Ni kweli Diamond na Zari Wanataka Kuachana? Ni kweli Diamond kahamishia Majeshi kwa Lyn?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Kinachoendelea sahizi instagram ni Mtifuano na ukorochoaji wa Maisha ya watu! Watu wapo busy,watu wapo katika pirika pirika za kutafuta ukweli kujua nini kinacho endelea kati ya Zari na Diamond na Diamond na Video queen wa Kwetu' Mama Diamond na mkwe wake na mawifi mtu!

Kama unavojua wabongo Umbea una nguvu kuliko Ripoti ya CAG insta kumechafuka.....Mama Diamond alianza kwa kufuta picha zote alizo post za Zari watu wakasema Mmmmmmmmh kuna kitu hapa,(mimi sidhani kama kufuta picha za mtu ni kitu kibaya lakini hakufuta za zari tuu mbona hata za wengine alifuta akaacha za Tiffa na Rommy tuu)

Wafuatiliaji wa mambo hawakuishia hapo wakasema Esma dada wa Diamond Ka muunfollow Zari (sina uhakika lakini Kwa usawahili wa huyu Dada nilishangaa kuona anapatana na Zari huyu ni mswahili mno na Diamond asipo kuwa Makini atamponza kwa uswahili wake)

Watu wakaendelea na story kwanini Zari hakutoa shout out kwa wimbo wa Raymond video ya Kwetu wakaguna wakasemaaa mmmmmmmmh hapa kuna kitu huenda Diamond anatoka na yule video queen wa hio video(Sioni tatizo tukumbuke Video ilitoka wakiwa bsy ulaya hata Mama Dai naye hajatoa Shout out kwenye video na hata picha alio post kuhusu hio video hamna)

Wafuatiliaji wa Mambo wakasema ishu ilianza kutokea world tour kuwa wakati wa kurudi kila mtu alipita njia yake Mama Diamond na Zari (mimi sioni Tatizo as long as Zari anaishi South Africa huenda alichukua ndege moja kwa moja hadi South na Mama Dai akaja bongo)

Juzi juzi hapa Dai na Zari wamepost picha zao wakionesha they are happy na mahusiano yao so Sidhani kama kuna kitu hicho ingawa leo bado hawajapost chochote

Kimbembe ni pale Mama Dai alipo like picha ya Video queen(anaesadikika kutoka na Dai)
d0fd828a7c769b9caf5121a3d96f9b61.jpg

Watu wakaendelea kupagawa na kuona kama yasemwayo yanaukweli baada ya video queen kupost picha hizi (Lakini ameshazifuta ila wajanja waliwahi)
66a3806a8a362c47ab8f4a3c38a0c43e.jpg
49d19880d7e8b9a9f1ca9f52d87bca28.jpg

Sasa Hatujui hii simema wapi itaishia lakini tuwe hapa hapa tutajua kila kitu! As long as hii ni JF! LENGO LA THREAD HII NI KUTAKA MWANA JF USIYUMBISHWE KUJUA NINI NI NINI?

MTAZAMO:
Kama Dai atakuwa kweli kaamua kuachana na Zari (Sidhani kama kitatokea) na kuja Kutoka na Video queen kwanza atakuwa amejishushia heshima yake hata kama Mama Dai ndo anampenda huyo video queen!, pili Dai atakufa Maskini maana wabongo huyo video queen atahamishia hadi ukoo wake pale white house sasa itakuwa bila bila Dai yupo na kijiji chake na huyu yupo na Kijiji chake!

Kingine ni kuwa Dai akae na dada zake na Mama ake awambie wapunguze uswahili kwa Zari! Utakuja kumponza Esma ni mswahili sana bora hata Halima! Esma yake yanamshinda anataka kuvuruga ya watu,pia Mama ake hata kama Insta kaikutia ukubwani Apunguze uswahili mwanae ashakuwa super star,yeye atulie afaidi matunda basi uswahili wakumuamlia atoke na nani ni ujinga na atampotezea mwanae Heshima!

Pamoja na kuwa zari ni mvumilivu namshauri Dai apunguze watu wakukaa nae Nyumbani kwake ana nyumba nyingi sio kila mtu lazima akae nae hata kama huruma sasa zinazidi! Ile ni nyumba yake na mke wake ndo maana ya mke,mama mkwe awe na nyumba yake,dada zake pia na ndugu wengine zari atakuwa anakosa uhuru ajifunze mbna Zari haleti ndugu zake! Ndoa ni kitu nyeti sana!

