Ni kwa nini mawifi hawapatani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kwa nini mawifi hawapatani?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SMU, Feb 3, 2009.

 1. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi uhusiano kati ya mawifi (mke na dada wa mume) unakuwa na walakini (hawapatani, hawapendani). Inaweza kuwa mke hawapendi dada wa mumewe au dada hawampendi mke wa kaka yao.

  Athari za mahusiano haya kuwa mabaya mara nyingine huweza kuleta madhara makubwa kwenye ndoa. Kwa uzoefu wangu naweza kuthubutu kusema kati ya relationships kumi za mawifi basi zaidi ya tano mawifi 'hawaivi'.

  1.Je unadhani ni nini hasa chanzo cha mahusiano haya kuwa na mushkeli? Je ni mke au dada wa mume?

  2. Je mwanaume anachangia kwa kiasi gani kufanya uhusiano huo kuwa m'baya?

  3. Je hili ni tatizo la sisi waafrika tu au hata wengine wanalo? Kama na wengine wanalo, je inawezekana kwamba ni kwa asili tu mawifi hawapatani?
   
  Last edited: Feb 3, 2009
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  vyanzo:-

  - umasikini (wa mali na akili):
  kama wewe ni kijana wa kiume uliyebahatika kuwa na maisha ya wastani (umesoma kiwango cha chuo kikuu, unapata mahitaji yako muhimu ya kijamii, unakipato cha kukuwezesha, e.t.c) mara nyingi unakuwa unategemewa na ndugu zako (wa-kiume/kike), na utegemezi ni wa mahitaji muhimu ya kijamii! Kwa mantiki hiyo basi unapopata mwenza (mchumba - mke) msaada wako kwa ndugu hupungua kwa ghafla na kwa kiwango kikubwa (sawa?) na mapokeo ni kwamba huyo mwenza ndiyo chanzo cha upungufu huo (sawa?), kwa hiyo dada zako wataanza kuonyesha vituko (wivu) kwa mwenza wako

  - udhaifu wa kiasilia:
  kila binadamu umwoneo binadamu mwenzake wa jinsia tofauti WIVU! Maana yake ni kwamba, Dada yako anakuonea WIVU (sio wa kushirikiana kimwili)unapoanza mahusiano na binadamu mwenye jinsia kama yake!

  - u-afrika:
  kama unaishi bila ndugu zako (without extended family) hakuna atakayeonea wivu mwenza wako!

  KWA HIYO
  - hakuna mwenye TATIZO!
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ni sahihi kusema ni tatizo lisiloepukika?
  Umasikini wa ndugu, wivu asilia na extended family ni vitu ambavyo ni vigumu kuviepuka!
   
 4. Mhache

  Mhache JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2009
  Joined: Jun 20, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tatizo nafikiri ni asili tu na kukosa maarifa. Pia unapooa inakuwa unakata au unapunguza huduma ulizokuwa unatoa kwa dada zako au wifi za mke wako. Wifi wanajenga chuki ambayo haina maaana kwani wanafikiri mke wa kaka amekuja kuziba ile mirija ya wao mawifi kumfaidi kaka yao.
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  wakati naolewa nilikuwa napatana sana na mawifi zangu kuliko maelezo,kukaa kidogo tulianza kutokuelewana/chuki zsizo na sababu..... walidhani mimi ndio chanzo cha wao kukosa matumizi yale waliokuwa wakiyapata kabla, kumbe ni majukumu yamekuwa mengi kwa kaka yao tofauti na kipindi alichokuwa single, lawama zote ni kwangu, tena zile za kiswahili"nimemteka kaka yao".....mama mkwe ndio kabisaaaaa...haaa ndoa hizi jamani.
   
 6. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nyamayao,
  Vipi shemeji zako (kaka wa mumeo) nao pia hampatani? Kuna mchangiaji amehusisha tatizo hili na umasikini. Lakini hata hivyo napata hisia kwamba tatizo hili lipo kwa wanawake zaidi kuliko wanaume (i.e. mashemeji). Hili linanipa shaka hasa kama umasikini inaweza kuwa chanzo cha tatizo hili. Tena tatizo hili lipo hata kwa mawifi ambao wana uwezo na hawamtegemei kaka yao kiuchumi.
   
  Last edited: Feb 3, 2009
 7. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,437
  Likes Received: 1,019
  Trophy Points: 280
  Nukuu "Adui mkubwa wa mwanamke ni mwanamke mwenzie", sasa haijalishi kama ni wifi au mama mkwe. Wanawake wao kwa wao hawapendani, hata akiwa house girl jua bifu litakuwepo, mawifi kutokupendana inakuwa katika narrow percipective ukitazama kwa upeo upana utaona ni zaidi ya mawifi.

  Kama kungekuwa na kipimo kwa ajili ya kiwango cha uchoyo na wivu kwa binadamu basi wanawake wengi wangekutwa na kiwango kikubwa ukilinganisha na wanaume. Hapa ndipo balaa linaanzia kama walivyoainisha wachangiaji wengine.
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  SMU mie na mashemeji 2po poa sana, wao ndio wakunifariji, tunasaidiana kwa namna 1 au nyingine,kwangu mie nitasema kwa wifi zangu sio umaskini coz ni 1 ndio anamtegemea yupo chuo, mwingine kaolewa na maisha yake ya kawaida, anafanya biznes na akikwama akija kwa kakake akijibiwa visivyo ndio hapo inakula kwangu, wa 3 ni mama mwenye uwezo wake sana tu but ndio huyo ambaye hatuelewani kupitiliza, kaka yao akiwaambia sasa hivi nimekwama nenda kwa dada nae anisaidie inakuwa ishu, dada akiambiwa tayari nyamayao ndio anamzuia kaka yao kuwasaidia...haaa nahamakigi sema ndio hivyo tena.
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Feb 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,770
  Trophy Points: 280
  waaambie kwenye biblia mume atamwaacha baba na mamake na kuambatana na mkewe hakuna sehemu walioonyesha atambatana na wifie!!!lingine ambalo tunakuwa nalo ni kwamba wanaumewengi awatambui umuhimu wa wake,,wewe umeoa anakuja dadko mara kwa mara naomba chumvi,naomba sukari,,kuona aitoshi ukigongana nae ati anakupiga busu ,saa mke akiangalia busu nalopigwa mumewe alitofautiani kabisa na lake pale kanisani au msikitini unafikiri kitaeleweka,,hivyo na sie wanaume tujue gap iliop[o kati mke ,dada,wazazi,,mfano mmoja mi baada ya kuoa dadazangu wengine awakumpenda mwenziwangu wakachukua jukumu la kupiga usiku wa manane ati anakuuliza uko juu ya kiuno then usiku mwema!!mmh mkewangu akasema awana muda mwingine ukiona logic,nikaamua kumwaga live beef-chicken mpaka leo ....n i dont mind
   
 10. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #10
  Feb 4, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0


  haaaa dada zako hao wanakuuliza hayo maswali? duuu! kazi kweli kweli.
   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Feb 4, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa wakristu kama utasoma biblia yako kuhusu ndoa kuwa ni kati yako na mume/mke. Heshima ibaki kwa ndugu. Kwa kifupi mawifi wengi wana wivu sana!!! Mama mkwe huwa kama ilivyo kwa kawaida ya binadamu, wanawe ni bora kuliko wewe mke wa mtoto wake (mkwewe). Ni bora ukiolewa uwe moderate tu, usijipeleke sana kwa mawifi i.e. kujipendekeza kwani kwa uzoefu hata kama mtashibana kiasi gani but maneno ya karaha yahakosekani. Cha msingi mke na mume wa set mipaka ya familia yao (mke/mume/watoto i.e. nuclear family) wengine ni second interest. Na hii ni lazima muiwekee msingi na mhimili from the begining ya maisha yenu ya ndoa. Vinginevyo, mtakuwa watu wa kutoelewana na mwishowe siyo mzuri kwa ndoa nyingi. Try to make your family or marriage a peaceful destination. Penye amani, upendo na furaha pana mafanikio.
   
 12. Mtumzima

  Mtumzima Senior Member

  #12
  Feb 9, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 140
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nawaunga mkono watoaji mada hasa wa kwanza.Ndoa nyingi zinavurugwa na Mama wa mwanaume na watoto wao wa kike.Tatizo hasa linaanza kwa hawa vizabinazabina (dada wa mwanaume) kuanza pekeche,umbeya, unafiki na majungu dhidi ya wifi yao!! Taabu na bahati mbaya kwa baadhi ya akina mama wakwe inakuja pale anapoungana na hawa wapuuzi ktk fitina hizo.Hapo wamesahau kwamba hata wao (mama wakwe) wangeweza kukutwa na matatizo hayo ktk ndoa zao vipi wangeweza kuwatunza hao wafitini(binti zao) na hata huyo wa kiume mwenye mke wanayempiga vita? Dawa ni kuwapiga marufuku kuja unapoishi na kila mtu akae kwake,mpaka akili ziwakae sawa!![/B]
   
 13. J

  John W. Mlacha Verified User

  #13
  Apr 20, 2013
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni njaa
   
 14. N

  NatJ JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2013
  Joined: Mar 6, 2013
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wengine sio njaa mkuu bali ni wivu wa kijinga, utawakuta wanauwezo mzuri lakini bado wanapeleka chokochoko za hapa na pale ilimradi wifi mtu asiwe na raha na kaka yao utafikiri wanataka waolewe wao.
   
 15. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2013
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  I concur with u 100%, mimi ni shuhuda/muhanga/muathirika wa yote uliyonena.
   
 16. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2013
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  niliwahi kuulizwa swali na dada zangu that kati ya mke wangu na wao nina mpenda nani na mm nikawajibu kama je wao wana ni penda mimi kuliko wanavyo wapenda waume wao, waka tazamana then waka baki kimya
   
 17. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2013
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,102
  Likes Received: 11,254
  Trophy Points: 280
  mawifi wamezoea kuwapiga mizinga kaka zao, kwahiyo akioa lazima huyo mwanamke apate cha moto kwasababu mianya yote ya pesa inakatika
   
Loading...