John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 110
- 210
Ni kwa vipi Daudi alivyoupendeza moyo wa Mungu
Daudi ni nani
Hebu tusome katika Matendo 13:21 “Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini.
22 Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, MTU ANAYEUPENDEZA MOYO WANGU, ATAKAYEFANYA MAPENZI YANGU YOTE”.
Daudi aliteuliwa kuwa Mfalme wa Israeli
Kijana Daudi, alikuwa nyikani akichunga kondoo. Basi wakamwita huyo mvulana ndani ya jumba naye Samweli akamtia Daudi mafuta "na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile" (1Samweli 16:13).
Wakati alitiwa wakufu kama mfalme wa Israeli, Daudi anakisiwa kuwa na umri wa kati ya miaka kumi na miwili hadi kumi na sita.
Daudi ndiye mtunzi wa kitabu cha Zaburi nyingi. Kati ya zaburi 150, Daudi peke yake aliandika zaburi 75 (50%). Katika zaburi hizo tunaona jinsi alivyotamani kumtukuza Mungu.
Mara nyingi alichukuliwa kuwa mfalme mchungaji na mtunga mashairi. Maandiko humwita "mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza" (2Samweli 23: 1).
Maisha ya Daudi yalionekana kuwa na hisia nyingi za kibinadamu, kijana mchungaji wa kawaida aliye na ujasiri mkubwa katika uaminifu wa Mungu ambaye aliheshimu mamlaka, alikimbilia usalama wake, na akawa mfalme dhidi ya wafalme wote wa Israeli wa baadaye. Alipigana vita 66 vya kijeshi na kupata ushindi katika vita vyote hivyo.
Aidha, alianguka katika dhambi kubwa, na familia yake ikateseka kwa sababu hiyo.
Lakini katika njia yote, Daudi aligeuka kwa Mungu na kumtumaini. Hata katika zaburi, wakati Daudi alipokufa moyo au kukata tamaa, tunamuona anainua macho yake kwa Muumba wake na kumpa sifa. Kumtegemea Mungu huku na kuendelea kutafuta uhusiano na Mungu ni baadhi ya mambo ambayo humfanya Daudi awe mtu ambaye alipendwa na Mungu.
Japo Daudi hakuwa mkamilifu kwa viwango kama vya watumishi wengine wa Mungu waliomtangulia au waliomfuata, mfano wa Musa, Samweli, Eliya au Danieli, lakini biblia inamshuhudia kuwa ni mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu sana (1Samweli 13:13-14; Matendo 13:22).
Mungu alimuahidi Daudi kuwa mzao wake utatawala katika kiti cha enzi milele.
Kabla ya kifo chake, Daudi alifanya maandalizi ya kujengwa kwa hekalu. Sababu ya Mungu ya kutomruhusu Daudi kujenga hekalu ni kwamba alikuwa amemwaga damu nyingi, lakini mwanawe Daudi angekuwa mtu wa amani na siyo mtu wa vita. Sulemani angejenga hekalu (1Mambo ya Nyakati 22:7-8).
JE, DAUDI ALIMPENDEZAJE MUNGU?
Hebu tuangalie baadhi ya mambo yaliyomfanya Daudi awe vile. Yanaweza kutusaidia na sisi katika safari yetu ya kutafuta kumpendeza Mungu.
Jambo la kwanza: Daudi alimwamini Mungu kwa moyo wake wote.
Hakujali ukubwa wa tatizo lilolokuwa mbele yake. Kadri tatizo lilivyoonekana kuwa kubwa, ndivyo alivyomfanya Mungu wake kuwa mkubwa zaidi ya hilo tatizo, na hiyo ilimfanya asiogope chochote.
Anasema katika Zaburi 27:1: "Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani"?
Wakati alipokuwa anapambana na Goliathi, hakuogopa ukubwa wake na vitisho vyake. Japokuwa alikuwa hana silaha yoyote mkononi mwake, Daudi hakuogopa, badala yake alimwambia maneno haya, 1Samweli 17:
45 “Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. 47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.
Nasi tujiulize, majaribu makubwa yanaposimama mbele yetu, je ndiyo tunamkimbia Mungu au ndiyo tunamuamini Mungu, na kumuacha ili aonyeshe yeye uweza wake?
Kumbuka Daudi hakufanya hivyo kwa Goliathi tu, bali katika matatizo mengi yote aliyowahi kukumbana nayo. Alisema pia, nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti sitaogopa mabaya, kwa maana Bwana yupo pamoja nami, Gongo lake na limbo yake vyanifariji (Zaburi 23:4).
