Tungefikiria sayansi ni ushirikina yasingegundulika yote haya, leo unajua kama alasiri saa kumi kuna mvua, basi huu nao ni ushirikiana? Baadhi ya watoto wanapozaliwa kuna mambo fulani yasiyo ya kawaida kuwepo au mtoto kuonyesha ishara zisizo za kawaida ingawa ni ishara za wakunga na wazazi lakini kuna kitu kinachoashiria upekee wa mtoto katika maisha yake ndani ya jamii inayomzunguka au dunia.
Hata maskini Lazaro alipokuwa anahangaika kuokota masazo ya tajiri yule aliona ni haki yake. Siku alipokufa Lazaro, tajiri naye yakamkuta yayo baada ya maskini Lazamo kuwa kifuani mwa Abraham, tajiri alivyotaabika kule ahera na kutamani Abraham amtume lazaro walao amtilie tone la maji ndani ya kinywa chake kukata kiu. Alikatishwa tamaa kwamba kati yao hakupitiki na yule tajiri aliashiria basi Lazaro afufuke akawatahadharishe ndugu zake wasifanya aliyomfanyia Lazaro.
Jibu lililomkatisha tamaa ni kwamba, wapo manabii huko, wasipowasikiliza hao, hata aliyefufuka kutoka kuzimu hatasikilizwa pia.
Kwa nini wengine huwa wazito kuukubali ujumbe wa wazi? Kazi kwelikweli.
inavyosemekana
Huo ushirikina ndio umetufikisha hapa tulipo. Badala ya kumtegemea Mungu watu watategemea wadudu na wachawi. Inavyoelekea huyo kaka kuona ni pepo tu anawachanganya. Hatuhitaji sijui mdudu /mnyama kututabiria mambo wakati tuna watumishi wa Mungu kila mahali.
Mapokea ya mnyama Kakakuona ni kuonekana kwake kwa nadra mno isivyo kawaia kitu ambacho huashiria jambo fulani katika jamii kutokea. Tofauti ya mtazamo wako ni kwamba huyu kakakuona achukuliwe awe anatabiri kila siku jambo ambalo umekwenda kinyume cha maana ya tukio hilo. Tafsiri ya kuonekana kwa nadra kakakuona linatafsiriwa hivyo kutokana na pale anapotokea pasipotegemewa na wenye uzoefu wa kumsoma hupata tafsiri ya kuashiria kitu au jambo fulani kuhusianisha na jamii.
Kwamba afugwe haita leta maana tena kwa vile akifugwa hatatokea kwa bahati ya pekee akama inavyotokea bali ni kuonekana kila siku kitu ambacho hakitatuletea tafsiri kadiri ya ishara za nyakati alizotuandalia Muumba wetu. Jaribu Sabayi kukuza kipaji chako cha critical thinking. Thanks.
Naona ameonekana DSM na anaoneshwa kwenye taarifa ya habari ya Clouds Tv. Kuna watu uwa wanaamini kwamba ana uwezo wa kutabiri je ni kweli ana uwezo huo?
Hivi Kakakuona ndiyo "Coyote" kwa lugha ya wenzetu?
huyu mdudu ni muhimu sana na kuonekana kwake ni mara 1 ktk miaka zaidi ya 10, huwa anatumika kama mtabiri i.e anawekewa unga, bunduki etc akichagua bunduki ujue hali ya amani itakuwa tete na akichagua unga basi ujue kuna njaa kubwa inakuja,,, na pia kipande cha gamba lake kilikuwa kikiuzwa kwa bei mbaya sana kikiaminika kumletea mtu bahati anapotembea nacho, biashara, siasa etc
Nafikiri ni Pangolin.
mbona unachanganya habari?!, kama unakemea utabiri wa kakakuona kemea pia na unajimu wa hao viongozi wako wa dini maana nao ni viumbe kama alivyo huyo mnyama.