Ni kweli wenye umri wa miaka 25 mpaka 35 wana stress sana?

emavalery

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
628
1,237
Habari wakuu, hivi ni kweli sisi kwenye hii age ya miaka 25 mpaka 35 wanakua na mawazo sana na pressure.

Naoana na mm kuna frustration na depressions kibao zinaingia kwa kichwa.

Kwa wale mliovuka salama, tupeane uzoefu, pressure ya pesa ndio kubwa sana.

Karibuni kwa maoni wadau.

Screenshot_20200916-072135.jpg
 
Kila kitu kuhusu future yako unapanga sasa wewe mwenyewe.

Kwa wengi inasababishwa na kutokujali muda, kutokuwa na special plans, kutokuwa na misimamo..

Vijana wengi miaka 15to27 hawana hivyo vitu hapo juu.

Kutokujali muda.
Vijana wengi wenye miaka hiyo hapo hawajali muda iwe kwa kujua ama kutokujua.
Wengi wakati wapo kwenye hiyo age walikuwa hawajali muda na hawajui kwanini wapo hapa duniani hivyo hutumia muda wao vibaya kufanya mambo ambayo yataifanya future yao kuwa mbovu.

Mtu mradi yeye ni mwanafunzi basi yeye hajali chochote wala hafikirii chochote kuhusu maisha anayoishi wakati huo aliopo yaani present zaidi ya kusoma shule tena hajui kwanini yupo shule wakati huo.

huku akifanya na kufikiria mambo kama Mapenzi yasiyo na lazima wala maana yoyote, Ngono zembe, stori za mpira, kukaa vijiweni baada ya masomo na kujadili au kubishana vitu visivyo na mantiki wala faida yoyote, kuvuta bangi nk.

Kutokuwa na special plans.
Mtu anayeishi bila mipango maalum ni sawasawa na kipofu anayekwenda sehemu ambayo hajawahi kufika na hajui kwanini anaenda anakokwenda.
Na hauna tofauti na mnyama yoyote aliyetofauti na binadamu.

Mtu anasema baada ya miaka kumi nitakuwa engineer au mfanya biashara wakati huo anafikiria mtu wake wakafanye ngono na kuchat ujinga, kwenda club, kukaa vijiweni kuongea ujinga, kujadili ujinga nk.

Mtu kama huyo baada ya muda aliyojipangia kufika sehemu fulani lakini baada ya muda kufika bado hajafika alipopataka lazima apate msongo wa mawazo na kukata tamaa sababu alikosa special plans ina maana alikosa kujali muda na utekelezaji pia.


Mtu kama huyo baada ya kumaliza masomo na kukutana na maisha halisi lazima apate msongo wa mawazo na kukata tamaa sababu akili yake hajaifundisha kufanya hivyo na nilisema mtu huyo hajui kwanini alienda shule zaidi ya ajira na akikosa hiyo ajira aliyotegemea lazima apate msongo wa mawazo na kukata tamaa mwisho kujiua tu.

Yote sababu hakujali muda, kuwa na special plans, kukosa misimamo, wala kutokujua kusudio lake hapa duniani.

Na bado wanaendelea kufarijiana kwamba maisha yanaanza 40 wakati ni uongo ili kupata amani ya moyo, maisha yanaanza baada ya wewe kutoka kwenye tumbo la mama ako.
 
Subiri mpaka 40 hapa ndo kuna siri kubwaa!
Ukifika umri huo huna kitu, unapunguza matarajio.

Kama ni kutembeza mbogamboga nyumba kwa nyumba hujali tena.

Kuhusu ndoto za kuwa kama Bakhresa, utasema tu Inshallah.

Mungu hakunijaalia.

Hapo hata mke utaoa yeyote tu. Hata nyumba ya miti utaishi tu, ndoto za mijengo ya instagram hakuna tena.

Na kama ni dada ndoto za kuolewa na Justin Bieber zinakufa, unatafuta yeyote kama Aunt Ezekiel.
 
Back
Top Bottom