Wadau, akiuliza maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuzagaa kwa silaha ikiwemo bastola. Lema alisema kuwa jijini Arusha, kila penye watu 100, watu 80 wanamiliki silaha ambazo huzitumia kuhatarisha usalama wa watu wengine. Amesema kuwa watu hao wengi wanamiliki silaha isivyo halali na wengine wamepewa kwa malengo yasiyojulikana.
binafsi nimetafakari sana maneno hayo ya Lema na hakika sikupata uhalisia na ndipo nilipoamua kuleta hoja hii hapa ili tudadavue kujua uhalisia wake au pengine Lema alikuwa na lengo la kujijenga kisiasa tu. watu wa Arusha naomba mtusaidie katika hili. Hapa matusi na itikadi za kisiasa tuziweke pembeni
Mkuu, inawezekana Lema hata huo utafiti hakuufanya bali ameongea kwa hisia zake tuhuu utafiti naukataa maana katika jamaa zangu wengi ninaoishi nao R ni wachache mno wenye hiyo kitu labda kama wanamiliki isivyo ,ni janga kama majanga mengine tu.
Mkuu, inawezekana Lema hata huo utafiti hakuufanya bali ameongea kwa hisia zake tu
inawezekani ni kweli maana mda si mrefu kuna mtu kapigwa ya tumbo maeneo ya soko kuu.umilikaji wa silaha huku arusha ni mkubwa sana na ndio maana matukio ya kuuana kwa risasi ni mengi mno.mkitofautiana na mtu kidogo tu,tayari maisha yako yanakuwa hatarini!
Hiyo ya man u kufungwa na watu kurusha risasi hewan mbona kali sana, Ila ni kweli umiliki wa silaa kwa arusha upo kwa hali ya juu sana, na sana ni hawa vijana wanaofanya biashara ya madini akipata kafaida ka milioni kumi na kagari(foresta) anaweka bastola pembeni.Yuko mmoja wa Sakina ashatabiwa Mawenzi na Mirembe anayo na kwenye mkesha wa mwaka mpya 2011 alipiga mtu wakati akishangilia bahati nzuri alijeruhi tu....... Kwa statistics za Lema sina uhakika!!! Ila bastola zinamilikiwa holela vijana wengi wa kitaa wanazo na ni watu wa kawaida sana, wengine ni vijana kula kulala kwa Shikamoo lakini wanazo na wanamiliki kihalali!! Wengine hata busara za kumiliki manati hawana, lakini wana bastola ..... Serikali isilichukulie kwa wepesi hili suala kweli Arusha kuna umiliki "holela" wa silaha za moto.
Man Utd kafungwa watu wanapiga risasi hewani!!!! Wanatunyima raha Aaaaahkkkk!!!