Wakuu, Amani ya bwana iwe nanyi!
Leo nilihudhuria maziko ya mama mmoja huko Simanjiro ambapo misa iliongozwa na Msaidi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati Mchungaji. Kivuyo.
Wakati akihitimisha mahubiri yake huko makaburini akawaambia waombolezaji hasa wamasai waache tabia ya kuelekeza mwili wa marehemu uwapo kaburini kaskazini kama wapagani wafanyavyo maana wakirsto huelekeza mwili "Magharibi" maana ndiko Yesu atakapotokea!
Sasa Mimi nikajikuta na maswali mengi kweli kweli ya kujiuliza;
Mosi, Ikiwa ni kweli kama alivyosema Msaidizi wa Askofu, Je huyu Mama sasa ataonekana vipi na Yesu anaetokea Magharibi na mama ameelekezwa kaskazini?
Pili, Maandiko yanasema "hatujui siku wala saa atakapokuja mwana wa adamu".....sasa swali langu ni Je kama hatujui siku wala saa atakapokuja Yesu, tutajuaje "upande" atakapotokea?...I meant huyu Askofu yeye amejuaje upande Yesu atapotokea ikiwa hata hajui siku wala saa?
Ama kweli kaniacha na maswali kichwani bila majibu lakini nafahamu humu ndani tunao wataalam wa Biblia na hapana shaka watatudadavulia haya masuala kama kuna ukweli kwa aliyotueleza leo M/dizi wa Askofu Mchungaji Kivuyo!