Ni kwanini walevi humnunulia mtu pombe na sio chakula?

cj21125

JF-Expert Member
May 12, 2013
3,016
2,445
Mara nyingi mtu akiwa ameishiwa pesa hata ya kununulia chakula na inapotokea akaomba msaada kwa rafiki zake au ndugu huambulia kununulia pombe za hela nyingi lakini kumpa hela kidogo ya kununulia chakula hawatoi. Wapo radhi kukunywesha pombe mpaka asubuhi kuliko kukununulia chakula hata kama una njaa ya siku 3.

Kwanini walevi wanafanya hivi?

Nawasilisha.
 
Kwa sababu wanathamini pombe

Wanaamini shida zako za chakula you can do something else kupata....
 
Hawajitambui tu pombe sio chai kunywa kiasi hata hivyo mlevi hatakiwi atembee na cash
 
Ni agents wa shetani, hivyo si wao bali ni shetan ndio anafanya kazi ndani yao.
 
Unakwenda kumwomba rafiki hela ya chakula mnakutana Bar atakachokupa kwanza pombe...!!
 
Mara nyingi mtu akiwa ameishiwa pesa hata ya kununulia chakula na inapotokea akaomba msaada kwa rafiki zake au ndugu huambulia kununulia pombe za hela nyingi lakini kumpa hela kidogo ya kununulia chakula hawatoi. Wapo radhi kukunywesha pombe mpaka asubuhi kuliko kukununulia chakula hata kama una njaa ya siku 3. Kwa nini walevi wanafanya hivi. Nawasilisha.

TUNAWEZA KUPATA PICHA MKUU??
 
Wewe Utakuwa si mlevi bali unasikia tu...
Wenzio tukienda tunakulaga Nyama Choma kwanza halafu vyombo vinatandazwa juu ya meza...
 
Mkuu wananunua au kunyweshwa pombe ili upate akili kubwa ya kupata mbesa ya kutosheleza mahitaji ya tumbo na starehe... so ni kama changamoto hivi ili ukitoka hapo uumize kichwa WHY jamaa anatafuna bia nyingi vile na home vijana wapishana kwenda choo??
 
Mara nyingi mtu akiwa ameishiwa pesa hata ya kununulia chakula na inapotokea akaomba msaada kwa rafiki zake au ndugu huambulia kununulia pombe za hela nyingi lakini kumpa hela kidogo ya kununulia chakula hawatoi. Wapo radhi kukunywesha pombe mpaka asubuhi kuliko kukununulia chakula hata kama una njaa ya siku 3.

Kwanini walevi wanafanya hivi?

Nawasilisha.
Bar sio hotelini
 
Back
Top Bottom