Napinga kwa asilimia 80% kuwa Dai anatka kumtosa Zari kwenda kwa video queen mtoto! Lakini ngoja tuone hii ngoma itaishia wapi

Reality Tv show ya Daimond huenda ikawa inatafutiwa Kiki kwa njia hii,mama Dai wabongo asha wajua kuwa akitoa Show yake hyo itauza maana wengi wanapenda umbea so huenda ni kiki

Mchezo huu hauhitaji hasira
 
Kama mwanamke angekuwa anasingiziwa mtoto mimi ningeshauri familia hii iwe imesingiziwa mtoto Dai ndio wazazi wake halisi wawe Kenya au SA lakini ni kama eeh ni kama tu ingewezekana.
#wabongo nuksi
 
Diamond hakufaa kuzaliwa Tandale.. Ni kama bahati mbaya, yani tandale kuna uswahili mwingi sana. Sijui Diamond akili alizitoaga wapi utadhani hajatokea tandale.

Huyo Esma na Mama Dai tatizo sio wao tatizo ni Tandale. Mtu mwenye hekma awezi kuishi wanavyoishi kina mama Chibu yani wanakaba mbaya.

Yani mama nae kwenye WCB yumo.

Mama mwanao ndio anakupenda ila inabidi ujiongeze wewe kila mtu atakuwa mbaya sio kweli bhana.

Mbona Queen anajiongeza ajakaba kihiivyo yupo busy kivyake anajihusisha inapobidi.
 
Mimi I doubt kama Diamond can take a step backwards-since amekuwa na Zari,Diamond amekuwa another level-he can play dirty(za Tandale) na he can mix na elites. Ni vigumu kwa mtu asiemjua Diamond,kuamini kwamba jamaa ni mbongo-ka raise game la bongo flavor to another level.Leo hii haya yote ayatupe sababu ya a nobody-no way. Somebody wrote eti mama yake anakaba mpaka mpira wa penalt eti na yeye yupo WCB-its time huyu mama akae pembeni,trying to influence Diamond is beyond her,sana sana she will bring the house down.All in all nadhani Diamond na washauri wake wamegundua weakness ya Watanzania hence wanatayarisha groundwork ya episode yao ya reality show. Zari must be laughing her head off,thinking how easy it is to take money off bongolala,s
 
Sidhani kama Daimond ata kuwa na ujinga usio mithilika wa kujua kutafuta pesa halafu mahusiano yake na faragha yake amuachie Mama yake na Dada yake ndio wawe waamuzi juu ya aishi na nani kwa kadri wanavyo taka wao,Kwa uwezo alio nao angeweza kuwatafutia makazi, na kama mtu mzima ana stahili kabisa kuwa huru vinginevyo ame alika vita tu, Mama yake sio mzee kiasi hicho na kumpenda mama yake si lazima aishi naye aache utoto sasa na mama ndio hivyo hana maadili asinge ikubali hali hiyo,hata kama wakimtafutia mwingine haita kuwa suluhu na bado atakuwa kashikwa kichwa hatakuwa huru.
 
Juzi juzi hapa Dai na Zari wamepost picha zao wakionesha they are happy na mahusiano yao so Sidhani kama kuna kitu hicho ingawa leo
Unajua ipo hivi: UKISIKIA Celeb couple/bond ipo kwenye ugomvi au UKASIKIA hali si shwari kati yao... bila kujali ikiwa habari hizo ni kweli au si kweli lakini wakaamua ku-post picha wakiwa pamoja(bila kujali picha hizo zimepigwa lini) ; hapo fahamu wanatoa ujumbe kwamba "Acheni kukuza mambo...!"

Kwamba hata kama ni kweli kuna conflict kati yao basi ni conflict sawa na conflict ya couple nyingine yoyote ile ambayo kuwapo kwa conflict hiyo wala haina maana kwamba watu ndo wanataka kugawana mbao za mashua iliyokumbwa na msuko suko!
 
Wewe mwenyewe mbea. Jamani hivi mkoje huko Dar? Utakuta hujaingiza hata mia mbili lkn kutwa kufuatilia maisha ya watu.
swala si Dar wakoje, swala ni nani anazungumziwa. huyu ni star wa Africa. akizungumziwa sio kwamba watu hawana kazi ila ni mtu maarufu, kila step ya maisha yake lazima ifuatiliwe kam huko uliko sijui wapi wanavyofuatilia maisha ya kina Kardashian, Beyoncé na JayZ wake, na wengine wengi wa namna hiyo. hapa sio umbea wala nini ila hali halisi.
kama hujui uchangie nini maana huwajui soma kaa kimya maana wewe ndio mbea usojua Star wa Tanzania na Africa kwa ujumla ni nani.
 
