Ni Kweli Sera za CCM zimeshindwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni Kweli Sera za CCM zimeshindwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 10, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tumeona mengi kuanzia kwenye nishati, madini, maji na kilimo. Na wiki hii tumeshuhudia makubwa zaidi katika afya na elimu ambapo kumomonyoka kwa sekta hizo kunadhihirishwa zaidi. Je ni hak kusema kuwa sera za chama tawala kwa kweli zimeshindwa?
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  completely derailed, sidhani kama hii serikali inaongozwa kwa kutumia sera yeyote ile, hapa ni rule of thumb ndiyo inayotumika from very few visionary leaders

  rescue inahitajika
   
 3. Alfred Daud Pigangoma

  Alfred Daud Pigangoma Verified User

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,778
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kwa sasa hakuna sera inayoongoza nchi! Watawala wa nchi hii hawana cha kuwaongoza! Mfano mzuri ni tukio la jana la kufanya marekebisho kwenye sheria ya mabadiliko ya katiba! Ukweli ni kwamba kwa hili ninaweza kusema sheria hii mwanzo iliundwa kwa sera ya CCM na jana imeundwa kwa sera ya CHADEMA! Hali hii imesababisha wabunge wa CCM kugeuka wapinzani na wabunge wa CHADEMA kuwa viongozi wa nchi! Hapa siongelei ushabiki wa vyama ila kila mmoja siku ya jana alijionea kilichotokea bungeni! Ninukuu kauli ya Mh. Machali-MB (NCCR) ''Kwa tukio hili atakayepinga atakuwa msariti!............... Kwa mara ya kwanza kama alivyosema Mh. T. Lissu nami naunga mkono hoja'' mwisho wa kunukuu!
   
 4. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kweli Mama Malecela ni muasi; tena hampendi JK kutoka moyoni na yuko tayari kwa lolote ali mradi JK afeli; very dnagerous woman, nilikuwa sikubaliani nao kabla sasa rasmi confirmed
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wapo watu wanafikiri sera nyingine kutoka watu walewale wa chama kilekile zitakuwa na tofauti!
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  "Kwa sasa uti wa mgongo wa nchi hii ni rushwa, sio kilimo...Karibia kila mtu nchi hii anaishi kwa rushwa. Wanaodai uti wa mgongo wa taifa hili ni kilimo wanadanganya watanzania. Shughuli pekee kwa sasa ambayo karibia kila mtanzania anajihusisha nayo ni kupokea,kutoa rushwa au kuathiriwa na rushwa kwa njia moja ama nyingine" - Yahoo! Groups
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  sio tu sera zimeshindwa bali hata mbinu za kudanganya kuwa sera zinafanya kazi zimeshindikana.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli mkubwa sana huu. Corruption has become a socio-political economic system within which all other private ad well as public activities are done. Without corruption certain things will never get done no matter the policies in place.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Nikuulize unazungumzia sera gani? CCM wana sera gani? Kama nchi yetu ni gari la abiria basi CCM ni dreva asiyejua tunakokwenda, hana ramani, basi tu ili mradi yuko barabarani akiimba umoja na mshikamano huku maliasili zetu zikiendelea kuporwa. Kama alivyosema Companero sera zilizopo hivi sasa ni rushwa tu. Kuanzia madini, uchumi, kilimo, kila kitu kinalenga uchumia tumbo wa viongozi. Hivi wewe unaamini kweli kwamba Pinda angeweza kuingia kwenye mradi hovyo kama ule wa Agrisol na kuupigia debe?
  We are lost with CCM in the driver's seat.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Wanakumbuka hata hizo sera ziko wapi? au zinasema nini? Nchi inaendeshwa kwa mfumo wa zima moto! Hakuna kitu kabisaaaaa
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii naomba iwe quote yangu for few days. It is objectively deep!
   
 12. B

  Bwanamdogo Member

  #12
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawana jipya maana sasa hivi kauli yao ni "TULIAHIDi, TUKAJARIBU, TUMESHINDWA NA TUNAZIDI KURUDI NYUMA"
   
 13. Companero

  Companero Platinum Member

  #13
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  mkuu mbona una-miss the point? rushwa ndio sera kuu ya nchi - ndio uti wa mgongo wa uchumi siasa wake!the political economy of corruption.
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Wameshindwa kabisa!Huo ndo ukweli!
   
 15. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Sera zinaposimama kwenye misingi hafifu ya utekelezaji sio sera tena bali ni mawazo duni yaliyoshindwa kuleta mabadiliko yenye tija.
  Chama tawala kinachanganya mambo mawili kwenye mfumo wake wa kuendesha nchi:
  1.Ilani ya chama cha mapinduzi(sehemu kubwa ikiwa siasa yenye nguvu bila misingi ya utekelezaji).
  2.Sera za kuendeleza nchi(mambo ya kitaaluma ambayo yanahitaji jitihada za makusudi ili kufanikisha utekelezaji wake)
  Ningependa kutoa mfano:
  Nilipata nafasi ya kushiriki kwa kiwango kidogo kwenye kuunda mpango mkakati wa kuendeleza sekta moja muhimu nchini.Baada ya kukusanya maoni ya wadau kwa ujumla kukawa na kikao cha wadau teule ili kuchambua sehemu muhimu za kuziwekea mkazo na kufanya masahihisho kwenye inception document ili kutengeneza first draft ya huo mpango mkakati.Tukaiomba wizara husika ituletee watendaji makini wanaoijua sekta ili kutoa mpango ambao umeshiba.Kwa mshangao wangu wakatuletea watu waliokuja wamebeba ilani ya CCM na kutaka hiyo ndiyo iongoze mjadala ya kutengeneza mpango mkakati.Haya ndiyo mambo yanayorudisha nyuma taifa hili.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sasa kwanini hata upinzani rasmi unaangalia CCM kuhusu sera? Nimefuatlia mambo ya Bungeni ambapo hata upinzani unaamini kuwa sera za CCM zinatekelezeka na hivyo unaziunga mkono?
   
 17. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Sera Yao ni chukua chako mapema. Kwa hili wamejaribu, wameweza na wanasonga melee kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi ya upepo.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimekupata vizuri kabisa! if corruption is the rule, then the rule is corruption!
   
 19. Companero

  Companero Platinum Member

  #19
  Feb 10, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  consensus ya sera ya nchi ilifikiwa zamani, toka zama za mwisho wa utawala wa nyerere - hata wanaharakati wana kaulimbiu yao ya "sera poa ila utekelezaji?" hivyo kimsingi upinzani na utawala uliopo haupingani. mathalan wote wanaamini uwekezaji ndio injini ya maendeleo. mbinu zao labda ndio tofauti.
   
 20. j

  jigoku JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Binafsi nachojua mimi hakuna sera kama Taifa labda kuna kauli mbiu ambazo ni kama nyenzo tu za kujairibu kulaghai wanachama wao wa CCM.hata leo hamkumsikia Prof.Tibaijuka alikiri bungeni kuwa hawana sera ya makazi ndo kwanza wanaindaa.
   
Loading...