Ni kiongozi gani wa kisiasa ana hotuba kali za kumbadilisha mtu?

Zito ni Kijana mwenye uwezo kweli wa kujenga hoja hasa kwa matukio anayoyaibua,maana ndio anajua ataanza vipi na kumaliza mjadala namna gani,ila kwa Utoaji wa Hotuba nampa 35% tu.
 
January Makamba ni kiongoz ambaye ana hotuba zenye mashiko ya kitafiti na za mvuto wa kisiasa' ukiacha mkuu wa nchi naamin January ndiye kiongoz mwenye hotuba za ushawishi,
 
Agrey Mwanri hujikakamua kushughulikia matatizo madogo madogo,Pia kwa upande Hotuba ni vitisho na mikwara tu.
 
Kati ya mwaka 2008 hadi 2010 niliwahi kumsikia Mh.Mbowe akihutubia Uwanja wa Mkendo Manispaa ya Musoma.

Alizungumzia mambo mengi ila alipoanza kulizungumzia suala Ufisadi wa EPA ndani ya BOT.

Nakumbuka siku ile watu walikuwa wengi sana walihudhuria wakiwemo wanachama na wapambe wa CHADEMA,CCM,CUF na wengi wasiokuwa wanachama wa chama chochote kile.

Kijana aliyeonekana kavalia Tisheti ya njano ikiwa inaashiria yeye ni mwana ccm aliyekunywa mpaka maji ya Bendera kama kiapo cha kutokukiuka masharti ya chama hicho.(kama wasemavyo watu)


Kijana huyo alionekana kumfuatilia Mbowe kwa makini wakati akiongea,Kijana aliyeaminiwa na ccm kuwa kamwe haitatokea akikane na kukiacha CHAMA CHA MAPINDUZI,ailiposikia fedha zile zikipangwa moja moja kutokea TZ zitafika Cairo Misri alipiga Yowe la nguvu UUWIIIII!!! HUKU AKICHANA ILE TISHITI ALIYOKUWA AMEIVAA MBELE YA HADHARA YOTE AKABAKIA KIFUA WAZI.

Kwa tukio hilo kutokea yamkini ilituthibitishia kwamba Hotuba ya Mbowe ilibeba ujumbe mzito mpaka kijana akaona haina maana ya kuendelea kuvaa Tisheti ya CCM huku akizidi kuwa masikini na Wakati huo huo Wengine wakiyala mema ya Nchi kwa kuifisidi Nchi kaa Mchwa anayatafuna Nyasi.

Wewe unaonaje? Mh. Mbowe aweza kuwa kiongozi wa Kisiasa mwenye Hotuba kali kiasi cha kuwabadili wengi na kuacha vyama vyao na kujiunga na CHADEMA?

Nawasilisha kwenu Wanajamii.

macho kumchuzi kazi yake dj, na kumbi za starehe
 
Mbatia ni vigugumizi tu vimetawala alifunikwa na Mbowe walipomwalika kwenye Uchguzi wao wa ndani ya NCCR-Mageuzi.
 
Dr Slaa ninamkubali sana ni Kiongozi mzuri wa Kizazi hiki ila kwa mambo Hotuba sidhani kama anamfikia Chairman wake F.A.Mbowe.
 
Wa kwanza naweza kusema ni Mwl. Nyerere then akifuatiwa na Hitler pamoja na Mussolini.

dah siku yangu ya leo nimeianza vizuri!!!! umenitajia
hao wote wawili hitler & mussolin,, nawakubali sana hawa watu,,, sijui lini tanzania itaongozwa na watu kama hawa,,,, napenda niwe hai ikifika hui siku!!!!
 
hivi kuna mtu ameewah msikia mchungaj msigwa akitoa hoja bungeni?? au mnaonesha mahaba tu kwa watu muwapendao me naongea reality sikiliza vyombo kutoka kwa msigwa ana akili sana huyu jamaa na anafikira sana tafuta video zake YouTube msikilze ndio utajua nan anajenga hoja.

hoja sio kupingana na mtu fulan hoja ni kutafuta ufumbuzi wa matatzo tulonayo kama CCM ni tatzo isemwe kwa hoja
 
Back
Top Bottom