DOKEZO Ni kwanini mpaka leo hakuna barabara ya lami inayounganisha Arusha na mikoa ya karibu Mwanza na Mara, usafiri ni wa kuzunguka mikoa mingine

DOKEZO Ni kwanini mpaka leo hakuna barabara ya lami inayounganisha Arusha na mikoa ya karibu Mwanza na Mara, usafiri ni wa kuzunguka mikoa mingine

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,455
Kisingizio hakiwezi kuwa mbuga kwani kuna mbuga nyingine zenye barabara za lami kama Mikumi.

Kisingizio si lazima kuwa ikolojia au kusema mbuga ni urithi wa dunia, ingawa hayo ni kweli. Hata hivyo, Watanzania wanahitaji usafiri wa haraka na wa gharama nafuu, huku wakifurahia mandhari ya kipekee. Ikiwa Mikumi imefanikiwa, hakuna sababu Serengeti isiwezekane,

safari ya Mwanza - Arusha ina abiria wengi sana, vivyo hivyo na ile ya Arusha - Mara. Magari mengi huzunguka mikoa mingi ya pembeni jambo linaloongeza gharama ya nauli, muda wa safari na uchovu wakati mikoa hii ipo kwa umbali mfupi na ingeweza kuwa na huduma bora zaidi za usafiri kama barabara ya lami ingejengwa.

1758024852442.png
 
Hiyo hoja ya Mbunga sio uongo ni kweli, Ikolojia ya mbuga za wanyama za North corridor ina watizamaji wengi kuliko huko Mikumi, Serengeti ni hifadhi yenye hadhi ya urithi wa Dunia. Hata kama ipo nchini kwako ukitaka kufanya ujenzi mkubwa wa Barabara wenye nguvu wataanza nongwa hapo kama nongwa zilizofanyika kwenye Bwawa la Nyerere na Bomba la mafuta, lakini miaka ya mbeleni nafikiri watatengeneza barabara ya kiwango cha Rami
 
Brother hao watu waliofungua kesi wapo backed up na wazungu ambao wapo tayari kumlalisha mtu nje kwenye mvua ili mbwa au paka alale ndani.

Highway imejengwa Mikumi mambo ya mbuga yanaendelea kama kawaida, wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa nao wanataka kuunganishwa moja kwa moja na mikoa ya kaskazini
 
Kisingizio hakiwezi kuwa mbuga kwani kuna mbuga nyingine zenye barabara za lami kama Mikumi.

safari ya Mwanza - Arusha ina abiria wengi sana, vivyo hivyo na ile ya Arusha - Mara. Magari mengi huzunguka mikoa mingi ya pembeni jambo linaloongeza gharaa ya naili, muda wa safari na uchovu, wakati mikoa hii ipo kwa umbali mfupi na ingeweza kuwa na huduma bora zaidi za usafiri kaa barabara ya lami ingejengwa.

View attachment 3473359
Hujui Dunia, ukitoa Arusha si waja kwa wagogo then what next
 
Brother hao watu waliofungua kesi wapo backed up na wazungu ambao wapo tayari kumlalisha mtu nje kwenye mvua ili mbwa au paka alale ndani.

Highway imejengwa Mikumi mambo ya mbuga yanaendelea kama kawaida
Wazungu au la si point.

Point ni barabara imejengwa au haijajengwa.

Hivi unaelewa ukishakiweka kitu kiwe cha UNESCO Heritage maana yake nini? Maana yake hicho ni kitu cha dunia nzima si kitu chako tu. Huwezi kuamua tu ujenge barabara ya lami unavyotaka katika UNESCO Heritage site.

Watanzania mnaelewa haya mambo au mnafikiri kujenga barabara hapo ni sawa na kujenga banda la uani Manzese kwa Mfuga Mbwa?
 
Bwawa la Nyerere walileta mambo yao likajengwa, sio kila kitu cha kukubali mkuu.

Watanzania wanaoishi ndani ya nchi wanahitaji hio barabara kuzidi hao wanaokuja na madarubini kuangalia wanyama kwa burudani siku chache kisha kurudi kwao.

Ila i am proud na sisi tunawaonyesha sio mazumbukuku kiasi hicho, nimesoma hio link ya pili

In March 2011, the Germany government offered funding to build an alternative road through the southern area of the park to Musoma, but the plan was shelved by the Tanzanian government.

