Ni kwanini DC wa Hai Lengai Ole Sabaya hasimamishwi kazi kupisha uchunguzi?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,484
30,162
Kuna tuhuma nzito sana alizotoa mfanyibiashara maarufu wa Hai, Cuthbert Swai, anayemiliki hoteli ya kitalii ya Wetu Weru River Lodge, kuwa DC huyo wa Hai, Lengeli Ole Sabaya, alimwomba rushwa ya shilingi milioni 8

Mfanyibiashara huyo amedai kuwa ana ushahidi wa kutosga kuthibitisha tuhuma hizo

Ninafahamu vilevile kuwa serikali ya utawala wa awamu ya tano imejipambanua kuwa yenyewe inapambana na ufisadi, ikwemo hiyo ya upokeaji wa rushwa kubwa kubwa

Tunafahamu pia sheria za kazi za nchi, zinavyoelekeza, mtumishi yeyote wa Umma, anayetuhumiwa kwa kosa kama hilo la DC wa Hai, hatua za kuchukua, ambazo ni pamoja na kumsimamisha kazi na kuunda Tume maalum iliyo huru kuchunguza tuhuma hizo

Baada ya kukamilisha uchunguzi wake Tume hiyo itatoa ripoti yake, ambapo kama ataonekana hana hatia, ararudishwa kazini na endapo atathibitika kwa tuhuma zinazomkabili, basi atafikishwa mahakamani mujibu mashitaka yake

Ni jambo la ajabu kwa tuhuma nzito ya aina hii, kuona mtuhumiwa bado anaendelea na kazi, kitendo ambacho kitaendelea kumpa kiburi na kuendelea na manyanyaso yake anayowafanyia wafanyibiashara wa wilaya hiyo, kama alivyodai mfanyibiashara huyo, Cuthbert Swai

Kama hatasimamishwa kazi, tutachukulia kuwa utawala huu wa awamu ya tano umeamua kwa makusudi kabisa, kizovunja sheria, na kuzifanya kuwa na "double standard" kuangalia ni nani anayetuhumiwa nazo

Pia itachukuliwa kuwa kuna baadhi ya wayeule wa Rais, ambao wamekuwa "untouchables" hususani wateule wa Rais, wanaodaiwa kuwa wanawafanyia manyanyaso makubwa sana wapinzani

Tunakuomba Mheshimiwa Magufuli, ili serikali ysko isiendelee kuchafiliwa, msimamishe kazi huyo DC wa Hai, na tume hiru ya uchungizi iundwe, kuchunguza tuhuma hizo nzito

Kama ambavyo mheshimiwa Rais umekuwa ukitamka kuwa MAENDELEO HAYANA CHAMA
 
Umesikia wanasema kuwa Olesaya husema"ametumwa Hai kwa special mission" na anaripoti kwa mkubwa...hatuwezi jua huenda alilofanya ni moja ya mission aliyotumwa. Mkuu mwenyewe aliwahi kutamka KASKAZINI MSUBIRI KWANZA, huenda ameamua hata kudhoofisha sekta binafsi ili wengine wapite mbele.
Aisee........

Hiyo inasikitisha sana, kwa Jiwe kuwaelekeza wateule wake wawanyanyase wafanyibiashara ili wafilisike kwa lengo la kuifanya kanda ya kaskazini izorote kiuchumi!
 
Anaripoti juu na wa juu hapangiwi kazi (ila tumempa kura ,leo anaturuka hatuwezi kumpangia ) haaa nchi yatu hii
Hayo madai yake ya kiburi Jiwe kuwa sisi wananchi hatupaswi kumpangia kazi, ndiyo kauli "itakayomtekeza" kwenye uchaguzi mkuu 2020!

Sisi tumempa dhamana ya kutuongoza, kwa hiyo ANALAZIMIKA kutusikiliza sisi wananchi wake tunachoshauri
 
kuwa DC huyo wa Hai, Lengeli Ole Sabaya, alimwomba rushwa ya shilingi milioni 8
DC "kajibu mapigo" kwa kwenda kijijini na kustage watu anaodai wamedhulumiwa haki zao na Swai, kwamba hicho ndio chanzo cha ugomvi wao. I hope huyo mfanyabiashara anao huo ushahidi wa messages na CCTV clips. Otherwise Ole Sabaya amekusudia kudeal nae perpendicularly
 
Kwa nini am-plant huyo bibi kizee kuwa ndiyo chanzo cha mgogoro huo??

Mbona hakujibu tuhuma alizorushiwa yeye kuwa ameomba rushwa ya mamilioni ya shilingi??

Ni dhahiri basi katika kile kinachoitwa kwenye sheria ya ushahidi kuwa hapo amejitumbukiza kwenye 18 ya mfanyibiashara, Cuthbert Swai, katika kile kinachoitwa " circumstantial evidence "
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom