Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 57,748
- 92,175
Kuna baadhi ya nyakati katika maisha binadamu mtu hupaswa kusimamia kile anachokiamini, akakiheshimu na kukiishi hicho! Binafsi nimechukizwa na nimefadhaishwa sana na kelele za baadhi ya wafuasi wa CCM wakimlaumu JK kuwa amefilisi nchi, nchi imefika pabaya kwa "uzembe" wa JK. si hao tu hata baadhi ya Viongozi wa kisiasa nikimaanisha DC na RCs na wengine wenye dhamana hizo wamesikika si mara moja wala mara mbili wakimkebehi JK aidha kwa maneno na matamshi yao au hata kwa vitendo vyao, mifano iko wazi kwa hili; kuzuia watu kwenda likizo, kufungia wafanyakazi nje ya geti, kufunga watu bila mpangilio eti tu kwa kushindwa kutekeleza jambo Fulani, na mara zote wakijibu kwa kujiamini kuwa hii ni AWAMU MPYA na kwamba sasa "wanafanya kazi" Rubbish!!!!
Lakini watu hawa hawa, miaka kumi iliyopita yaani karibia siku 700 nzima wamekua wakimsifu JK, hata pale tulipolalamika, watu hawa hawa waliandaa Press Conference na maandamano ya kumsifu JK, magazeti yakajazwa maneno mazuri ya sifa dhidi ya JK. Tulilia weeeee kuwaomba watu waone kuwa nchi inakoelekea siko kwenyewe lakini kamwe hatukusikilizwa. Cha ajabu leo hii watu hawa ndio wako mstari wa mbele kumkosoa JK kwa mgongo wa JPM..... kweli watu hawa wana akili timamu? Huu ni unafiki uliopitiliza.
Labda la mwisho kwa leo, kwa dhambi yenu hii hii ya unafiki, Magufuli nae mtamfanyia haya haya ya JK kwakua wengi wenu ni wachumia tumbo na mnaolinda maskahi yenu na watoto wenu, mimi nasema hivi, serikali ya CCM labda atokee malaika ndio itakua safi, nje ya hapo sitakaa nitegemee lolote toka kwa mtu aliye ndani ya CCM.
Hakuna dhambi mbaya kama unafiki.