Ni kitu gani kitakufanya useme namshukuru Ex-girlfriend/Ex-boyfriend?

Chakorii

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
18,586
50,683
Habari za mchana ndugu jamaa na marafiki,😊natumai mnaendelea vizuri.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Unajua si kila Ex anakuwa amekufanyia mabaya tu, si ndio e Ehee. Kama mlimaliza kwa ubaya basi kuna mazuri mengi yalishatangulia.

Hebu tuambizane mbali na zile moments za kupiga game, ni kitu /vitu gani ambavyo unakaa pekee yako na kusema yes tumeachana lakini ninakushukuru umenisaidia hiki kwenye maisha yangu.

Binafsi bhana 😊😊namshukuru Ex wangu amenifundisha maisha na amenibadilisha mno, namshukuru mno..na ni namshukuru Mungu kwa ajili yake.😊

Kuna wakati nakaa najiuliza hivi kama nisingekutana nae ningekuwa na maisha gani, nakosa jibu😔

😅😅kuna wale watu wakusema mtapasha kiporo😁😁najua hamkosekani..ila amini usiamini kuna watu wanakuja kwenye maisha yako kwa kufikisha ujumbe wa Mungu na kuondoka.


Karibuni🧚‍♀️🧚‍♀️🥂🥂🥂🥂
 
Alinifundisha hata hela ndogo inajenga na inatakiwa kuanza taratibu,(Kama ulianza kwa kupanga chumba kimoja,kwa nini usiinue chumba na sebule tu kwako sio uanze na ramani mpaka chumba cha wageni self)Naikumbuka sauti yake kwa mbali muda huo niko wimbi balaa.
 
Namshkuru kwenye mapenz alifanya nione kutambulishwa ni kitu cha kawaida maana hapo kabla nishawahi kua na pisi kali zaidi yake lkn mimi mwenyewe hata kuongozana nae nilikua naona ni ushamba,

zile movement akikutana na marafiki zake au wafanyakazi wenzie anasimama wakishasalimiana utaskia huyu ni fulani,ndie boyfriend wangu na mume wangu mtarajiwa Mungu akitufanyia wepesi ktk mipango yetu...daah aisee ilikuaga ni bonge la mtihani

zile za kushikana mikono wakati mnatembea nilikua naona ni ulimbukeni wa kutosha maana nilikua ni mgumu haswaa,ilikua hata tukitoka kupiga gem iwe home ama lodge hakuna nafasi ya kusindikizwa hata stendi nitakupa nauli nakwambia tutawasiliana hata wakati wa kuja napo staili ni hiyo hiyo na sio kwamba nilikua simpendi nilikua nampenda kweli kweli,lkn kupitia yeye vyote vilibadilika anafuatwa mpaka stendi na wakati wa kumsindikiza sasa muda mwingine nilikua nafika mpaka karibia na kwao kabisa

kiuchumi ndio kabisa siwezi kumsahau maana alikua na mradi wake na kufyatua matofali wakati nipo nae alinipa kazi ya usimamizi maana km mnavyojua vijana wa tz ni ngumu sana kumuheshimu boss hasa akiwa jinsia ya kike,alinipa hilo jukumu maana nilikua mission town tu kipindi hiko,alipoondoka kwenda mbele huko aliniachia ule mradi niumiliki km zawadi yake ya kumbukumbu kwangu...nami nilimpa vya kumbukumbu japo havikuzidi thamani ya ule mradi wake...yapata miaka 8 sasa toka aondoke na hatujawahi kuwasiliana maana wakati anaondoka alinambia hana ndoto tena km atarudi Tz.
 
Namshukuru ex wangu alinipiga chini kisa nilishindwa kumpa pesa ya kusuka. Akaniambia kwa style hiyo hutakuja to**ba demu mkali kuanzia Leo usinijue. Dah ikawa hivo bhana. Nilianza kuisaka pesa kwa nguvu zote. Alhamdulilah alinitia nguvu Sana mpk Sasa nasema yule manzi alitumwa na Mungu asee.
 
Yule chibonge alifanya nikajua kuwa mwiko ukiwa na ujiuji wa ugali wa moto ni siraha tosha na inaweza kuua!.. yule alienisevu kiberenge alifanya nijue kuwa nipo mbelembele kama kichwa cha tren nisie na subira ni mbele kwa mbele tu ndio maana akanisevu kiberenge!

Yupo huyo alifanya nikajua na nimesaini kabisa na ninaamini kuwa mapenzi bila pesa ni sawa na kumfumania kunguni akinywa maji ni zoezi gumu kwelikweli!.
 
Back
Top Bottom