Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni hivi majuzi tu gazeti la Mwanahalisi lilitujuza kuwa Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, BEN SAANANE ambaye amepotea tangu Novemba 19, 2016 anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa. Habari hiyo ilileta mshtuko miongoni mwa wanachama, wapenzi na wafuasi wa CHADEMA hasa kutokana na muda, gharama na usumbufu uliojitokeza wakati wa kumtafuta kiongozi huyo. Kupitia habari hiyo, Wafuasi wa CHADEMA walimshinikiza mmiliki wa gazeti hilo, SAED KUBENEA kuthibitisha madai yake ama aombe radhi kwa kuandika habari ya upotoshaji.
Hata hivyo, SAED KUBENEA hajaomba radhi na wala hajathibitisha habari hiyo. Ninaamini kwa wote wenye akili timamu, bado wana kumbukumbu ya habari hiyo hasa wale walioendesha kampeni ya kuchoma gazeti hilo.
Inashangaza sasa watu wale wale wakiwa na akili zilezile wanafurahia habari ya aina ile ile juu ya Elimu ya PAUL MAKONDA. Mbaya zaidi ni pale wanapommiminia sifa lukuki kwa kuandika habari za uongo ambazo hazijathibitishwa na upande wowote. Ndipo nilipojiuliza, je, ina maana wamesahau kuwa ni Mwanahalisi ndilo lililodanganya juu ya kuonekana kwa Ben Saanane kwenye vijiwe vya kahawa?
Nitumie fursa hii kuwashauri CHADEMA, tumieni akili japo kidogo tu!