Ni kweli Rais Kikwete hapigiwi Mizinga Zanzibar?

Ni kweli Rais Kikwete hapigiwi Mizinga Zanzibar?

Huu muungano kuna watu wameufanya kakichaka kakuficha uovu wao na sehemu ya kuneemesha matumbo yao. Kimsingi kilichoandikwa kwenye KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ambayo ndiyo msingi na kiapo cha watawala walioko madarakani sicho kinachotendwa, kusimamiwa na kulindwa kama walivyoapa. Mengi ni usanii mtupu ambao haufai hata kuelezewa mbele ya watu wenye uoni timilifu.

Tukio la sherehe za mapinduzi tarehe 12 Januari 2014 zilizohudhuriwa na Kikwete kama mgeni wa kawaida huku Shein akiwa mgeni rasmi na Amiri Jeshi Mkuu ni ushahidi usiohitaji elimu ya unajimu wala wapiga ramli.

Rais na amiri jeshi mkuu Dkt Shein alipendeza sana
 
Hujui lolote bora ukae kimya.

Unajua itifaki ya kupigiwa mizinga na kukagua gwaride au we ni wa Rumumba? buku saba

kuanzia sasa ikifikia wakati wa mizinga kupigwa tbc itakuwa inazimwa ili watu wasione
 
Mheshimiwa Raisi atabaki kuwa Amiri Jeshi Mkuu pekee nchini.General Mwamunyange ana ripoti kwa Kiwkete na sio mwingine

Kupigiwa mizinga ni ceremonial tu ,kiutendaji Shein hana mamlaka yeyyte ya kijeshi.Tuache upotoshaji

Hata kama ni ceremonial, lakini kwa protocol, hii haiko sawa! Ukweli lazima usemwe, jambo hilo halitakiwi kuachwa, Amir Jeshi mkuu ni mkuu wa Nchi, ni makosa mtu asiye na hadhi hiyo kupewa asichostahiki. Hili ni bora likasahihishwa,hata kama tunabembeleza lakini inaanza kuwa too much! Haikubaliki!
 
Watu8, sasa kipi ni kipi kati ya hiziz nukuu kutoka kwako na mwenzako? Tusaidieni, kipi ni sahihi?

Mkuu mimi nimekuwekea source bado tu umeshindwa kuamini?
 
Mkuu mimi nimekuwekea source bado tu umeshindwa kuamini?

Hata mimi niliquote post ya mdau mwingine nikawaunganisha, aliweka hadi video ya sherehe za mapinduzi za mwaka huu lkn kwa bahati mbaya nilipom quote video haikukubali, lakini nakumbuka pposti yake ni namba 25.
 
Shein atapigiwa mizinga hata 42, ataitwa amiri jeshi mkuu, ataitwa mkuu wa nchi lakini mwisho wa siku atabaki kuwa kama mkuu wa mkoa wa singida. maelekezo yote yanatoka magogoni.
waache wajipe moyo kuwa wanajitawala lakini sote twajua Tanganyika ndio mabwana zao.
 
Hata mimi niliquote post ya mdau mwingine nikawaunganisha, aliweka hadi video ya sherehe za mapinduzi za mwaka huu lkn kwa bahati mbaya nilipom quote video haikukubali, lakini nakumbuka pposti yake ni namba 25.

Rais wa JMT ana heshima yake hata kama si mgeni mualikwa...

Katika hizo posts naona kama Bw. Shein anakagua magwaride kitu ambacho ni sahihi kwa kuwa ndiye mkuu wa serikali ya mapinduzi na dhifa inahusu sherehe za kumbukumbu ya mapinduzi
 
Jana Jaji Warioba amaetoa majibu kuwa wakati wakikiusanya maoni ya mabadiliko ya Katiba, Wanajeshi walimwambia wamechoka kupiga mizinga 21 kwa marais wawili katika nchi moja.
 
Back
Top Bottom