Ni kweli Mwanaume ni Zaidi ya Mwanamke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kweli Mwanaume ni Zaidi ya Mwanamke?

Discussion in 'JF Doctor' started by ndyoko, Aug 15, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kuna hili jambo niliambiwa kitambo, ila leo naomba tulijadili. Natanguliza maombi yangu ya msamaha kwa nitakao wakwaza. Jambo lenyewe ni kwamba, jamaa liidai kwamba pindi mimba inapotunga ndani ya mwili wa mwanamke iwe ya mtoto wa kiume au kike, wote mwanzoni wanakuwa na jinsi ya kike-hii inamaanisha kuwa hata yule atakayekuja kuwa wa kiume, huwa anakuwa na jinsi zote mbili, kike na kiume. Tofauti ni kwamba kadiri muda unavyokwenda mimba itakayokuja kuwa ya mtoto wa kiume hupigana kufa na kupona kuhakikisaha kuwa sehemu ya kike inapotea na kubakia na sehemu kiume tu.

  Ili kuhakikisha hilo alilolisema, alituambia kuwa tuchunguze kwa watoto wote wa kiume, kati ya sehemu ya haja kubwa na kile 'kichwa' cha pili kuna kitu kama ngozi hivi ambayo ni kama kovu. Jamaa akadai kuwa watoto wote wa kiume hata wanaume wote wazima wanalo hilo kovu. Mdunguaji hebu jicheki utaona hiyo kitu. Na wakina mama jaribuni kuwaangalia watoto wenu wa kiume (wodogo wakubwa kubwa watawapiga) mtaona hako kakovu kadogo kati ya 'anus' na 'penis'. Narudia hii ni kwa wanaume wote- wakubwa na watoto. Katika kukamilisha hoja yake akadai kuwa hiyo ndio ilikuwa sehemu ya jinsi ya kike ambayo ilipotezwa na kubakia ya kiume tu.

  Kutokana na hilo nililolieleza hapo juu, jamaa akadai kwamba, ujio wa mtoto wa kiume ni matokeo ya jitihada za 'embryo' kukataa kuwa mwanamke. Akadai kuwa ujio wa mwanaume duniani ni matokeo ya jitihada binafsi za mhusika kukataa kuwa mwanamke. Kwa kuwa mwanaume alishaanza misele ya kuwa aggresive katika kuwa kwake mwanaume tangu tumboni, ndiyo sababu wanaume wengi hadi leo, narudia wanaume wengi hadi leo, wameendelea kuwa aggressive kwenye mambo yao kuliko wanawake wengi. Na kwamba wanaume wote lazima tutembee kifua mbele kwa kuwa kuwa kwetu wanaume ni matokeo ya struggle setu binafsi kukataa kuwa wanawake.

  Akahitimisha kuwa tofauti hii ya struggle kabla hata hatujazaliwa ndio chanzo cha hali iliyopo sasa duniani kote ya wanaume kuendelea kuwa 'the strongest gender' under the sun. Jamani nimeeleza kile nilichoambwa, naomba msininyonge wala kunilaani.

  TUPO PAMOJA DAIMA, MPAKA MWISHO WA DAHARI!!!!!!!!!!!!!
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Mkuu huyo jamaa yako alieleza lolote kuhusu hawa Ma-aggressive wenzetu ambao huamua kuwa na tabia za kike? Je ilikuwaje basi wanashindwa kuendelea kuwa aggressive mpaka kufikia kukubali au kujigeuza/kugeuzwa kuwa wanawake? Pili, huo uchunguzi wa jamaa yako ulikupatia na majibu yeyote kuhusu ma-shemale?
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hapo mi mgeni so no coment
   
 4. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  duh! hii kali.
   
 5. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Ngoja tusubirie ukweli kwa wataalam,ila hiyo kitu kwangu hamna
   
 6. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,333
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  kuzaliwa mwanaume ni toleo maalum
   
 7. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  huyo jamaa nadhani kajenga hoja tu huku akishabihisha maumbile ya m.mke na m.mme.hiyo haina tofauti na ile story ya kwamba watu weusi walitokana na nyani.hata mimi kuna jamaa aliwahi kuniambia **** binadamu wote huzaliwa wakiwa waislam kwamba mtoto anapokuwa tumboni huwa anafanya ibada sana pia huwa amefunga swala huku ameinamisha kichwa chake chini kama ishara ya utii mbeke ya mugu.na kabla hajatoka huwa anakumbushwa kusali sana atakapo kuwa duniani tena huonyeshwa pepo kama makazi yake iwapo atakuwa ana sali,moto nao huonyeswa kama atamuasi mungu.ndiyo maana mtoto anapozaliwa tu lazima alie kwanza hulia kwa kukumbuka kwamba sasa kaingia duniani sehemu ambayo ina kila aina ya mazambi anapojiuliza na kukumbuka ule moto aliyo onyeshwa akiwa tumboni hapo hapo hulia.
   
Loading...