Ni kweli Mkapa alianzisha TRA?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,885
Ni vizuri kukawepo na ukweli zinapoandikwa historia za Viongozi wetu na historia ya nchi yetu Kwa ujumla..

Nimesikia mara kadhaa watu wakisema Rais Magufuli kajenga daraja la Kigambon na nabaki na maswali mengi..

Sasa hili la Mkapa kuunda TRA pia linanitatiza sana ..kivipi?

Nimemsikia mara kadhaa Rais mstaafu Kikwete akisema aliunda TRA alipokuwa waziri wa fedha wakati Rais ni Mwinyi..
Na alisema alienda Uganda nafikiri kupata uzoefu wao WA URA..na wapo waliokuwa wanamshauri vinginenevyo..

Ifahamike wakati Rais Mwinyi anamteua Kikwete kuwa waziri wa Fedha hata uchaguzi wa ndani wa CCM wa mgombea ulikuwa bado na hakuna aliekuwa anajua kama Mkapa au anyone atakuja kuwa Rais wa Tanzania miezi michache baadae...

Binafsi nafikiri kuna 'watu wanaostahili' credit za kuunda TRA lakini hawatajwi..
Hata Kikwete probably alikuta 'process' IPO tayari akafanya kuiongeza nguvu..
Na Mkapa alipokuwa Rais miezi michache later 'ikawa rasmi'...

Kusema Mkapa aliunda TRA sio sawa..
Na hata Kusema Kikwete aliunda TRA pia sio Sahihi..labda tuseme Mwinyi? Au
'wataaalam wetu wa wizara ya Fedha'
Ambao hawatajwi na kuacha wanasiasa kubeba credits ambazo sio zao?..

Ni Sawa na kusema Mkapa alianzisha DSE
Au UTT wakati nimewahi msikia Mtaalam mbobezi na first CEO wa DSE na first CEO wa UTT akisema alikuwa anaenda waeleza
Viongozi kuhusu UTT hawaelewi kitu..wanamshangaa..hata DSE walikuwa wanasema nchi bado haipo tayari...

Sijui Yuko wapi Hamis Kibola Leo hii na kama kuna mtu hata anamtaja kama
'The brain behind DSE na UTT....

Swali linabaki pale pale je Mkapa ndo aliunda TRA?
 
Kulingana na kitabu cha Mzee Mtei, from goatherd to Governor'' uundwaji wa TRA ilikuwa ni wazo lake, aliishauri Serikali ya JMTZ wakati akiwa kati ya IMF au WB sikumbuki sawa sawa, hivyo ni Rais gani aliyetekeleza nimesahau inabidi nikisome tena kama siyo Mkapa basi ni Mwinyi, lakini kulingana na Mzee Mtei (kwenye kitabu chake) waliunda TRA kwa kufwata/iga mfano wa Kenya na KRA.
 
Kaka Marehemu hupewa sifa zote safi hata asizostahili....zile mbaya zake kimyaaa....

Watu wamebakia vilema & wajane Kule Zanzibar nani anasema?
 
Uanzishwaji wa TRA mchakato ulianza kipindi cha Rais Mwinyi kama moja ya masharti ya Structural Adjustment Policy ambayo Serikali ya Tanzania ilishauriwa na The Breton Woods Institutions (IMF & WB) kwamba kuwe na chombo kimoja kilichoanzishwa kisheria, na huru (Autonomous) ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia ukusanywaji wa mapato yote nchini.

Mambo mengi ya kuzifanya taasisi zilikuwepo kipindi cha Rais Mwinyi kuwa ni za kisasa ili kuendana na mabadiliko ya soko huria yalifanywa chini ya Mzee Mkapa: Vyombo vingi vilikuwepo japo aidha vilikuwa chini ya Wizara fulani na siyo huru kama ilivyo leo. Japo lazima tukubali kwamba Mzee Mkapa ana sehemu yake kusukuma hili kufanyika ili aweze kuendana na mahitaji ya Uchumi wa soko huria ambao yeye aliauamini sana.

