Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,187
- 670
haya wale magwiji wa michezo ambao mlikuwa mkifatilia kwa muda mrefu mvutano uliopo kati ya ZFA na TFF hii inatokana na kuwa ZFA ni wapenda migogoro au kuna namna.
jee huyu mwakalebela hutumia kutofahamina kati ya ZFA na SMZ ni kisingizio cha kuhalalisha ufifilishi wao kwa ZFA na zanzibar kwa ujumla?
ZFA ni wapenda migogoro - Mwakalebela
2008-06-18 09:03:14
By Somoe Ng\'itu
Shirikisho la soka nchini (TFF) limesema kuwa Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kinatumia muda mwingi kuanzisha malumbano na migogoro inayohusiana na safari za nje ya nchi badala ya kuandaa programu za maendeleo ya mchezo huo visiwani humo.
Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa TFF, Frederick Mwakalebela alisema kuwa viongozi wa ZFA ambao hivi karibuni wametangaza rasmi kutoshirikiana na shirikisho hilo kuhusiana na timu ya taifa, Taifa Stars kila siku wamekuwa wakianzisha `hoja` zinazopingana na serikali yao na pia wakilalamikia vitu ambavyo ufafanuzi wake wanaufahamu na kuipotosha jamii.
Mwakalebela alisema kuwa katika kuonyesha kuwa chama hicho kinatumia muda mwingi `kulumbana` badala ya kufanya shughuli za maendeleo kimetangaza kutoshirikiana na TFF huku timu zao za vijana za umri chini ya miaka 17 ziko jijini Dar es Salaam na zinashiriki katika mashindano yanayojulikana zaidi kwa jina la Copa Coca Cola yanayoendelea katika viwanja mbalimbali.
``ZFA wanashindwa kujielewa mambo wanayosema na wanayofanya, kama wamevunja ndoa na TFF ni kwanini wameleta timu katika mashindano ya U-17 na mjumbe wao pia yupo,`` alisema Mwakalebela.
Aliongeza kuwa kila inapotokea safari ya viongozi wa TFF wanakwenda katika mikutano ya kimataifa kuiwakilisha nchi ndio malalamiko yanapoanza na wao wanashindwa kuwaelewa ZFA ambao wanafahamu wazi kuwa waalikwa wa mikutano hiyo ni TFF ndio wanachama wa mashirika ya soka ya kimataifa.
Alisema pia kila kinachofanywa na TFF kinatokana na maelekezo yaliyopo katika katiba na wao ZFA wana katiba yao inaowaongoza katika shughuli za kila siku za kuongoza soka hapa nchini.
Alisema kuwa ZFA mara kadhaa wameshindwa kukubali kuihudumia timu ya taifa, Taifa Stars inapotaka kwenda visiwani humo na wakati TFF imeisaidia timu yao, Zanzibar Heroes na kuinunulia vifaa ilipokuja katika mashindano ya Kombe la Chalenji mwaka jana lakini yote hayo hayasemwi.
``Umefika wakati wakaacha kuipa kipaumbele migogoro na kuangalia mambo ya msingi ya maendeleo, TFF ni wanachama wa FIFA (Shirikisho la soka la kimataifa) tutafanya kila kinachotakiwa kukuza soka hapa nchini,`` aliongeza.
Siku moja kabla ya Stars haijacheza na timu ya taifa ya Cameroon, Makamu wa Rais wa ZFA, Haji Ameir alikaririwa akisema kuwa wao wamevunja `ndoa` na TFF na kudai kuwa Stars ni timu ya Tanzania Bara.
SOURCE: Nipashe