Ni kitu gani watu wengine huona kuwa cha kawaida ila wewe huwezi kufanya au kuwa nacho?

Kuna vitu ambavyo watu wengine wanaona kama trend au kawaida ila Mimi siwezi kufanya au kumiliki.Mfano kuweka na mito mingi kwenye kitanda,kuwa na Snapchat kwenye simu au account ya TikTok n.k! Wadau ni kitu au jambo gani hilo huwezi kufanya au kumiliki?
kula mahindi ya kuchoma ndani ya daladala🐒

lakin pia siwezi kabisa kama jamaa wengine kunyonya ice cream baridi ya ukwaju, kahawa, maziwa au strobell 🐒
 
Kupost vijembe whatsapp....mtu akipost vijembe aibu huwa naona mimi, kugombana kidogo wasapu mie siwezi!!!

Kujirekodi rekodi unaimba imba vinyimbo huku unafinya finya na kulamba midomo kisha kupost sijawahi na siwezi na huwa nashangaa wanaoweza wanawezaje
Nilipo highlight red hapo yaani hii ni tabia ya Mabinti wengine anaji snap au anatengeneza video TikTok huku anaimba nyimbo za Mbosso au za kuitamani ndoa huwa nawashangaaga sana. Alafu hiyo anayefanya hivyo ni graduate kabisa
 
Yani mtu analamba lamba mdomo anabinua binua macho anapost.....aseee hata na hela mie hicho kitu hapana, sijawahii siweziiii
 
Back
Top Bottom