Blood of Jesus
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,199
- 10,832
Rejea swali hilo hapo juu. Ninaongea haya nikitokea katika utumishi wa Mungu. Tunzeni hili mtakuja kulithibitisha soon. Ni kwanini hata angetumia mbinu na njia gani kamwe hatofanikiwa?
1. Kukosa kibali(kwa Mungu na kwa wanadamu) Hana kibali ndio maana ametumia na anatumia nguvu nyingi sana. Mfano mdogo ni kuanza kampeni hata kabla ya muda. Mioyo ya waTanzania haiko pamoja naye kiukweli. wale wanaoonekana kuwa pamoja naye ni wale wenye unafiki na wenye kukumbatia masilahi binafsi.
2. Kutokusikia/kuzidharau sauti za watumishi wa Mungu. Mungu hutumoa watu kuleta ujumbe kwa wanadamu. Ujumbe wa Mungu ni kuonya, kukaripia, kuelekeza, kufundishia, ... Mtu awaye yote anapowapuuza watumishi wa Mungu huwa amempuuza Mungu mwenyewe.
3. Kuuza/kugawa rasilimali za Taifa (hasa Taifa la Tanganyika) kinyume na matakwa ya waTanganyika wenyewe. Kuupuuza chombo muhimu katika Taifa kama TISS.
4. Kutumia mbinu kandamizi kulazimisha kukubalika. Mambo kama utekaji, uteswaji, uuaji kwa wale wote wanajaribu kumkosoa. Mioyo ya wananchi inaumia na kulia kwenye haya madhila wanayopitia. Kuwafunga wapinzani wake kisiasa kwa kuwabambikia kesi kubwa kubwa na za kutisha.
5. Kuupuuza mchakato halali wa kikatiba wa kichama kupata nafasi ya kugombea nafasi hiyo ya uRais kama ilivyo desturi ya vipindi vyote.
6. Kushindwa kutafuta na kuanzisha njia sahihi za kupata mapato ya nchi katika kujiendesha na kubobea katika kukopa madeni ambayo muda sio mrefu yataigharimu nchi kwa namna isiyoelezeka. (rejea kauli ya Ndugai)
7. Kugombana na mtu aitwaye Josephat Gwajima. Jambo hili limebeba hatari kubwa rohoni (yeye inawezekana hajui). Kuifungia huduma za kiroho katika makanisa ya ufufuo na uzima ni hatari zaidi ya anavyoweza kuwaza. Katika kanisa huduma mbalimbali hufanyika, - kufunga ndoa, usuluhishi wa ndoa, maombi na maombezi, ubatizo, watu kuokoka, nk Kuzuia kazi hizi kwa sababu yeyote Ile ni kushindana na kazi za Mungu Muumba mbingu na nchi.
NDIO MAANA NINARUDIA KUSEMA: HATOFANIKIWA KATIKA YALE ANAYOYAWAZA YEYE, na anajitia katika hatari kubwa. Bado ana nafasi ya kujirudi. Mungu ni wa rehema. Naomba Mungu amsaidie ATUBU atengeneze na waTanzania , la sivyo mtajionea.