Ni kesi ya udhalilishaji, au?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni kesi ya udhalilishaji, au?!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by NasDaz, Feb 23, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,307
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280

  Kuna mshikaji mmoja anafanya kazi kwenye benki moja nchini. Wakati huo tulikuwa tunafanya kazi pamoja. Mwaka 2006 kuna mteja alipeleka madai kwenye tawi analofanyia huyo jamaa kwamba alimwachia kiasi cha shilingi milioni tano ( 5M ) ili amuwekee kwenye akaunti yake. Madai ya mteja huyo yalikuwa kwamba pamoja na kumwachia huyo staff Shs. 5,000,000/= lakini huyo staff hakuziweka pesa hizo kwenye akaunti ya mteja. Na huyo staff alipoulizwa endapo kweli aliachiwa pesa na huyo mteja, yeye akakanusha kuachiwa pesa. Kutokana na hilo, huyo mteja akaambiwa alete copy ya deposit voucher. Mteja akasema hakuwa na copy! Pamoja na hayo, staff wa tawi husika wakaanza kutafuta original vourcher toka kwenye vocha zote za mwezi ambao mteja alidai kwamba alileta hizo pesa. Hata hivyo, hakukuonekana vocha yoyote! Mteja akaambiwa atoe ushahidi wowote unaweza kuthibitisha madai yake. Kutokana na hilo, akadai kwamba siku aliyofika hapo benki kulikuwa na foleni kubwa sana ya wateja. Na kwavile yeye alikuwa hajiskii vizuri (alikuwa anaumwa) akamuomba mteja aliyekuwa mbele zaidi ampe nafasi ya mbele yake. Yule mteja aliyeombwa, akakubali na kumpisha mlalamikaji. Mlalamikaji alivyopishwa mbele, akachukua kitita chake na kumwachia huyo mshikaji staff( ni Teller). Baada ya kuacha hicho kitita, mlalamikaji akaondoka huku akiamini pesa zitakuwa deposited kwenye akaunti yake.

