Ni kweli CCM Imekufanya kuwa Maskini au ni Mwenendo Wako tu Wamaisha?

Misss Chuga

Senior Member
Oct 6, 2021
181
327
Habari za mda huu!

Naenda kwenye mada moja kwa moja.

Babu zetu walisema umaskini wao waliupata kutokana na wakolon. Wazee wetu umaskini waliupata kutokana na sera za Tanu na Mfumo wa Alioutumia Nyerere wa ujamaa!

Kijana wa leo Tanzania anasema yeye ni maskini pia anamaisha magumu sababu ccm ipo madarakani pia serikali haimwangalii.

Ni kweli umaskini wetu unaletwa na utawala na mfumo wake, au ni mwenendo tu wa maisha ya mtu?
 
Mimi naona ni mimi mwenyewe tu akili haijachangamka...wala sio ccm ingawa ccm ingeamua kumfanikisha kijana wa leo pia inawezekana
 
Kenya, uganda, burundi, congo, malawi kote huko kuna CCM au hakuna maskini?

Hizo ni siasa mtu mmoja ambaye anaweza kukutoa hapo ulipo nenda kasimame kwenye kioo utamuona.
 
Serikali ipo pale ili tuitupie lawama kwa kila baya linalotupata sisi kama wananchi wake, whether wao ndio wamesababisha au laa.
 
Mfumo unotokana na siasa ya Nchi unasababisha watu wengi kuwa masikini,but Watu wakiamua wanaweza badili mfumo mzima wa kisiasa na ukaleta mabadikiko mabadikiko ya kiuchumi na kijamii.
 
nani anayeilaumu serikali kwa umaskini wake? nnachojua wananchi tunailaumu serikali kwa kushindwa kuprovide zile public goods kwa ufanisi kwa miaka yote 60 ya uhuru.

Sasa wewe mke wa mkuu wa wiraya kisarawe sijui umendika nini sasa hapo.
 
nani anayeilaumu serikali kwa umaskini wake? nnachojua wananchi tunailaumu serikali kwa kushindwa kuprovide zile public goods kwa ufanisi kwa miaka yote 60 ya uhuru. sasa wewe mke wa mkuu wa wiraya kisarawe sijui umendika nini sasa hapo.
Nilichoandika nipo nacho sahihi sana. Kama hujakutana nao hao watu hongera zako. Watu wanalalamika sana umaskini wao umeletwa na serikali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom