuwa fedha zile, kiasi cha dola 150 zilizoibwa kwenye tukio, bila hata ya kuuwa, kwani ni kiasi kidogo sana cha fedha ukilinganisha na uhai wa mtu.Akionekana mwenye majonzi, mume wa marehemu, Davidi Howells alisema kwamba, wezi wale ni sawa na wanyama kwani wamedhulumu uhai wa mkewe pasipo sababu.

  Baada ya Polisi kufanya mahojiano na watu kadhaa, wakiwemo waalimu wenzie na marehemu na majirani zake, walikuja kugundua kwamba, pamoja na sifa nzuri alizomiminiwa kuwa ni mwalimu mzuri kwa watoto, hasa katika masomo yake ya Historia na Dini, lakini majirani zake walimwona kama mzazi mkali sana kwa familia yake. Ilielezwa kwamba, nyumba yake haikuwa na amani kwa sababu ukali wake, na walifikia hatua ya kuifananisha familia hiyo na jehanam. Maelezo yale yaliwafanya Polisi wakiongozwa na mpelelezi Carry Heigh kuichunguza zaidi familia husika kuhusiana na kifo mcha mama yule.

  Ni tukio lililotokea mnamo Agosti 1995 katika mji mdogo wa Dalton nchini Uingereza ambapo mama mmoja aitwaye Eve Howells aliyekuwa na umri wa miaka 48 wakati huo, ambaye alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi, aliuawa kwa kupigwa na nyundo na mwanae aitwae Glenn ambaye alikuwa na miaka 15 wakati huo wa mauaji. Ukweli huo ulikuja kujulikana baada ya Polisi kuitilia mashaka familia husika. Inasemekana baada ya kuwahoji watoto hao wa marehemu kwa muda mrefu ndipo hatimaye Glenn alikuja kukiri kwamba, ni yeye aliyemuuwa mama yake kwa kumpiga na nyundo kichwani, baada ya mama yake kumuita ‘toto vivu na goigoi,' kwa sababu hakumtembeza mbwa kama alivyoagizwa na mama yake. Ndipo kwa hasira akaenda chumbani kwao na kuchukua nyundo na kuja kumpiga nayo mama yake kichwani. Baada ya kufanya mauaji yale alimuita mdogo wake na kwa kushirikiana walivuruga nyumba na kuvunja mlango wa uani ili kuonesha kwamba, wezi wa kuvizia (burglary) ndio waliomuua mama yao.

  Kwa mujibu wa maelezo yao walikiri kwamba, kumuua mama yao ilikuwa ni suluhisho la kumaliza mateso waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa mama yao huyo, kwani mama ayao alikuwa akiendesha nyumba kwa mkono wa chuma, alikuwa ndiye mwenye sauti na mwenye maamuzi yote ya familia.Kwa mfano alikuwa akimpa baba yao dola 50 tu ya matumizi yake binafsi kwa wiki, na alikuwa akifunga majokofu yote kwa kufuli ili kuwazuia wasile kitu chochote bila idhini yake, na wakti mwingine alikuw akiwapiga na kuwafungia ndani kwa siku nzima kama adhabu hata kwa kosa dogo namna gani. Awali Polisi walishindwa kumhusisha baba na watoto wake katika kesi ile ya mauaji ya mkewe, lakini walipozidi kuwahoji watoto wale, ndipo mamo mengi yalipoibuka.

  Mpango mzima wa kumuuwa mama yao uliandaliwa kwa miaka miwili na baba akishirikiana na wanae, kwani wote walikuwa wamechoshwa na vitendo vya mama yao pale nyumbani.
  Inasemekana awali walipanga kumsukuma barabarani ili agongwe na gari lakini wakashindwa, halafu wakapanga wakienda likizo kwenye maeneo yenye maporomoko ya maji wamsukumie huko, mbinu hio nayo pia ikashindikana, mwishowe ndipo ukasukwa mpango wa kumpiga kwa nyundo kichwani akiw amekaa sebuleni, ambapo ndio mpango uliokuja kufanikiwa. Pamoja na mateso yote yaliyoainishwa katika maelezo yao, lakini kubwa lillokuwa likimuuma mume wa marehemu ni kitendo cha marehemu kuwa na uhusiano nje ya ndoa na rafikie wa karibu kwa muda wa takriban miaka 12.

  Kwa mujibu wa maelezo yake, alikiri kwamba mkewe alikuwa ni mjanja wa kutumia maneno kiasi kwamba ilikuwa si rahisi kwake yeye kuinia kwenye mabishano na mkewe, kwani alikuwa na mamlaka na kila kitu ndani ya nyumba. Kutokana na ushahidi uliopatikana baba na wanae walifikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la kula njama kwa pamoja na kisha kumuuwa Rve Howells. Kesi iliunguruma na hatimaye walipatikana na hatia. Baba alihukumiwa kifungo cha maisha jelana watoto wake wawili waliamriwa kupelekwa kwenye jela ya watoto hadi hapo watakapotimiza umri wa miaka 18 ndipo watakapohukumiwa rasmi.

  Akihitimisha hukumu yake jaji aliyeongoza jopo la Majaji katika kesi hiyo mheshimiwa Alliott, alisema kwamba, kitendo cha Eva Howells kuwa katili kwa watoto wake pamoja na mumewe, si cha kuvumiwa lakini hiyo haihalalishi yeye kuuawa.
   
 2. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #2
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hii habari ni mahsusi kwa wazazi au walezi wanaoziendesha familia zao kwa mkono wa chuma.............................................!
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwenyezi mungu atustiri na watoto wetu,huyu bwana siangempa talaka yakajishia kuliko kuua...
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  duh................
   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  aisee hii ni hatari sana hasa kwa mi mama kama hiyo..
   
Loading...