Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,865
- 730,439
Tumeombwa tumehimizwa tumeshawishiwa na hata kutakiwa na serikali yetu tusaidie kufichua uovu popote pale na tutalindwa.
Pengine na inawezekana kabisa serikali yetu Kupitia jeshi la police ama haikumaanisha inachokisema au haikusema inachomaanisha.
Raia wenye utii na upendo mkuu kwa serikali yao, raia waso hatia wameuawa wengine kwa vifo vya mateso huku wengine wakifukuzwa kazi na wengine kubambikiwa kesi kubwa na sasa wako lupango kwa kosa moja tu KUISAIDIA SERIKALI KUFICHUA UOVU.
mifano ni mingi michache hii hapa
-Raia aliyewezesha kukamatwa kwa madawa mengi wakati wa kikwete anaozea jela kwa kesi isiyoeleweka (Ushuhuda wa mwakyembe waziri wa sheria)
-Raia aliyeuawa kikatili baada ya kufichua familia inayodili na Biashara ya meno ya tumbo (Mmoja wao ni kada na mbunge wa CCM)
-mifano ni mingi sana, na waliopotezwa si haba kwa ajili tu ya kujitoa kwao kufichua uovu kwa rai ya serikali.
Tunamaliza wiki hii na sinema ya Mangekimambi na Makonda... Huyu binti pamoja na mapungufu yake yote lakini suala la Makonda kalitendea haki na amesaidia pakubwa na kuweka ushahidi usioacha Shaka na vielelezo jadidi vinavyomfanya Makonda kwa sasa awe yuko nyuma ya vyuma vya gereza kama ingelikuwa hakuna makengeza kwenye maamuzi.
Vita aliyoianzisha Makonda haikuwa ya kweli bali ya kujikusanyia mali, tena kwa vitisho lakini badala Mange apongezwe na jeshi letu na serikali imetolewa hati ya kumkamata popote atakapopatika.
Tunavunjwa moyo na kukatishwa tamaa ama la pengine kuna wa kuripoti wale wasio nacho wauza bhangi na gongo uswahilini halafu kuna wale untouchables hawa usijaribu utakwenda na maji.
Tuhuma za Makonda ni nyingi na nzito sana zenye vielelezo vyote...lakini bado yuko huru ndani ya ofisi ya serikali akiendelea kutamba.
Isaidie serikali yako kufichua uovu lisaidie jeshi la police(ni jambo jema ni ni uzalendo) lakini jiongeze