Ni kipi hasa kilichomuondoa Balozi Ombeni Sefue ikulu? Atapangiwa kazi gani nyingine?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,596
36,018
Tumekuwa tukipaza sauti kuwa mtu anayeondolewa kwenye nafasi yake ya utumishi basi ni lazima zitolewe sababu za msingi za kuondolewa kwake! Haiwezekani katibu mkuu kiongozi anaondolewa kimyakimya tu huku tukiwa hatupewi sababu za kuondolewa kwake!

Kiongozi huyu alikuwa akitoa matamko mbalimbali huku rais Magufuli mwenyewe akituaminisha kuwa ni mtu wa viwango na anayekidhi kile anachokiita "speed yake" Leo kulikoni?

Hatupingi kuondolewa kwa watu hawa kama wamefanya makosa! Lah! Tunapinga namna wanavyoondolewa huku kukiwa na sintofahamu ya hali ya juu!

Tulishuhudia Daktari Hoseah akitenguliwa uteuzi wake kimyakimya! Pia wapo watumishi wengine wengi huku mambo lukuki yakifichwa!

Sasa leo tunaambiwa kuwa Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine? Ipi? Cheo cha katibu mkuu kiongozi ni cheo cha nne kwenye mhimili wa serikali! Atapangiwa kazi gani? Waziri mkuu? Makamu wa rais? Rais? Kutumbuliwa kwake kunaonyesha kuwa alikuwa na kasoro katika utendaji wake na si vinginevyo! Zipi?

Hali hii ya kufukuzana kimyakimya inaweza kuzua uhasama wa aina yake nchini! Kwanini mtu akifukuzwa na au kusimamishwa kazi zisitolewe sababu za msingi zilizopelekea kuondolewa? Nini tatizo? Tunajenga nini?

Angalizo kwa wana JF: Wakati Ombeni Sefue akitoa matangazo mbalimbali wengi wenu mlikuwa mkishangilia! Wengine mkadiriki kuandika kuwa Ombeni, Magufuli na Majaliwa wanatosha kuendesha nchi! Mkasema kuwa hakuna haja ya baraza la mawaziri! Leo Ombeni Sefue anatenguliwa mnashangilia kwa maandiko mbalimbali! Mmesimamia wapi? Hamuoni kasoro za wazi kwenye huu utenguaji wa watumishi (baadhi yao? ) Mimi ni miongoni mwa wale tunaoamini kuwa, kama ni kusafisha kwa kwelikweli! Hata Magufuli mwenyewe ni jipu!
 
Nahisi linakuuma hili jipu. Angalizo tu sio kila anae badilishwa ama kuachishwa kazi katumbuliwa. Mengine ni kwa ajili ya masilahi mapana ya taifa. Hatuwezi tukaendelea kukaa na watu walewale kila siku. Tunahitaji mabadiliko na ndo hayo. Tunaamini viongozi wetu wanafanya kwa nia njema na sivinginevyo. Mungu ibariki tz
 
Aliachwa tu ili atoe ushirikiano kwa serekali mpya. kiufundi hakustahili kuendelea wakati aliyekuwa amemteua ndio huyo imedhihirika madudu aliyokuwa anayafanya, hivyo hatua nyingi zilizokuwa zinachukuliwa zilikuwa zinamuacha uchi hata yeye. kocha mpya.akiingia.anakuja na timu yake ya wasaidizi wanaotambua ma.kuikubali falsafa yake. Na huo sio mwisho, wakuu wengine wa idara na taasisi za umma lazima wafanyiwe mabadiliko ili rais aweze kufanya kazi kwa mbinu zake na sio kutumia hao aliowakuta ndani ua uchafu
 
Tumekuwa tukipaza sauti kuwa mtu anayeondolewa kwenye nafasi yake ya utumishi basi ni lazima zitolewe sababu za msingi za kuondolewa kwake! Haiwezekani katibu mkuu kiongozi anaondolewa kimyakimya tu huku tukiwa hatupewi sababu za kuondolewa kwake!

Kiongozi huyu alikuwa akitoa matamko mbalimbali huku rais Magufuli mwenyewe akituaminisha kuwa ni mtu wa viwango na anayekidhi kile anachokiita "speed yake" Leo kulikoni?

Hatupingi kuondolewa kwa watu hawa kama wamefanya makosa! Lah! Tunapinga namna wanavyoondolewa huku kukiwa na sintofahamu ya hali ya juu!

Tulishuhudia Daktari Hoseah akitenguliwa uteuzi wake kimyakimya! Pia wapo watumishi wengine wengi huku mambo lukuki yakifichwa!

Sasa leo tunaambiwa kuwa Ombeni Sefue atapangiwa kazi nyingine? Ipi? Cheo cha katibu mkuu kiongozi ni cheo cha nne kwenye mhimili wa serikali! Atapangiwa kazi gani? Waziri mkuu? Makamu wa rais? Rais? Kutumbuliwa kwake kunaonyesha kuwa alikuwa na kasoro katika utendaji wake na si vinginevyo! Zipi?

