Ni kifungu gani kinamlazimisha mwanaume wa kikristo kuwa na mke mmoja?

shetani ame create id huku jf
 
Hapo Mathayo 19:5B umesema na hao wawili watakua mwili mmoja na sio hao watano au watatu.
 
Hapo Mathayo 19:5B umesema na hao wawili watakua mwili mmoja na sio hao watano au watatu.
Lakini wanaofanya makubaliano ya kuoana ni wawili ndio maana amesema na hao wawili. Kwa mfano ukioa mke wa kwanza ninyi wawili mnakuwa mwili mmoja na ukioa wa pili hivyo hivyo mnakuwa mwili mmoja, yaani mwili mmoja unahusisha ninyi mlioingia makubaliano ya kuoana hata kama mmojawapo yuko mwili mmoja na mtu mwingine. Samahani najaribu kutoa tu mawazo yangu....ni katika kujifunza tu zaidi
 
Zaman nilikuwa nikitaka kuongea na mtu anauliza maswali tashititi kama mtoa Uzi huu nilikuwa namuuliza alikuwa wangapi darasan. Yaan vifungu vyote vya biblia alivyonukuu vinampa majibu ya swali lake lakini bado eti haelewi.
1. Unasema Mungu akafanya mwanamke akamleta kwa Adam. Huo ndo mpango wa Mungu toka uumbaji mwanaume awe na make mmoja. Kwan alishindwa kumletea zaid?
2. Mwanaume atamuacha baba na mama anaambana na mkewe nao wanakuwa mwili mmoja. Mbona iko wazi wapi unakwama? Je Yesu hakujua wingi na umoja? Watu wameungana na kuwa mwili mmoja wanawezaje kuungana na watu na wanne nk.?
Kifupi nukuu zote hakuna sehemu anapoambiwa awe na wake wengi. Kwani mwenzetu unakwama wapi hasa
 
Hongera kwa kuwa na akili darasani
 
Ahsante mkuu lakini hivi ukisema huyu ni mwanangu mwenyewe maana yake yuko mmoja sio?
"Huyu ni mwanangu mwenyewe", kauli hii inaashiria umoja maana kama ingekuwa wingi, kunapaswa kuwa na neno 'wanangu' na sio 'mwanangu'.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…