Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,367
Wadau, akiuliza maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alitaka kujua mikakati ya serikali katika kuzagaa kwa silaha ikiwemo bastola. Lema alisema kuwa jijini Arusha, kila penye watu 100, watu 80 wanamiliki silaha ambazo huzitumia kuhatarisha usalama wa watu wengine. Amesema kuwa watu hao wengi wanamiliki silaha isivyo halali na wengine wamepewa kwa malengo yasiyojulikana.
binafsi nimetafakari sana maneno hayo ya Lema na hakika sikupata uhalisia na ndipo nilipoamua kuleta hoja hii hapa ili tudadavue kujua uhalisia wake au pengine Lema alikuwa na lengo la kujijenga kisiasa tu. watu wa Arusha naomba mtusaidie katika hili. Hapa matusi na itikadi za kisiasa tuziweke pembeni