  Uongozi wa tawi la benki ukachukua jukumu la kumuita huyo mteja ambae mlalamikaji alidai alimpisha. Huyo mteja alipoulizwa endapo anakumbuka kumpisha mlalamikaji, akakubali kwamba ndio alimpisha ingawaje hafahamu kama hizo pesa aliacha au hapana. Baada ya kuona utata huo, nikachukua jukumu la kupitia transaction zote (kwenye system ambako niliamini suala la kupotea vocha halipo) zilizofanyika hiyo siku, ajabu ni kwamba sikuona transaction ya aina yoyote iliyofanywa na huyo mteja ambae alijivika ushahidi. Nikapitia akaunti ya huyu mteja mpya (shahidi), kwa kuangalia siku saba mbele( i.e. siku saba baada ya siku iliyodaiwa kufanyika hiyo transaction) na siku saba nyuma lakini nikakuta mteja huyo nae hakufanya transaction yoyote na benki. Kwavile tawi lenyewe si kubwa sana na wateja wetu wengi tunawafahamu, nilianza kupitia akaunti ya mkewe shahidi kama nilivyofanya kwa shahidi mwenyewe. Nako hakukua na transaction yoyote iliyofanyika kwa kipindi hicho chote! Kwavile nafahamu yule shahidi ana tabia ya kutuma tuma pesa kwenda kwao, basi nikaamua tena kupitia transaction zote za tawi za muda wa wiki mbili ili nione endapo kuna money transfer yoyote iliyofanyika kuelekea mitaa ya mikoa ya anakotoka yule shahid. Hapo napo sikuona transaction yoyote ya money transfer kuelekea mikoa ya mteja huyu shahidi! Hapo nikajiuliza, sasa huyu mteja anayedai alimpisha mwenzake alikuja benki kufanya nini wakati hakukuwa na transaction yoyote ambayo angalau tu inafanana fanana na yeye! Nikawasilisha findings zangu kwa branch management nao wakamuita tena huyu mteja shahidi na kumuuliza endapo ana uhakika alimpisha mlalamikaji! Shahidi huyu akasimama kwenye madai yake kwamba kweli alimpisha! Alipobanwa alikuja benki kufanya nini, tena siku iliyokuwa na wateja wengi kiasi hicho wakati hakuna transaction yoyote iliyofanywa na yeye au mtu wake wa karibu( kwamba labda alimwagiza); jamaa akagwaya! Alipobanwa sana akatoa siri kwamba hakuwahi kumpisha huyo mlalamikaji isipokuwa alisema hivyo kwavile alilishwa bia (Mlalamikaji alikuwa anamiliki bar)!
  Baada ya kuona hivyo, branch management ikaitisha kikao kilichotuhusisha wote pamoja na mlalamikaji. Bado mlalamikaji aliendelea kudai ni kweli aliacha hizo pesa, lakini sasa kauli zake zikawa zinakinzana mara kwa mara. Na mlalamikiwa nae akaendelea kukataa! Kufikia hapo, kama tawi tukaona issue ishakuwa tight kwetu-kwamba ilituzidi kimo! Kutokana na hilo, branch management ika-foward hiyo issue Head Office ambako nako wakatuma watu wawili kwa nyakati mbili tofauti kufanya management audit. Wote, hawakupata japo chembe ya ushahidi wa kumtia hatiani mlalamikwa (bank staff). Aidha, mlalamikaji akaarifiwa juu ya matokeo ya auditing iliyofanyika.
  Suala lenyewe, likaishia hapo!
  Jumamosi iliyopita, mteja yuleyule (mlalamikaji) akapeleka suala lake lile lile polisi hapa ikiwa imepita miaka zaidi ya mitatu! Ingawaje polisi wale wanafahamu jamaa anapatikana wapi, walimvizia hadi alipotembelea sehemu za public na huko huko wakamuibukia na LandRover 110 ! Walifanya hivyo jioni ya jumamosi, na kwavile haikuwa siku ya kazi jamaa akalazwa mahabusu. Baada ya kufanya utafiti, ikaonekana kwamba hata huyo mlalamikaji mwenyewe hakuwapo kwenye mji huo-jambo linalozua hofu kwamba huenda alitoa maagizo yake kw simu. Kutokana na mchezo wenyewe ulivyofanyika, kuna hofu kwamba mlalamikaji huyo alifanya hayo makusudi kwa lengo la kumdhalilisha. Na kweli, jamaa kadhalilika ile mbaya-kama mjuavyo, kwenye vimji vidogovidogo banker ni mheshimiwa ile mbaya- na unaweza ukakuta unafahamika na kila mkazi wa mji na vitongoji vyake!!!! Nasikia the whole town, stori ni kuhusu jamaa kukamatwa na polisi! Vilevile kuna hofu alikula njama na baadhi ya askari ili kufanikisha azma hiyo. Hofu hiyo inatokana na maswali kama:
  · Ni kwanini polisi walisubiria hadi jumamosi jioni ndipo wakamkamate huyo jamaa wakati wangeweza kumkamata siku hiyo hiyo ambayo walipelekewa malalamiko! Isitoshe, jamaa mwenyewe anakaa jirani sana na kituo cha polisi na wote wanamfahamu. Hapa watu wana hofu kwamba walifanya hivyo makusudi kwavile asingeweza kupata muda wa dhamana na hivyo zima ya kumdhalilisha ingetimia.
  · Taarifa zilizopo (mimi sipo huko hivi sasa, kwahiyo hapa naongea nilichoiskia) ni kwamba kutokana na ukorofi wa huyo mteja, ama wiki chache, au miezi michache iliyopita, benki imepiga mnada nyumba yake baada ya kugoma kulipa mkopo ambao alikopeshwa na benki. Binafsi sina hakika endapo aligoma kulipa au hakuwa na uwezo wa kulipa; ingawaje yote sio excuse especially kama alikuwa less cooperative! Baada ya nyumba yake kupigwa mnada, inasemekana huyo mteja akaanza kujitapa mitaani kwamba lazima benki watamtambua! Kutokana na hilo, bila shaka akaanza kutafuta nani mnyonge wa kuanza nae; akampata jamaa!

  Kutokana na maelezo hayo hapo juu, jamaa anasubiria mwisho wa sakata hili jipya ili amfungulie mashitaka yule mteja-mashitaka ya kumdhalilisha. Je, suala hilo linawezekana kisheria? Au ni mashitaka gani zaidi ambayo anaweza kuyafungua dhidi ya huyo mteja?
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  font mkuu imenitia uvivu kusoma.......maandishi madogo
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,933
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  Dah huyo Teller mpe pole sana, mambo kama haya kwenye kazi yapo sana. hakukuwa na uhasama wa kibinafsi kati ya huyo mtemi na teller? au Teller kala mali za huyo Bingwa?
   
