Ni lazima au hiari kuchangia harusi?

Ni lazima au hiari kuchangia harusi?

koba lee

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Posts
982
Reaction score
1,612
Naombeni tusaidiane kwa hili,nina rafiki zangu kama watatu hivi, walifunga ndoa katika nyakati tofauti, na hawa jamaa kidogo maisha yao washajipanga hela ya kubadilisha mboga sio tatizo kwao,magari ya kutembelea wanayo so nahisi kila kitu kinawaendea vizuri.

Sasa katika michango yao ya harusi nilimchangia mmoja tu yule aliyefunga ndoa akiwa wa kwanza lkn cha ajabu sikupewa kadi ya kuhudhuria harusi na pia kiwango nilichoahid kutoa chote nilitoa kama asilimia 80, sasa sijui hilo ndo lilikua tatizo au vp (hata angenipa nisingehudhuria),hawa wengine sikumchangia hata mmoja sio makusudi bali maisha hayajaniendea vizuri bado napambana. Wote wamenizidi kipato na wanaelewa hali halisi.

Sasa basi nimegundua jamaa kama nikiwapgia simu wananikunjia hawaongea kwa furaha kama zamani na mda mwingine unapiga cm haipokelewi wala nini.nikaona sio tatizo wasijeniona kama nawaomba undugu nimepotezea pia naendelea na yangu najua tatizo ni michango.

Sasa wakuu hivi kuchangia harusi ni lazima au imekaaje,na usawa huu ulivyokaa tenge watu budget mda mwingne haziruhusu
 
Leo nimepewa kadi tatu za kutumika ndani ya mwezi mmoja wasaba kadi 10000 na nimepigika sana,bahati yao wamewatumia kamati wangekua wamekuja wenyewe wangeona bora waahirishe
 
mi nishaachaga hizo mambo ila jipange sio usichangie wenzio alafu wewe uje uombe hela
 
Kuchangia ni hiari lkn kwa wabongo usipochanga unachukuliwa kama siyo mshirika utasubiriwa siku yako ikifika una sherehe utasikia yule anajitenga hashirikiani na wenzake
 
Wengine mnatuona hatuoi sababu mahesabu ni makali sana. Sasa wewe unaamua kuoa halafu unakuwa kero..toka vikao vimeanza hatupumui

Muonege aibu na muwe waelewa

Kuomba mchango ni aibu ila basi tu.

Ila naamini ipo siku huu ujinga utaisha..

Wenzenu kama uwezo mdogo..wanavaa nguo tuu wanaoana, wanakunywa pepsi kwishney

Sasa mtu unakuwa mwiba
 
Utakuwa umekosea umeandika thread badala ya sms kwa mlegwa.
 
Utakuwa umekosea namba mkuu au jamaa yako yupo hapa jukwaani?
 
Mkuu changia tu ata kama huna pesa kakope nawewe tutakuchangia
 
Nawakubali sana wazungu.
Huku sisi tunahudhuria harusi za watu ambao hata hatuwajui.
 
Michango ni ya ugonjwa au msiba tu kuchangia ndoa ya mtu kwa mimi ni upumbavu
 
Hii iliwahi tokea mwaka 2008 nimepewa kadi ya Mr & Mrs ili nichangie ,mzee nikajipiga piga nikapata 70,000/= maana double ilikuwa laki,single hamsini, basi baada ya kutoa ile kwa kujidhiki na kumheshimu mshikaji ajabu na kweli nilikosa sikupata hata kadi ya single kwa kuwa kiwango hakikutimia ,kiukweli iliniuma sana,toka kipindi hicho huwa napokea kadi za harusi na kumpa mwanangu achezee,,,
 
Back
Top Bottom