Ni kwanini maji hayajai mtera ?

Avocado

Member
Aug 23, 2010
97
4
Ni jambo la kushangaza sana kusikia kuwa maji hayaongezi kwenye bwawa la umeme la mtera wakati huku ambako ndio chazo cha maji hayo mvua ipo ya kutosha,tena inanyesha sana,hebu tujiulize hayo maji yanapotelea wapi ? na ni jambo ambalo si kawaida kina cha maji kushuka kwa kiasi hicho wakati huu wa masika,je ifikapo juni au julai hali itakuwaje ? Mimi kinachonishangaza ni kwanini issue ya umeme imevamiwa sana na wanasiasa na kila mmoja ni msemaji,hivi kwanini tunashindwa kupata suluhisho la kudumu la tatizo hili tena katika nchi ambayo Mungu ameibariki kwa kuwa na vyanzo vyote vya nishati vijulikanavyo duniani,tuan maji.upepo,makaa ya mawe,jua la kufa mtu,Uranium n.k hivi ni nani aliyeturoga nchi hii ?
 
Unachosema ni kweli; siasa za ubabaishaji ndizo zinazo itafuna nchi yetu. Utaona wanasiasa wanajitia kimbelembele katika mambo yanayohitaji utaalamu wa kitaaluma, matokeo yake tatizo linaendelea kukua huku wamejizolea mamilioni ya fedha bila kulipatia ufumbuzi tatizo husika.
 
Kwani Life span ya mtera wakati inajengwa ilikuwaje, Ukarabati wake. Je maagizo ya wataalmau yalifuatwa.

Kinachovuruga Tanzania ni wanasiaa kuwa juu ya kila kitu.

Mhandisi mkuu wa nchi pale ujenzi anajiona sisimizi mbele ya waziri mbaye ni kama Tembo. badala ya Mhandisi yeye kumshauri wazirri yeye ndo anashauriwa nini kifanyike. Ukiona mChezo wa Dowans ni yale yale

Channel of communication ni Top down hakuna majadiliano. Rais ,Waziri mkuu , RC etc anaaagiza watendaji wanatekekeleza.


Sijui kama hata hayo mabwa maitanance yake inafanyika . Hata ukiwa na Marcedez benz ambalo ni imara kuliko MarkII bila kufuata usahuri wa kitaalama na Utunzaji litakaa juu ya mawe tu.

So sabbau ya msingi ni kwamaba watanzania tumewekeza na akili zetu ziko kisiasa zaidi
 
maji yatajaa vipi wakati bwawa limejaa matopee??????????
 
Maji hayajai Mtera kwa sababu serikali inataka kushinikiza kuwashwa kwa mitambo ya Dowans. Siku ukisikia tu serikali imeweka mkataba mwingine na Dowans basi siku hiyo hiyo maji yatajaa Mtera.
Hatuna watu bali manyang'au tu.
 
Back
Top Bottom