Ukiangalia vizuri kipindi hiki ndiyo yalifanyika mabadiliko makubwa sana kwenye sheria za nchi ambayo yalibadilisha muundo wa taasisi mbalimbali za kitaifa na kuzipanga upya. Sheria nyingi sana zilikuwa Revised na taasisi nyingi zikawekwa kisheria.
 
Kulingana na kitabu cha Mzee Mtei ,,from goatherd to Governor'' uundwaji wa TRA ilikuwa ni wazo lake, aliishauri Serikali ya JMTZ wakati akiwa kati ya IMF au WB sikumbuki sawa sawa, hivyo ni Raisi gani aliyetekeleza nimesahau inabidi nikisome tena kama siyo Mkapa basi ni Mwinyi, lkn kulingana na Mzee Mtei (kwenye kitabu chake) waliunda TRA kwa kufwata/iga mfano wa Kenya na KRA, ...
Siyo wazo lake, lilikuwa ni moja ya pendekezo kwenye The Structural Adjustment Program.
 
Nadhani ni Mkapa aliyeanzisha TRA! Kama unakumbuka hotuba ya Baba wa Taifa Nyerere 1995 aliwahi kuiponda serikali ya Mwinyi kuwa ni corrupt! Nchi zote ambazo ni corrupt HAZIKUSANYI KODI.
Wakati huo alikuwa akitaja sifa za mtu anayetakiwa kuwa Kiongozi wetu.Kwa hiyo ni dhahiri wakati wa Mzee Ruksa hakukuwa na ukusanyaji wa Kodi.

Baada ya Mkapa kuchaguliwa kuwa Rais ndipo TRA ilipoundwa katika kipindi chake cha Uongozi.
Niko tayari kukosolewa!
 
The Boss , credits bado zinaenda kwa BWM. Ni kweli kuwa sheria iliyounda ("establish") TRA ilipitishwa mwaka 1995 (kabla BWM hajawa Rais).

Sasa kupitishwa sheria ni jambo moja na kuitekeleza ni jambo jingine kabisa. Ukitaka kuamini hili rejea lile sakata la madawa ya kulevya la Makonda. JPM wakati anamuapisha Commissioner wa kupambana na madawa ya kulevya alisema sheria (ya kuunda Mamlaka ya kushughulikia madawa ya kulevya) ilikuwepo muda tu (tangia March 2015), lakini haikuwahi kutekelezwa mpaka mwaka 2017 (Magufuli alipomteua Commissioner General).

TRA ilianzishwa (kuanza operations) tarehe 1 July 1996 wakati BWM akiwa ndio Rais. BWM asingetaka TRA iwe, isingekua. Kwa hivyo credits zinakwenda kwake....japo conception ilianzia kwa Mzee Ruksa.

Kama tu ambavyo credits za uundaji wa Mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya itakwenda kwa JPM, ingawa conception ilianzia kwa JK.

RIP Mzee Mkapa.
 
Kulingana na kitabu cha Mzee Mtei ,,from goatherd to Governor'' uundwaji wa TRA ilikuwa ni wazo lake, aliishauri Serikali ya JMTZ wakati akiwa kati ya IMF au WB sikumbuki sawa sawa, hivyo ni Raisi gani aliyetekeleza nimesahau inabidi nikisome tena kama siyo Mkapa basi ni Mwinyi, lkn kulingana na Mzee Mtei (kwenye kitabu chake) waliunda TRA kwa kufwata/iga mfano wa Kenya na KRA, ...

Since Mtei aliwahi kuwa waziri wa fedha
Possibility ni kuwa wazo lake kama kweli lake
Lilikuwepo Tu hapo wizarani likifanyiwa kazi na
Review miaka kibao..na ndo maana naona sio Sahihi kusema Mkapa alianzisha TRA
 
Back
Top Bottom