Ni kweli CHADEMA itanufaika na msaada wa mafisadi 2020?

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,505
Reaction score
16,006
Kumekuwa ni shangwe miongoni mwa wanachadema wengi wakiamini kuwa hatua za serikali na CCM kuwaondosha mafisadi kuwa watakuwa na msaada mkubwa kukiwezesha chama hicho kuwa na ushawishi kwa wapiga kura na hatimaye kushika dola.

Ikumbukwe uwepo wa mafisadi kwa miaka takribani kumi ulipelekea CCM kushuka umaarufu kwa wananchi ambao kimsingi waliitaka CCM iwaondoe ili kurudisha imani.

Je ni kweli sasa wananchi wamewasahau watu hawa waliopewa jina la ''magamba'' na CCM?..ikumbukwe si kila maovu ya kisiasa hupelekwa mahakamani bali mara nyingi mahakama ya mafisadi ni wananchi kupitia sanduku la kura.

Nawatakia CHADEMA kila laheri katika mpango wao wa kuwatumia wahalifu,wezi na mafisadi katika ujenzi wa chama imara kitakacholeta ushindani nchini.

Nawasilisha.
 
Itasaidia ...maana chadema imeacha ajenda yao ya kupinga ufisad
 
Tatizo sio mafisadi tatizo hapa ni mfumo unaozalisha mafisadi.
Usikimbilie kuangalia tukio kabla ya kuangalia chanzo cha tukio.
 
yaani mbona hapo ndio safi, kwani kama ulikuwa mchafu ukafanya usafi wa kutosha kisha ukatupa takataka nje jirani akaja akazoa akapeleka nyumbani kwake wakati kila siku unaomba mungu amuondoe jirani yako msumbufu,acha maradhi yamuondoe harafu wewe ufanye sherehe kushineh.
 
KWA hiyo unataka kutuaminisha kuwa CCM ni CHUO cha mafisadi? Au watatoka wapi? Tatizo ni mfumo wa maisha tulio nao wa kuamini tunasoma ili tuajiriwe na si vinginevyo, wewe unavunja fito kwako unajenga (kufikirika) Chadema bila kujua, think twice.
 
Hivi watanzania wengine mnakula nini?! 'Uwepo wa mafisadi kwa miaka takribani kumi...'!!! Yaani ufisadi kama EPA, IPTL, MEREMETA, KAGODA, RADA...nk siyo tatizo tena!
Na kwa hiyo sasa ccm na serikali yake wanawatimua wahusika wa ESCROW, LUGUMI, KIVUKO chakavu cha DAR-BAGAMOYO, nk?!
Kama vipi waambieni wasisahau kuna mafisadi wa kura za raia wa nchi hii kila kunapokuwa na uchaguzi...
 
Tatizo sio mafisadi tatizo hapa ni mfumo unaozalisha mafisadi.
Usikimbilie kuangalia tukio kabla ya kuangalia chanzo cha tukio.
Na huo mfumo ndio Rais Magufuli anapambana nao. Hii vita si ya kitoto. Magufuli anaelewa hivyo na ndio maana anawalia ganja
 
Kuna ukweli hapo mbona Lugumi ni kama imepotezewa kiaina Funika kombe mwanaharamu apite.
 
Back
Top Bottom