Halafu hio rpute ipo kutoka Musoma hadi Arusha tatizo ni barabara ya vumbi na nauli ni kubwa elf 60
 
Bwawa la Nyerere walileta mambo yao likajengwa, sio kila kitu cha kukubali mkuu.

Watanzania wanaoishi ndani ya nchi wanahitaji hio barabra kuzidi hao wanaokuja na madarubini kuangalia wanyama

Ila i am proud na sisi tunawaonyesha sio mazumbukuku kiasi hicho, nimesoma hio link ya pili

In March 2011, the Germany government offered funding to build an alternative road through the southern area of the park to Musoma, but the plan was shelved by the Tanzanian government.
Watanzania wengi hawajui kuji organize kupata wanachotaka wanaishia kulialia mitandaoni kama wewe.

Wewe umeshafanya nini kwenye kusimamia jambo hili litekelezeke?
 
Watanzania hawajui kuji organize wanaishia kulialia mitandaoni kama wewe.

Wewe umeshafanya nini kwenye kusimamia jambo hili litekelezeke?
kujadili tu hivi kunahamasisha awareness na ni hatua muhimu. Hata kama hatuwezi kutekeleza moja kwa moja, kuleta uelewa kuna impact yake, ndio maana tupo humu
 
miaka ya 1990-2000 Tuliosoma Moshi Tech tulikuwa na Passport au ETD maana kutoka Moshi hadi Musoma/Mara lazima upitie Kenya au Uganda
Duh ! mkuu tiririka zaidi, mlikuwa mnapitia mikoa ipi, mnatokea wapi, nauli , changamoto, muda wa safari, n.k.
 
Ninapinga hata hotel kuendelea kujengwa Serengeti. Sasa hivi ukifika Serengeti utadhani uko Ngarenaro hasa mida ya usiku. Taa nyingi sana kiasi kwamba inawavuruga sana wanyamapori. Ikijengwa barabara ya lami watu watalazimisha kuwe na hotel za watu kula bila kusahau sehemu za kuchimba dawa. Hizo shughuli zote huwafukuza wanyama na mwishowe kuipoteza Serengeti. Shughuli za kibinadamu karibu na mbuga zimeharibu mno maisha ya wanyama.
 
miaka ya 1990-2000 Tuliosoma Moshi Tech tulikuwa na Passport au ETD maana kutoka Moshi hadi Musoma/Mara lazima upitie Kenya au Uganda
umenikumbusha enzi hizo, lazima upite Nairobi, wala siyo Moshi tech pekee, hata shule nyingi za Arusha na Manyara
 
Watanzania wanaoishi ndani ya nchi wanahitaji hio barabara kuzidi hao wanaokuja na madarubini kuangalia wanyama kwa burudani siku chache kisha kurudi kwao.
"Hao wanaokuja na madarubini" hawalipi chochote kuangalia wanyama? Kiukweli bado adui UJINGA ana nguvu mno hadi leo.
 
kujadili tu hivi kunahamasisha awareness na ni hatua muhimu. Hata kama hatuwezi kutekeleza moja kwa moja, kuleta uelewa kuna impact yake, ndio maana tupo humu
Sawa.

Lakini mnasema hivyo kila siku bila kuchukua hatua yoyote.

Unajenga awareness ili ifanye nini kama kila siku hufanyi lolote zaidi ya kujadili?

Una action plan gani? Una timeline gani? Una strategy gani?

Hilo jambo unalolitaka umelisoma vizuri na kuhakikisha uko sawa?

Unaelewa migration ya wanyama Serengeti ilivyo, inavyovutia watalii, na barabara ya lami pamoja na kuongezeka magari vitakavyoiathiri hiyo migration?

Unaelewa tofauti ya nyendo za wanyama Serengeti kulinganisha na sehemu kama Mikumi?

Unaelewa impact ya kujenga barabara kwenye migratiin hiyo? Unaelewa impact kwenye utalii kushuka kutoka kwa bad publicity ya kujenga barabara hiyo?

Unajenga barabara ili usafirishe nini? Ikiwa utalii utadoroa kwa bad publicity utadoroa kwa kiasi gani na unachotaka kusafirisha kitafidia mapungufu yatakayotokana na kudorora utalii baada ya kujenga barabara?
 
Back
Top Bottom