Ni kweli wanaume hutangulia kufa?

Shinto

JF-Expert Member
Dec 6, 2010
1,781
96
Ndugu,
Mimi nimeoa na nina watoto. Nimekuwa nikisikia mara kwa mara kutoka kwa wake wa kaka zangu wanashitakia kwangu kuwa kaka zangu hawafahamishi wake zao juu ya mali zote wanazomilki, deals zao na business contacts.
Hoja wanayoileta ni kuwa pindi wanaume wao watakapo kufa wao na watoto watapata shida!
Hivi karibuni na mimi nimeanza kupigiwa makelele haya haya.
Ninachojiuliza kwa nini hawa wanawake wanadhani wanaume ndio watakufa kwanza wawaache wake na watoto? Nadhani hata nyinyi ndugu mmewahi kusikia hili..
Je kuna ukweli wowote? Kuna takwimu zozote za kuthibitisha hili? Au ni janja yao tu kudai maslahi?

Tafadhali saidia mimi
 
Kwa asilimia kubwa ili jambo linaukweli ndani yake we ukitaka kujua ukweli fanya utafit wa kujua idadi ya wajane walifiwa na waume zao.
 
Ni kweli ndugu. Wajane kina mama ni wengi sana kuzidi wajane wanaume. Yaonesha wanaume wanakufa mapema zaidi. Hii pia ni kwa vile wanapofunga ndoa mara nyingi mume anakuwa anamzidi miaka kadhaa mke wake. Na hii kufanya mme kuzeeka kabla ya mke na hivo kuwa na uwezekano wa kufa kabla ya mke. Kumbe yafaa kupanga mapema mambo ya mali na urithi.
 
Sababu nyingine ni kuwa wanaume wanafanya kazi nyingi zilizo-risky na kwa hiyo kuongeza possibility kufa mapema
 
Mimi nilikuwa nadhani kuwa na wajane wengi ni kwa sababu wanawake wengi wakifiwa huwa hawaolewi tena, wakati wanaume hata awe 65 and above lazima ataoa?!
 
Ndugu,
Mimi nimeoa na nina watoto. Nimekuwa nikisikia mara kwa mara kutoka kwa wake wa kaka zangu wanashitakia kwangu kuwa kaka zangu hawafahamishi wake zao juu ya mali zote wanazomilki, deals zao na business contacts.
Hoja wanayoileta ni kuwa pindi wanaume wao watakapo kufa wao na watoto watapata shida!
Hivi karibuni na mimi nimeanza kupigiwa makelele haya haya.
Ninachojiuliza kwa nini hawa wanawake wanadhani wanaume ndio watakufa kwanza wawaache wake na watoto? Nadhani hata nyinyi ndugu mmewahi kusikia hili..
Je kuna ukweli wowote? Kuna takwimu zozote za kuthibitisha hili? Au ni janja yao tu kudai maslahi?

Tafadhali saidia mimi
Mhhh mkuu umeenda mbali sana, hapo sio swala la kufa tu, anawaza akifa yeye mwanzo ni sawa je ukifa wewe inakuwaje ikiwa humwonyeshi mali zako zote? au unataka mpaka ufe ndio aanze kutafuta mali zako?
 
kuna ubaya gani ukimshirikisha mkeo mali/biashara mlizonazo..........wakati mwingine mali zinapotea au kutokujua namna ya kuziendeleza unapofariki.....kumbuka ni faida pia kwa watoto wako unaowaacha

kuna ubaya gani ukimshirikisha mkeo mali/biashara mlizonazo..........wakati mwingine mali zinapotea au kutokujua namna ya kuziendeleza unapofariki.....kumbuka ni faida pia kwa watoto wako unaowaacha

Hilo nakubali.....ila la kutangulia kufa nina mashaka nalo! wasije wakawa wanatumachame kwa kuamini tunatakiwa tufe mapema!
 