Jambo la pili: Daudi aliipenda sheria ya Mungu kuliko kitu kingine chochote.
Anasema, katika Zaburi 119:
47 "Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda.
48 Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako".
Zaburi 119:140 "Neno lako limesafika sana, Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda”.
Katika sehemu nyingi kwenye Zaburi, utaona Daudi akionyesha upendo wake katika Neno la Mungu. Hiyo ilimfanya awe analitafakari sana, siyo kulisoma tu kama gazeti, bali alikuwa analitafakari sana mchana na usiku.
Je, nasi tunao moyo kama huo wa kulipenda Neno la Mungu?
Tunapoambiwa uzinzi ni dhambi, tunafurahia kusikia hivyo? Tunapoambiwa vimini ni dhambi tunafurahia kusikia hivyo? Tunapoambiwa usengenyaji ni dhambi, je tunazingatia kujirekebisha? Je, tunapoambiwa ulevi na uvutaji wa sigara ni dhambi, tunasikiliza? Tunalitafakari hilo usiku na mchana.
Kama ndiyo hivyo, basi tujue kuwa tupo katika njia ya kuelekea kumpendeza Mungu.
Daudi anasema hivi, katika Zaburi 1:
1 “Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. 2 Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, NA SHERIA YAKE HUITAFAKARI MCHANA NA USIKU. 3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa”.
Jambo la tatu Tatu: Daudi alikuwa ni mtu aliyekubali na kuyakiri makosa yake haraka sana, na kutubu.
Alipozini na mke wa Uria (mwanajeshi), na pia kumuua Uria, baada ya kuletewa habari hizo na nabii Nathani (2Samweli 12: 13), utaona kuwa, saa ile ile, Daudi alikiri kuwa kweli ametenda dhambi.
Japo Mungu alimsamehe kwenye kosa la kuzini na Bathsheba, mke wa Uria, lakini alimuadhibu kwa kosa la kuua, na kumwambia "upanga hautaondoka nyumbani kwake" (Zaburi 51:4).
Lakini sisi, ni mara ngapi tunamficha Mungu dhambi zetu, hata kama uthibitisho wote unaonekana. Tutajaribu kutengeneza mazingira, na kusema ni kwa sababu ya hiki au kile, ndiyo maana nimetenda hivi au vile. Ni kama tu vile walivyofanya Adam na Hawa pale bustanini.
Katika Zaburi 51, tunaona jinsi Daudi alivyoungama dhambi zake zote.
Vivyo hivyo na sisi, Mungu atusaidie tuwe na moyo huo huo, wa kukiri makosa yetu na kutubu kwa kumaanisha kabisa kuacha.
Jambo la Nne: Daudi alikuwa ni mtu wa kuustaajabu uweza wa Mungu, na hivyo hakuona aibu kuutangaza uweza huo kwa kila mtu.
Zaburi 119:46, inasema "Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu".
Daudi alikuwa yupo radhi kumtukuza Mungu hadi nguo zinamtoka, bila kujali yeye ni mfalme, (Daudi alicheza mpaka nguo zikaanguka). Alimtukuza Mungu, hadi dunia nzima ilijua kuwa yeye kweli ni mtumishi wa Yehova. Katika Zaburi, sehemu kubwa utaona Daudi anavyoihubiri kazi ya Mungu na uweza wake na utukufu wake duniani kote.
Je, sisi tunaounea aibu ushuhuda wa Yesu Kristo?
Mtume Paulo aliandika katika Warumi 1:16, "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia".
Hivyo, na sisi tunapaswa kuitangaza injili kwa nguvu zetu zote Mungu alizotupatia, ili na sisi tumpendeze Mungu. Bwana atusaidie wote katika hayo.
Naamini tutachukua hatua nyingine katika kujirekebisha katika mambo hayo manne, na mengine.
Tunachojifunza kutoka kwa Daudi
1. Bila sisi kujua, Mungu anaona mioyo yetu na kuitathmini kwa ajili ya mapenzi yake.
2. Kumuamini Mungu kwa moyo wote.
3. Kuzipenda sheria za Mungu na kuzitekeleza.
4. Kukubali na kukiri makosa haraka na kutubu. Kutubu ni kujitakasa.
Aidha, kutubu ni sawa na kusema “kubali yaishe”, na kuanza upya.
5. Kuustaajabu uweza wa Mungu na kutokuona aibu kuutangaza uweza huo kwa watu wengine.