 4. bht

  bht JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  asante now I can read.........
   
 5. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 366
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hakika huo ni udhalilishaji wa mchana kweupe peee!Kuna sheria unaweza kumfungulia mashtaka lakini kwa mfumo wetu usio wa haki nachelea kukuambia ahame mji huo tuu maana kitakachofuatia ni kibaya zaidi.
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,768
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  hhahaha now B what is ur opinion?

  nadhani polisi watamwambia kwa nini walimkamata, then from hapo atajua afungue kesi gani kama defamation au la!
   
 7. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,307
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kwa hilo, lakini nililokuwa na uhakika nalo ni kwamba huyo mteja ni mkorofi kishenzi. Nakumbuka kuna mshikaji fulani alishawahi kumzushia kwamba anatangaza siri za akaunti yake, kwa bahati mbaya hapo alikumbana na kisiki kwavile jamaa alimpandishia kishenzi na akamwambia akashitaki kokote-akanywea! We si unaona tu hata mkopo wa benki kashindwa kulipa kwa jeuri tu!!!
   
 8. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,307
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  Polisi tayari washaanza kujichanganya na maelezo yao!! In short na wao wameshagundua wamechemsha!
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  sasa mbona umenijibia!!!!

  alafu tena kama mtu mwenyewe ndo huyo kafilisiwa na benki sasa fifia ya kumdhalilisha ataweza kulipa kweli..
  wee NasDas mwambie huyo mshikaji wako akamfunfulie hiyo kesi ya kumdhalilisha na amlipe fidia kadhaa. vya yeye kuweza au kutoweza kumlipa mlalamikaji ni huko mbele kwa mbele anagalau hiyo itampa jamaa yako relief na kumsafisha hata kwa jamii amabayo kwa sasa wanamuona ni mchafu...
   
 10. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh kisa kirefu kweli lakini kinasikitisha sana.,anaweza kufungua kesi ya Malicious Prosecution ambayo ni Tort, lakini hii ni baada ya hiyo kesi aliyofunguliwa kwisha na mahakama ishindwe kumtia hatiani.,hapa anaweza kudai fidia nzuri tu.
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,307
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280

  i got u mkuu
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,900
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Wasanii ni wengi sana tuwe makini.
   
 13. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,160
  Likes Received: 915
  Trophy Points: 280
  Tatizo la polisi wetu ni watu wa mishiko. Na mishiko yenyewe basi ni mikia ya mbuzi unaweza kukuta mchezo wote huo wamelambishwa haizidi elfu ishirini. Shame to them. Washeria mnasemaje? Kwangu kuna kesi ya udhalilishaji na kutoa taarifa za uongo polisi
   
 14. Devils Advocate

  Devils Advocate Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 16, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ya kutoa taarifa ya uongo polisi inaweza isifanikiwe sana kwa sababu polisi wenyewe ndio hao wanaohusika. kwa hili labda PCCB wanaweza.

  Lile la kudhalilishwa kwa kweli ni malicious prosecution ambayo ni Tort na ni kesi ya daawa. if the facts are as stated na kuna mashahidi wa kutosha then possibility ya kushinda ni kubwa sana.
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,307
  Likes Received: 1,679
  Trophy Points: 280
  Mkuu, sijapindisha fact hata kwa nukta moja!!! sana sana nilichopindisha ni amount ambayo huyo mteja anadai alimwachia huyo teller- amount ipo chini ya hapo na nimefanya hivyo ili kutotoa picha halisi ya wapi hiyo issue imetokea coz' siwezi fahamu nani na nani anaweza kusoma hii story!! inaweza kusomwa na wahusika halafu wakapotosha! and i hope kutotaja actual amount hakuwezi athiri the content of story. Mashahidi ni full mkoba, coz' issue inafahamika at branch level ( wote wanafahamu) na hata head office coz kama nilivyosema b4, ilifanyika management audit kwa ajili ya hiyo issue! But all in all, thanks for advice
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...