Hilo nakubali.....ila la kutangulia kufa nina mashaka nalo! wasije wakawa wanatumachame kwa kuamini tunatakiwa tufe mapema!

kutangulia kufa sina uhakika....... inawezekana tabia hiyo ipo............ iwapo uliyemwoa atakuwa na tamaa ya kumiliki mali ..... na hii huwa inajengeka toka mwanzo kabla ya kuona au ushauri kutoka kwa marafiki.

kuna ubaya gani ukimshirikisha mkeo mali/biashara mlizonazo..........wakati mwingine mali zinapotea au kutokujua namna ya kuziendeleza unapofariki.....kumbuka ni faida pia kwa watoto wako unaowaacha

Labda anaogopa mtindo wa baadhi ya wanawake kuwaua wanaume kwa lengo la kumiliki mali
 
Hilo nakubali.....ila la kutangulia kufa nina mashaka nalo! wasije wakawa wanatumachame kwa kuamini tunatakiwa tufe mapema!
Kwa hilo neno ulilobold ghafla nimekosa msukumo wa kuchangia thread yako...kila la kheri!
 
Let me say like this....
Wanaume wengi ni wazito/wavivu kupika!! Huenda(ingawa siko sure sana) tunawekewa mavitu mengi kwenye chakula bila wenyewe kufahamu, hasa ukiwa kwenye ndoa na kuna tendency ya kuchokana!! Hivi vitu tukiendelea kuvi-consume,slowly death inakuja!!
Vilevile umri...wanaume wengi wanaoa wadada walio chini ya umri wao(wengi ni 5 to 10 age diffrnc) sasa expectance yetu ni ndogo, so wanaume wengi tunaondoka at certain age tukifika!!
 
ni kweli wanawake wanaishi miaka mingi kuliko wanaume. Biologically mtu ameumbwa kwa the so called gamete. A gamete (from Ancient Greek γαμέτης gametes "husband" / γαμετή gamete "wife") is a cell that fuses with nother cell during fertilization (conception) in organisms that reproduce sexually. a female is an individual that produces the larger type of gamete-called an ovum (or egg)-and a male produces the smaller tadpole-like type-called a sperm. hivo kutokana na wanawake kuwa na gamete kubwa kuliko za wababa (approximately 20 times), then wanauwezo wa kuishi miaka mingi kuliko wanaume, hata katika hali ya kawaida mwanamke ana uwezo wa kukaa bila kula kwa muda mrefu kuliko mwanaume.nakumbuka tukiwa darasa la tano tulisoma kuwa mwanamke anaweza kukaa hadi siku saba bila kula yle men ni ndani ya cku tano tu.Ikumbukwe kuwa utafiti huu ulifanyiwa yle other factors are constant, eg diseases,age etc.
PIA NAOMBA NIWASILISHE HOJA KUWA KWA ASILI MWANAMKE ANANGUVU NA NI JASILI KULIKO MWANAUME.
 
sababu nyingine ni kuwa wanaume wanafanya kazi nyingi zilizo-risky na kwa hiyo kuongeza possibility kufa mapema

hapo kwa kweli umenena maana wanaume huwa tunafanya kazi za kuumiza vichwa hata kama ni ngumu huwa hatukati tamaa kamwe. Hiyo hufanya akili kufanya kazi zaidi ya uwezo wake
 
wanasema life span ya mwanamke na mwaname ni tofauti. while ya mwanamke ni ndefu zaidi ya mwanaume of course ni fupi zaidi. kwa hiyo wanaume tunawahi kufa
 
Wanaumme kufa haraka ni ukweli kutokana na majkumu ambayo dunia hutubebesha...................na akia mama hutusubiria tupumzike kwa swala............ili wapasue dunia bila ya zengwe....................................ukizingatia mali tulizochuma sasa hawataki tule wote...................wanataka baada ya mali kupatikana watuharakishe ili wapasue nchi na dogodogo.........................ila siyo wote kwenye haya.............
 
ni kweli wanaume hufa haraka kuliko wanawake,unaweza mshirikisha mkeo na familia yako mapema kny mirathi....tafakari chukua hatua....:smiling:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom