Ni kitu gani kilimsibu Ndg Julius Mtatiro CUF?

Ni kitu gani kilimsibu Ndg Julius Mtatiro CUF?

Nyamemba

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
845
Reaction score
447
Julius Mtatiro mwanasiasa na mwanaharakati kijana ni miongoni mwa Vijana waliojipambanua katika medani za kisiasa toka alipokuwa masomoni UDSM.

Haikushangaza baada ya kumaliza masomo yake alipojitokeza kuutaka ubunge kupitia chama cha wananchi CUF, hata hivyo hakufanikikiwa juu ya adhima hiyo kwani Mh John John Mnyika - CHADEMA aliibuka kidedea, baadae kijana huyu machachari kwa siasa za Bongo kwa maana ya Tanzania alichaguliwa kuwa naibu katibu Mkuu wa CUF kwa upande wa Tanzania Bara.

Nisichokijua na ninachotaka leo tujadili ni kitu gani kilimkumba kigogo huyu hadi kupelekea kunyang'anywa nafasi yake na Mh Magdalena Sakaya? Mpaka leo hii bado yupo na hatujui nini kilimkumba ndg Mtatiro? Na pia nisichokijua, ile kazi ya kuchambua wanaoutaka ukubwa ndani ya CCM anaifanya kwa maslahi ya nani? Kwanini watia nia tu wa CCM? Kuna uzi hapa jf Yericko Nyerere aliwahi Kusema amenunuliwa na mojawapo ya kambi kufanya hiyo kazi, je hilo limekaaje? Kuna ukweli wowote?

Naomba tujadili.
 
Julius Mtatiro mwanasiasa na mwanaharakati kijana ni miongoni mwa Vijana waliojipambanua katika medani za kisiasa toka alipokuwa masomoni UDSM. Haikushangaza baada ya kumaliza masomo yake alipojitokeza kuutaka ubunge kupitia chama cha wananchi CUF, hata hivyo hakufanikikiwa juu ya adhima hiyo kwani Mh John John Mnyika - CHADEMA aliibuka kidedea, baadae kijana huyu machachari kwa siasa za Bongo kwa maana ya Tanzania alichaguliwa kuwa naibu katibu Mkuu wa CUF kwa upande wa Tanzania baba. Nisichokijua na ninachotaka leo tujadili ni kitu gani kilimkumba kigogo huyu hadi kupelekea kunyang'anywa nafasi yake na Mh Magreth Sakaya? Mpaka leo hii bado yupo na hatujui nini kilimkumba ndg Mtatiro? Naomba tujadili.

Pale kwenye zile nafasi za juu alikuwa "peke yake" nadhani kuna mambo alikuwa hakubaliani navyo. Hivi sasa Mtatiro yuko Imara kabisa chini ya UKAWA. Anapiga shule pale mlimani. Anatarajiwa kuwepo Bungeni kwenye bunge lijalo inshallah
 
Huo ni umbea sasa,kwani hujui kulifanyika uchaguzi,na kunakupata na kukosa?!
 
Ufafanuzi pekee yake maana yake nini.

Pale kwenye zile nafasi za juu alikuwa "peke yake" nadhani kuna mambo alikuwa hakubaliani navyo. Hivi sasa Mtatiro yuko Imara kabisa chini ya UKAWA. Anapiga shule pale mlimani. Anatarajiwa kuwepo Bungeni kwenye bunge lijalo inshallah
 
Swali zuri sana.
Kwa namna Mtatiro alivyopewa unaibu katibu Mkuu CUF ilikuwa ya haraka sana hivyo wengine tulitegemea pia ipo siku angevuliwa haraka sana.
 
Bado sijaelewa neno ''Peke yake''. Lakini kama ulitaka kuumanisha vileee basi Magdalena Sakaya atakuwa yuko ''Peke yake zaidi''
 
Swali zuri sana.
Kwa namna Mtatiro alivyopewa unaibu katibu Mkuu CUF ilikuwa ya haraka sana hivyo wengine tulitegemea pia ipo siku angevuliwa haraka sana.

Mimi nadhani huwa nafasi hiyo huwa inatolewa kwa zamu,kwa maana ya kipindi cha miaka mitano mitano au zaidi ya hapo au chini ya hapo.
 
Jamani mbona mnataka kufitinisha watu? Uchaguzi ndani ya chama ndio uliomuengua mtatiro na wala hakuna jambo jingine.
 
Bado sijaelewa neno ''Peke yake''. Lakini kama ulitaka kuumanisha vileee basi Magdalena Sakaya atakuwa yuko ''Peke yake zaidi''

Hapana mkuu, Fuatilia kwa ukaribu kati ya Magdalena na Sakaya kuna "kitu" hapo kinasahaulika kwa makusudi. Hicho ndio kinachomfanya Magdalena asiwe "mpweke" chamani.
 
Kwa sasa ni mwandishi wa makala kwenye gazeti la Mwananchi.
Anataka ubunge segerea japo hajafanya kazi yeyote ya kisiasa jimboni hapo!
 
Amewahi kuandika kuwa aliacha nafasi za kiungozi ili kupata muda wa kuongeza kiwango chake cha elimu, ameshapata Masters yake na sasa anasomea degree ya Sheria.
 
Kwa sasa ni mwandishi wa makala kwenye gazeti la Mwananchi.
Anataka ubunge segerea japo hajafanya kazi yeyote ya kisiasa jimboni hapo!

True! Nitawashangaa sana chadema wakitoa hili jimbo kwa cuf!
 
Uchaguzi tu labda wewe unajua zaidi tuambie maana Mimi sioni kingine
 
Uchaguzi tu labda wewe unajua zaidi tuambie maana Mimi sioni kingine

Mtatiro alisema mwenyewe kuwa hagombei uongozi CUF anataka autumie muda wake kusoma shule. Kilichotushangaza ni kuwa ameshindwaje kujipanga? Mbona mawaziri kina Juma Nkamia hivi sasa ndo wanasoma digrii ya kwanza pale yudom? Nkamia ni naibu waziri.
Mama wa kambo wa W. J. Malecela bi Anna Kilango amemaliza B.A yake kwenye Education akiwa mbunge. Mtatiro ameshindwa nini kusoma na kujenga chama? Ndio 'watu' wakadai eti alikuwa 'mpweke' chamani. Si unajua tena maneno ya watu?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom