Ni kupenda au kukomoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kupenda au kukomoa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by cheusimangala, Mar 1, 2010.

 1. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kuna mkaka mmoja alimtogoza dada mmoja mwaka mmoja na nusu uliopita lkn huyo dada akamkatalia kistaarabu tu,sasa pamoja na muda mrefu kuwa umepita lkn huyo kaka kila siku anampigia huyu dada simu wkt wowote anapojisikia hata usiku wa maneno akimbembeleza na wkt mwingine kumuandikia dada sms za mapenzi as if ni wapenzi na dada hawezi kubadili namba yake na pamoja na kaka kuonywa mara kibao lakini hakomi,mbaya zaidi huyo kaka akijua kuna kijana anayemfuatilia huyo dada au ana uhusiano wowote wa karibu basi anamfuata huyo kijana na kumtishia kua akae mbali na huyo dada akidai kuwa huyo dada ni mchumba wake, na ameshamtishia kaka mmoja aliyekua akimfuatilia huyo dada kwa kutaka kumgonga kwa gari yake,pia amekwenda hadi nyumbani kwa mama wa huyo dada na kulia machozi kama mtoto mdogo na kumtishia huyo mama wa huyo dada kuwa akisikia amejinyonga basi ajue ni kwa sbb binti yake kamkataa.pia anapita kila mahali akitangaza kuwa huyo dada ni mchumba wake,na vitu vingi kama hivyo,SASA WADAU HIVI HUYU KAKA NI AMEKUA CRAZY IN LOVE AU ANAMKOMOA HUYU DADA!!
   
 2. handsomeboy

  handsomeboy Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hiyo tena kero sasa kwanini huyo dada asiende kumlipoti polisi. Huyo jamaa anaonekana ana matatizo kidogo 'hau camu' amnyime mwenzie maisha kwa mawazo yake. Nendeni kunakohusika kwa rafiki zake waongee nae au ikibidi kwenye mkono washeria.

  Sito staajabu nikisikia jamaa kamtandika dada kisu kisa kamuona na kaka mwingine au yeye kajinyoga, tuombe in the worst case scenario the latter happens. Dada anahitaji kuhakikisha analimaliza hili kwa namna yeyote kwa usalama wake na kaka anahitaji kumuona a mental health proffesion yuko mmoja kule mwananyamala B, DR. Mamuya.
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Shabashi jamni midume mingine haisikii kha!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  how old are they??????
   
 5. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mapenzi kizunguzungu jamani...lkn huyo sasa itakuwa kiarabuarabu maana mwendo wa matishio tuuu mpaka kieleweke lkn anaweza toa mtu roho jamani..wakae mbali wanaomfuatilia huyo dada...unaweza nitajia jina lake na anapokaa ili nimlinde huyo dada maana anahitaji mijitu kama sie ili huyo jamaa tumtoe roho yeye kabla hajaathiri wengine..
   
 6. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ujue kila anayesikia kuhusu hii issue anasema hivyo hvyo kuwa jamaa lada chizi lkn cha kushangaza uchizi wake anamfanyia huyu dada tu maana kwingine koote sio chizi tena ana cheo mahala na anafanya kazi vizuri tu.asante kwa ushauri lkn dada anashindwa kumripoti polisi sbb marafiki wa huyo kaka pia ni marafiki zake huyu dada kwa hiyo anafeel guilt.
   
 7. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  huyu dada ni 27 na jamaa 32!
   
 8. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  yaani huyo ni kinganganizi imagine kila siku asubuhi mchana na jioni amejiwekea ratiba anatuma sms za mapenzi bila kujali anachosema huyu dada.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  cheusi mangala,
  hivi hiyo shepu yako
  ndo zile dawa za wachina sio????????
   
 10. handsomeboy

  handsomeboy Member

  #10
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  haya choice ni yake guilty conscious against usalama, wake, maisha yake na vyote dada wa miaka 27 anatakiwa kufanya kwa muda huu. Au aendelee kum-entertain a psychopath chizi si lazima aokote makopo Mrembo.
   
 11. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  magu thanx kwa offer ya kumlinda lakini sorry siwezi kutaja jina wala adress ya anapokaa!wee huogopi kugongwa na gari?
   
 12. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mshauri huyo dada abadili namba ya simu au amblock hiyo inaweza saidia hiih ihihi ila ningekuwa mie namfata kwao nampa live maana hakomi aagrrr
   
 13. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  the boss toa maushauri acha kutoka nje ya mstari!umeuliza umri nimekupa nangojea hekima zako boss!
   
 14. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  dada hawezi kubadili namba yake labda kumbloc nitamshauri,lkn maria roza huyo dada keshampaka hadi kwa matusi oficini kwake lkn kaka huyo is of his own kind my dear,ni kero,kero hakomi nadhani anakomoa.
   
 15. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  A psycho stalker ... huyu crazy dude inabidi achukuliwe a restraining order haraka, maana akiachiwa ndio wale ma psychotic killers wana weza ingiza semu kuua fammilia nzima , dah kaa nae mbali kabis ahuyo jamaa hafai.
   
 16. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Dah hapo sasa hakuna jinsi mshauri huyo dada akae chini na huyo kaka amueleze tu vizuri inaweza saidia kidogo mhh kaka kweli kapenda :cool:
   
 17. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  he he heee,nilijua whats next,huyo ndio the big boss bwana.
   
 18. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  labda ya polisi ndio itasaidia na sidhani kama naweza kufungwa na akiwa huru najua ataendeleza tu maana hamna maneno anayoambiwa akaelewa,anakero kishenzi!
   
 19. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  hivi maria roza ingekua ni wewe unafanyiwa hivyo ungedhani ni kupendwa au kukomolewa sbb ulimkataa?
   
 20. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Ningeanza kuogopa maana nimemfahamisha mara zote bado anakuwa haelewi na nitaanza kuhisi labda anaweza kutumia njia nyingine za ajabu ili anipate, nitaanza kuwa mbali nae hata kuhama eneo ninalo ishi na kama anajua kazini kwangu bas nitawataarifu japo walinzi wa geti siku akija aambiwe nimehama ofisi na sitasahau kuchukua RB maana sijui alilonipangia anaweza hata mtuma mtu aje aniwekee kitu kwenye kinywaji.
  Kama haitoshi bas nitatumia wazee wenye hekima waende kwa wazazi wa huyo kijana na kuwaambia kinacho endelea!
   
Loading...