Ni kosa gani ulilifanya kwenye ujenzi wa nyumba yako na usingependa wengine walirudie?

Usiwaamini sana mafundi wa kitaa. Kama una hela tumia professional fundi au engineer. Napambana na sisimizi haijawahi tokea. Marumaru hadi natamani nibomoe nianze upya space kati ya tile na tile walibana sana kiasi kwamba grout haikai matokeo yake space ni nyingi na sisimizi wanatokea humu. Fundi rangi pia naye ni shida pia nilimwamini sana fundi wangu lakini nimekuta baadhi ya vitu hajui. Kama issue za Marumaru, rangi, furniture nk.

Sent from my Infinix X672 using JamiiForums mobile app
Kwenye sisimizi ina maana kuna kosa lilifanyika hapo ninavyoelewa kuna dawa ilitakiwa kuwekwa wakati wa kupiga jamvi au sakafu sasa hili kwako halikufanyika....
 
Wiring inabidi uifikirie vizuri sana.

Nilisema kwamba sebule ya pili (morning room) itakuwa ya ukimya, haitakuwa na TV wala computer. Itakuwa ya vitabu, makochi, meza na kusoma.

Kwa hivyo sikufanya wiring yoyote ya LAN (RJ 45).

Fast forward nimemaliza kujenga, uhalisia wa kuishi, sebule hiyo imewekwa TV, All in One computer, several laptops, natamani ningekuwa nimeweka RJ45 ports.

Luckily the wireless router is pretty good.

Somo hapa, ni bora ukafanya wiring kama ya RJ 45, halafu usiihitaji, kuliko kutofanya halafu ukaihitaji.
 
Habari wana JF

Ni kosa gani ulilifanya kipindi unajenga na ungependa wengine wajifunze ili lisitokee kwao?
Nilitoka Ulaya nakiwa nime-save bilioni moja nikitaka nijengewe nyumba yenye ubora sawa na Ulaya. Mafundi wa Dar es Salaam ambar walikuwa wanafisiwa na watu wengi walinifanyia kazi ya hovyo kiasi kwamba maji ya moto yalikuwa hayatoki, nyumba inavuja, rangi haijapakwa vizuri. Tulikaa mwaka mmoja, tukaamua kuhama. Kwa kuwa kiwanja kilikuwa ni prime plot na ilinichukua miaka mingi kukusanya pesa za kukinunua. Sikutaka kuishi kwenye nyumba ambayo sikuwa na furaha. Nikaamua kuibomoa nyumba yote, nikakopa benki halafu nimkatafuta architect kutoka Afrika ya Kusini, nikachora ramani mpya. Nikatafuta kampuni ya ujenzi kutoka Cape Town (Wana uzoefu wa kujenga nyumba za kwenye fukwe au mija yenye joto). Nyumba mpya imenipa furaha kubwa. Somo: Mafundi na wachoraji wa ramani wetu (with all due respect) wanakosa exposure lakini wanaamini wanajua kila kitu. Tanzania tumejifungia Saną; tunahitaji kujifunza kutoka nchi nyingine. Tunahitaji kuwatia moyo watt wasafiri kwenda Afrika ya Kusini, Kenya na kwingine kote tukiwa tumefungua moyo na akili wa kutaka kujifunza. Kama unataka prime property/high end house, nakushauri uangalie njee ya mipaka ya Tanzania.
 
Tunaomba picha ya hio nyumba mpya tuwe inspired
 
20231003_173552.jpg
20231001_082216.jpg
20231001_082239.jpg
hii nyumba namjengea bibi ina vyumba viwili,jiko na sebule ..kupaua fundi ameniambia inakula bati 150,4×2 mbao 160..
Fundi yupo sahihi na hesabu zake?
 
Mbona bati nyingi sana mkuu kwa ukubwa wa hiyo nyumba yako! Nusu ya bati ningeweza kubali... yaani 80. Hata hizo mbao za 4x2 ni nyingi!
Fundi kazingua,au unaagiza atakua ajenge yake pia pitia ela Yako,Mimi Ina vyumba 4 sebule, Dining na store...lkn fundi amekadilia itakula 120 bati. Take care!
 
Nilitoka Ulaya nakiwa nime-save bilioni moja nikitaka nijengewe nyumba yenye ubora sawa na Ulaya. Mafundi wa Dar es Salaam ambar walikuwa wanafisiwa na watu wengi walinifanyia kazi ya hovyo kiasi kwamba maji ya moto yalikuwa hayatoki, nyumba inavuja, rangi haijapakwa vizuri. Tulikaa mwaka mmoja, tukaamua kuhama. Kwa kuwa kiwanja kilikuwa ni prime plot na ilinichukua miaka mingi kukusanya pesa za kukinunua. Sikutaka kuishi kwenye nyumba ambayo sikuwa na furaha. Nikaamua kuibomoa nyumba yote, nikakopa benki halafu nimkatafuta architect kutoka Afrika ya Kusini, nikachora ramani mpya. Nikatafuta kampuni ya ujenzi kutoka Cape Town (Wana uzoefu wa kujenga nyumba za kwenye fukwe au mija yenye joto). Nyumba mpya imenipa furaha kubwa. Somo: Mafundi na wachoraji wa ramani wetu (with all due respect) wanakosa exposure lakini wanaamini wanajua kila kitu. Tanzania tumejifungia Saną; tunahitaji kujifunza kutoka nchi nyingine. Tunahitaji kuwatia moyo watt wasafiri kwenda Afrika ya Kusini, Kenya na kwingine kote tukiwa tumefungua moyo na akili wa kutaka kujifunza. Kama unataka prime property/high end house, nakushauri uangalie njee ya mipaka ya Tanzania.
Chai na mandazi
 
Wasichokielewa wengi ni kwamba hao wataalamu mnaowasema hawana utaalamu wowote kuwazidi mafundi wapo mafundi wameenda shule wamepoteza miaka 5 au 3 utamuambia nini na yuko practical zaidi mainjinia wengi hawawezi na hawajui kazi ni makaratasi tu injinia mwenyewe anamtegemea fundi kufanya hesabu na ujenzi kiufupi ni amubane fundi yeye afanikiwe

Msiwadharau mafundi ila Mara nyng maboss ndio wanaosababisha nyumba kujengwa chini ya kiwango kumminya fundi unatoa hela ya material labda million 14 halafu hela ya ufundi laki 8 au million upaua nyumba kwa bati la kigae/versatile halafu hela kiduchu kwa ushauri wa paa nitafute inbox kukufanyia kazi ni ngumu kwani nabanwa Sana na muajiri Wang muda sipati na sipendi kuacha mafundi saiti wakaharibu kazi ya mteja
Mafundi wote duniani ni wapuuzi yaani wee kaa nao benet kabisaa ndio utatoa kitu cha maana.
Problem gao kubwa wao wanataka kumaliza kazi haraka iwezekanavyo na sio kizingatia kuwa kazi imefanywa kwa ufanisi
 
Back
Top Bottom