Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,300
- 25,920
Hakuna haja ya kukumbushia utendaji wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr. Wilbrod Peter Slaa. Kila mpenda demokrasia na mfuatiliaji wa mambo ya kisiasa hapa Tanzania anajua utendaji wa Dr. Slaa alipokuwa CHADEMA na hadi kuwa gumzo ndani na nje ya CHADEMA.
Takribani miezi kumi iliyopita, Dr. Vicent Mashinji aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA. Kuna tofauti kubwa ya kiutendaji na kimuonekano kati ya Dr. Vicent Mashinji na mtangulizi wake, Dr. Slaa. Dr. Mashinji haonekani katika kutoa kauli za kichama na kadhalika.
Dr. Mashinji, kama mtendaji mkuu wa kichama pale CHADEMA, ndiye mpishi wa mikakati ya kichama na hata mtekelezaji mkuu wa maamuzi ya mamlaka za kichama. Kiukweli, Dr. Slaa alikuwa na makeke ya kutosha katika siasa za kitanzania.
Dr. Slaa alikuwa mzungumzaji, mshiriki na mthubutu katika kukitumikia chama chake. Aliiva pia kimkakati. Yawezekana katazo la mikutano ya hadhara ya kisiasa na kuhamia kwa Lowassa, ambaye binafsi namuona kama ni 'speed governor', ni sababu za kutoonekana kwa makeke ya Dr. Mashinji katika ujenzi, uenezi na uimarishaji wa chama chake?