Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,566
- 41,082
Ukitafakari kwa umakini unashindwa kwa kabisa kuelewa Serikali yetu wakati wote imekuwa inaundwa na watu wa namna gani. Maana karibia kila kitu inachofanya, huwa hakina matokeo ya mafanikio.
Uzalishaji wa umeme ni teknolojia ya chini kabisa ambayo hata vijana wenye akili ya kawaida wanaoweza kusikiliza maelekezo wana uwezo wa kufanya.
Kikubwa unachohitaji ni nguvu ya kuzungusha turbine, na kitu cha kubadilisha ule mzunguko ambao unatoa mechanical energy, kupeleka kwenye electrical energy.
Nguvu ya kuzungusha turbine, unaweza kuipata kutoka kwenye maji yenye mporomoko, pressure ya mvuke uliotokana na kuchemsha maji kwa kutumia gas au kuchemsha kwa kutumia nuclear energy.
Ukishauzalisha umeme, kuna mambo machache hapo katikati kama transformer kwaajili ya kuongeza au kupunguza. Lakini kilicho kikubwa ni kuusafirisha tu kwa kutumia wire ili uende ukamfikie mtumiaji.
Kama tunashindwa hata kuzalisha tu umeme, tukizalishwa tunashindwa hata kuusafirisha, hivi sisi ni kitu gani tutakiweza hapa Duniani? Wizi tu wa kura?
Siamini kuwa Watanzania wote wameshindwa kuihakikishia jamii umeme wa kutosha. Fikiria shirika la TANESCO linashindwa hata kusimika tu nguzo kwa umakini. Sasa hivi maeneo mengi yanakosa umeme kwa sababu nguzo zinadondoka hovyo.
Tunakosa umeme kwa sababu TANESCO ni shirika la Serikali. Kama lingekuwa shirika binafsi, tungekuwa na umeme mpaka wa ziada. Kitu chochote kikiwa chini ya Serikali tegemea uhovyo na ufanisi duni kabisa.
TBL ilipokuwa chini ya serikali, wanywaji kupata bia ilikuwa tatizo kubwa. Leo wanywaji wanabembelezwa.
TCC ilipokuwa chini ya setikali, wavutaji sigara ilikuwa ni kwa mwendo wa kuruka.
Huduma za simu zilipokuwa chini TTCL ya Serikali, kuunganishiwa simu kwa haraka ukitaka kupiga simu mpaka uwe unampa rushwa station master. Leo watu wanabembelezwa kupiga simu.
Maadam TANESCO bado ipo chini ya Serikali iliyofeli kwenye masuala yote ya uchumi na biashara, tusitarajie muujiza.
Wakati wa usafiri wa mabasi ya Railway, kupata ticket ni lazima ukamhonge station master au mfanyakazi wa Railway, leo abiria anakimbiliwa na wapiga debe kumbembeleza.
TANESCO ifutwe. Makampuni yenye uwezo wa kuzalisha umeme hata kama ni kwa kijiji kimoja, Wilaya au mkoa, yapewe uhuru wote wa kutoa huduma hiyo bila ya kuingiliwa na Serikali au ukiritimba wa TANESCO. Tunaweza kuamza na mikoa michache, huku tukipima mafanikio. Nima hakika yakipewa makampuni binafsi, kuna siku wananchi watakuja kubembelezwa kutumia sana umeme.
Kuanzia jana nipo mkoani Tabora. Jana yote mchana hakuna umeme. Leo mchana yote mpaka usiku huu, hakuna umeme.