hiv positive living
Senior Member
- Jan 6, 2020
- 153
- 218
Naimani mko poa kabisa
Kiufupi tu;
- Jinsia KE
- Umri 32
- Sijazaliwa nao
- Sijawahi kutumia ARV
Niende moja kwa moja kwenye swali langu, hivi ni kwa nini kwenye jamii yetu ukishawaambia "NINA UPUNGUFU WA KINGA MWILINI " asilimia kubwa wanapatwa na taharuki, hofu, kunyanyapaliwa, kuzodolewa, kusemwa na kusimangwa, kutengwa?
Niliwahi kuulizwa swali mahali (akaniita kwa jina) kwa nini huwaambii ndugu zako hata mmoja?
Mimi: Kuwaambia ni nini?
Kwamba unaumwa?
Mimi: Naumwa nini?
Ukimwi
Mimi: Mimi mbona siumwi?
Si uliniambia una Ukimwi
Mimi: Ndiyo, ila sikukuambia ninaumwa. Bali tu nina Upungufu Wa Kinga Mwilini hivyo nakula mlo sahihi, kwa wakati sahihi ili kinga zangu zisishuke basi mimi siumwi.
Kwani tangu umenifahamu mwaka wa 10 huu (kipindi ananiuliza) umewahi kuniona ninaumwa nini ?
Akabaki ameduwaa tu!
Wapendwa, upungufu wa kinga si ugonjwa, kwanza jua hilo
Sema tu familia zetu ukishajulikana, utahukumiwa kwa kila neno na kila kauli
Sasa ingekuwa si unyanyapaa na mengine yanayoendana na hayo ningeweka hata picha
Yaani wewe mwenye lishe mbovu ndio ungejiona unaumwa sasa
Kwa leo niishie hapa! Nikutie moyo tu wewe mwenye upungufu wa kinga, pandisha kinga zako wewe huumwi,
Mimi si mwandishi mzuri sana hivyo napokosea msipashikilie sana
Nawapenda na wenye unyanyapaa n.k mbadilike
Sent using Jamii Forums mobile app