Hali hii ya kufukuzana kimyakimya inaweza kuzua uhasama wa aina yake nchini! Kwanini mtu akifukuzwa na au kusimamishwa kazi zisitolewe sababu za msingi zilizopelekea kuondolewa? Nini tatizo? Tunajenga nini?

Angalizo kwa wana JF: Wakati Ombeni Sefue akitoa matangazo mbalimbali wengi wenu mlikuwa mkishangilia! Wengine mkadiriki kuandika kuwa Ombeni, Magufuli na Majaliwa wanatosha kuendesha nchi! Mkasema kuwa hakuna haja ya baraza la mawaziri! Leo Ombeni Sefue anatenguliwa mnashangilia kwa maandiko mbalimbali! Mmesimamia wapi? Hamuoni kasoro za wazi kwenye huu utenguaji wa watumishi (baadhi yao? ) Mimi ni miongoni mwa wale tunaoamini kuwa, kama ni kusafisha kwa kwelikweli! Hata Magufuli mwenyewe ni jipu!

NAJUA UMRI WA KUSTAFU ULIIISHA FIKA.PILI SUALA LA NSSF HUENDA LINAONDOKA NA WATU WENGI KWANI TAARIFA NYINGI ZIMEKUWA ZIMEKUWAZIKIWEKWA HADHARANI HAPA.NADHANI RAIS AMEZIFANYIA UCHUNGUZI NA AKAONA KUNASHIDA AFADHALI KUMSTAFISHA BILA KASHIFA KULIKO KUMUACHA HALFU AKADHALILIKA WAKATI MUDA WA KUSTAFUN ULIISHAFIKA.
NASHANGAA UNAJIULIZA HILI,MBONA KAGAME AMEKUWA ANAWANDOA TU NA KUWAPELEKA MAHAKAMANI.
 
huyi jamaa si kaondolewa siku tatu baada ya lile gazeti la dira kuandika kashfa zake?
nikiunganisha dots hapa naona hii sio coincidence, magufuli ameona jamaa yake kaanikwa akaamua amtoe,
ila hapo aliposema kapangiwa kazi nyingine ndio kizungumkuti, kwa mtu mkubwa kama yeye akipangiwa kazi nyingine tulipaswa kuambiwa ni kazi gani
 
Hongera Balozi John Kijazi kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Ulipoteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania India kuchukua nafasi ya Balozi Eva Nzavo ulikuja kutuunganisha Watanzania na kuleta harmony ambayo haikuwepo baina yetu Watanzania na pia baina yetu na Ubalozi ingawa assault iliyofanywa kule Bangalore dhidi ya wanafunzi wa Kitanzania kwa mtazamo wangu hivi majuzi haikuwa handled properly lakini sitakuhukumu moja kwa moja .

Leo miongoni mwa viongozi wa Jumuiya za Watanzania Uliowaongoza kwa namna moja au nyingine bado utaendelea kukwaruzana nao

Nape Nnauye(Akijisomesha na Taasisi Binafsi) -Aliyekua kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania Ukanda Kusini Mwa India (Bangalore)ni Waziri katika serikali unayoiongoza kama Chief Secretary

-Ben Saanane (Akisomeshwa na Serikali ya Tanzania)-Aliyekuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania Kaskazini (Allahabad) ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti ya Chama kikuu cha upinzani dhidi ya Chama chako Tawala .Watch Out!

Nakutakia kila la Kheri ,Mapambano yanaendelea.

So far tuna

Agness Kijazi-Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa

Allan Kijazi-Mkurugenzi TANAPA

John Kijazi-Incoming Chief Secretary

Wasiibuke watu na kulalamikia majina badala ya competency yao sasa.

Vilevile asiibuke Mtu akakumbushia Tuhuma juu yako kuhusu mchezo usiofaa katika upanuzi wa barabara ya Chalinze-Segera kabla Hujateuliwa Kuwa Balozi India. Nimekemea (Kidding).
 
No one is perfect.kajitengenezea kitambulisho cha kazi juz tu leo hakina kazi.
 
Nadhani( sina uhakika) kosa lake itakuwa Ameshirikiana na Waziri mmoja kushauri Mamlaka kubadilishwa kwa Mkurugenzi mmoja kwa lengo la kuweka Mtu wao awe Mkurugenzi ambae si Mtanzania wakijua hilo tena mwenye elimu ya Internet ( E Goverment) ambayo haina tija kwenye taasisi hiyo inayohitaji mjuzi wa Masuala ya Uchumi na Uwekezaji na wakapinga Mkurugenzi wa Operation wa Taasisi hiyo kupewa u DG, Mbaya zaid kubariki Waziri kujipa Mamlaka ya kuteua Kaimu Mkurugenzi Mkuu kazi ambayo ni ya Mkuu wa Nchi peke yake.
 
Back
Top Bottom