Ni lazima kulala ubavu wakati wa kujifungua?

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,289
12,957
Habari za jioni wapendwa wana jukwaa...

Kuna swali linanitatiza, je kuna uhusiano gani kati ya kulala ubavu??? Maana nimejaribu kuangalia katika mitandao naona wenzetu wazungu huwa wanajifungua bila kulala ubavu.

Lakini sisi wabongo ukitaka kujifungua unaambiwa na manesi ulale ubavu...

Naomba msaada wanajukwa!!

CL
 
Unalala ubavu kabla ya kujifungua huku wakimonitor mapigo ya moyo ya mtoto na progress ya njia kufunguka. Hata wazungu huwa wanalala ubavu only wakati sasa ndo njia iko fully na mtoto ni tayari kwa kuzalisha ndio wanageuka na kulala chali na hizo ndio picha wanazoonesha kwenye mitandao the actual process of delivering.

Maana ya kulala ubavu ni kuwa kuna mshipa mkubwa unaorudisha damu kwenye moyo (inferior vena cava), ukilala chali muda mrefu na kizazi ni kikubwa kwa sababu ya kuwa na mtoto ndani huweza kukandamiza huu mshipa kitu ambacho husabanisha pressure kushuka, mapigo ya moyo kuongezeka na mama kijisikia vibaya. Hivyo ukilala ubavu ubakwepa hiyo adha.

Na pia kujifungua sio lazima uwe uko chali kwenye kitanda. Wenzetu wame advance na kuna water birth siku hizi ndani ya bath tub nurse anakuja kukuzalisha home kwako wanasema water reduces labour pains for those going natural labor.... charminglady my daughter nimejibu Swali lako?
 
Back
Top Bottom