Upendeleo katika Ulipaji Malimbikizo ya Mishahara ya Watumishi wa Umma

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,053
33,906
Habarini Wadau.

Ninaandika jambo ambalo nimelifanyia Utafiti wa kutosha na kujiridhisha kuwa Ofisi ya Utumishi ngazi ya Taifa & Hazina Taifa wana uzembe mkubwa na Upendeleo wa kujuana katika kuwalipa Watumishi wa Umma Malimbikizo ya mishahara yao.

Wanafanya hivi kulingana na matakwa yao na sio kwa kuzingatia waliotangulia kujaza form za Arrears.

Mathalan, kuna Watumishi wa Bodi ya Takwimu wilayani na mikoani wanadai mishahara walioifanyia kazi bila kulipwa na walishajaza form za Arrears na kuattach kila walichohitajika kuattach tangu miaka ya 2017-2019 hawajalipwa pesa zao.

Waalimu pia vivyohivyo, wapo wenye madai ya miaka ya nyuma huko na wamekamilisha taratibu zote hawajalipwa...ilihali wapo waliojaza form mwaka huu huu mwanzoni tayari wamelipwa.

Katika kufuatilia na kuuliza kuna A.Utumishi mmoja Wilaya, anajibu kuwa

''Kama una Mtu kule Utumishi chonga nae akusaidie''

Je, kazi yao wao ni IPI? imefikia mahali ni mpaka Mtumishi apitie njia hizo zinazoshawishi Rushwa ndio asaidike?

Kwanini serikali isishughulike na hawa watu?
 
Hii sera ya kila mtu kulamba asali kwa urefu wa kamba yake italeta maumivu makubwa sana kwa taifa.
 

Mama Anaupiga Mwingi Sana

Adera Kaa Mguu Sawa Umetajwa Kwenye JF Ujue Unalo

 
Back
Top Bottom