Tafadhari sana dada star kwangu ni mama yangu tu basi.
 
Sidhani kama Daimond ata kuwa na ujinga usio mithilika wa kujua kutafuta pesa halafu mahusiano yake na faragha yake amuachie Mama yake na Dada yake ndio wawe waamuzi juu ya aishi na nani kwa kadri wanavyo taka wao,Kwa uwezo alio nao angeweza kuwatafutia makazi, na kama mtu mzima ana stahili kabisa kuwa huru vinginevyo ame alika vita tu, Mama yake sio mzee kiasi hicho na kumpenda mama yake si lazima aishi naye aache utoto sasa na mama ndio hivyo hana maadili asinge ikubali hali hiyo,hata kama wakimtafutia mwingine haita kuwa suluhu na bado atakuwa kashikwa kichwa hatakuwa huru.

Tatizo la na Dai ni kulundika ndugu nyumbani kwake wakati ana uwezo wa kuwaweka sehemu nyingine ambayo ni nzuri pia. Anashindwa kujua kua maisha ni mume, mke na watoto na sio mume, mke, watoto, mama, dada na wengine.
Na hao ndugu wenyewe basi waswahili kupita kiasi. Dai, amejitahidi sana ku cope na hali ya u celeb wake, kiasi uswahili umemtoka ila kashindwa kuweka mbali ndugu. hawa wata cost ndoa yake iwapo atataka kumuoa Zari. I wish apate message imuingie, amsomeshe mama aelewe. mama akielewa na ndugu wengine wataondoka. maana sijui mama anahangaika nini kukaa na mtoto na mkwe nyumba moja wakati hawana shida hata moja.
Hata kama amemlea Dai kwa shida sana lakini sio mzazi pekee alipitia hizo shida. wapo waliolea kwa shida zaidi yake lakini hawagandi watoto kiasi hicho kwa kisingizio kua kapata shida. ampe mwanae uhuru na familia yake. Hata hivyo Zari namsifu ana moyo hasa.
 
Hii ndio Reasoning Capasity ya Watu wa Daslam...Full Umbea...Ule uchunguzi wa yule jamaa aliyesema 90% ya maongezi ya watanzania ni Pumba tupu nadhani angesema asilimia kubwa ya Maongezi ya watu wa Dar ni Pumba tupu...
 
Tatizo la na Dai ni kulundika ndugu nyumbani kwake wakati ana uwezo wa kuwaweka sehemu nyingine ambayo ni nzuri pia. Anashindwa kujua kua maisha ni mume, mke na watoto na sio mume, mke, watoto, mama, dada na wengine.
Na hao ndugu wenyewe basi waswahili kupita kiasi. Dai, amejitahidi sana ku cope na hali ya u celeb wake, kiasi uswahili umemtoka ila kashindwa kuweka mbali ndugu. hawa wata cost ndoa yake iwapo atataka kumuoa Zari. I wish apate message imuingie, amsomeshe mama aelewe. mama akielewa na ndugu wengine wataondoka. maana sijui mama anahangaika nini kukaa na mtoto na mkwe nyumba moja wakati hawana shida hata moja.
Hata kama amemlea Dai kwa shida sana lakini sio mzazi pekee alipitia hizo shida. wapo waliolea kwa shida zaidi yake lakini hawagandi watoto kiasi hicho kwa kisingizio kua kapata shida. ampe mwanae uhuru na familia yake. Hata hivyo Zari namsifu ana moyo hasa.
Hapo umenena Diamond katika uswahili ameshajikomboa tatizo ni mama na ndugu wanaona motto wao anadhulumiwa-hawajui kafikaje hapo
 
Nimegundua kitu.

Kwa idadi ya wapumbavu waliopo nchi hii, ni rahisi sana kuwafanya hao wapumbavu wakuzungumzie.

Ingia tu huko Instagram na futa picha ya mtu, penda picha ya yule, andika neno au maneno yasiyo eleweka na kadhalika na utawachota karibu wapumbavu wote.

Wewe ndo utakuwa gumzo la jiji.
 
Back
Top Bottom