Ni kweli Watekaji hawajulikani?

Ni kweli Watekaji hawajulikani?

Mdude na Soka hawajulikani waliko. Mzee Kibao kutekwa mchana kweupe, sijui mwelekeo wa nchi kwenye usalama wa raia ni upi. Tuhuma nzito za ufisadi kila kona, maisha ya watanzania ni magumu. Kwa kipindi kifupi taifa linakosa mwelekeo.
 
Kennedy Mwamlima anasema alivyotekwa Mbeya mwezi April 2024, watekaji walimfunga pingu na kumvalisha mzula usoni ili asione lakini mzula huo ulikuwa unaangaza.

Anadai gari hilo lilikuwa linaendeshwa kwa kasi mno kuliko ambulance huku dereva akipuuza kuzingatia alama za usalama barabarani. Anasema gari lilisimamishwa na askari wa Usalama barabarani kwa kosa la kuzidisha mwendo Chimala, mmoja wa askari akamsogelea dereva na kumfokea kwamba kwanini anazidisha mwendo ambao ni hatarishi? mmoja wa watekaji akashusha kioo kidogo na kumuonyesha askari huyo kitambulisho. Baada tu ya kuonyeshwa kiitambulisho askari huyo alikuwa mpole na kuruhusu gari haraka.

Gari ilivyofika Igawa likakamatwa tena kwa wrong overtaking, tena askari mkamataji wa safari hii alikuwa na cheo cha Inspector. Askari huyo alikuwa mkali kwa dereva kwamba kwanini anaovateki eneo ambao haliruhusiwi kuovateki? Lakini alipooneshwa kitambulisho tu akakausha na wala hakutaka majibu ya swali lake zaidi ya kuruhusu gari liondoke haraka.

Je ni kweli watekaji hawajulikani kama wanavyosema polisi, waziri wa mambo ya ndani na Rais Samia? Kwani nikisema Samia ndio mtekaji na kikosi hiki cha kuteka kina baraka zake nitakuwa sahihi?
Inasikitisha Sana.

M.A.P Sumu ya Nyigu 7x70.
 
hautakuwa sahihi kama unaushahidi nenda katoe taarifa polisi siyo kuropokaropoka tu hovyo hujitambui wewe kijana wa hovyo sana hufai katika jamii ya wastaarabu
Naona Roho yako ina Amani sasa baada ya kutimiza lengo lenu na la 29october..
Haya yote ili mtawale milele??
Siku yajaa na yote yatawarudia ninyi na familia zenu
 
Back
Top Bottom