Mkuu ni hatari sana. Tena bora mara Mia uende shule kuliko kupoteza Muda. Other ways unaweza ukasimama na nchiBora wewe umeliona hilooo....wengine wako bize na tar 1 Sept....utasikia
1-ukuta
2-ukum
3-siku ya usafi kwa majeshi
4- siku ya kupatwa jua
5-.........
6-.......
Natamani nirudi shule nikuchukuwe masters na PhD n dani ya miaka mitano inji ukiwa imesimama mie niwe nimegain education.
Sitaki kusimama na nchi iliyoamua yenyewe kuisimamisha.
mm pia huwa nashangaaa sanaa siasa kuingilia professionalsNa bado
Hongera kwa kutambua mkuu. Ila Mimi sasa hivi najipanga ili nihamie Kenya, baada ya miaka 5 nitarudi. Siwezi kukubali kupoteza muda wangu hapa wakati kila dalili za hali ngumu ya maisha zinaonekana. Na watawala wetu wametia pamba masikioni.Wakuu wa Wilaya na mikoa, wakuu wa Polisi, wote wanahisi kuwa jukumu lao kubwa la kikazi ni kuhangaika na wapinzani. Kwa bahati mbaya hakuna hata tofali moja la kiwanda linalotengenezeka kwa kudhibiti upinzani.
Tunatumia gharama kubwa ikiwa ni pamoja na muda mwingi kuhangaika na vitu vya kijinga, vitu ambavyo haviwezi kulisogeza Taifa hili hata hatua moja mbele, huku kuna mambo mengi ambayo tungehangaika nayo, wote kwa pamoja kama Taifa, yangeweza kusogeza mbele Taifa letu.
Watawala ni muhimu wakatambua kuwa hakuna hata siku moja ambapo watu wote watakuwa na fikra za aina moja, yaani wote wakakuunga mkono kwa kila jambo na kwa wakati wote, ukilazimisha utawapoteza hata wale ambao walikuwa wakikuunga mkono.
Hali ngumu ikiwa kwako usifikiri na kwa wengine ni hivyo hivyo. Binafsi naona mambo murua kuliko kipindi kingine chochote.Binafsi nahisi ni kama Tanzania kwa sasa hivi tuna wakati mgumu kuliko kipindi chochote cha uhai wa nchi hii kilichopita.
Sasa hivi wataalamu wote wa nchi hii wanakwazwa na wanasiasa ambao 100% hawana utaalam wowote. Doctor msomi na mzoefu kazini anaweza kufukuzwa kazi na mkuu wa wilaya! Ambaye hata kusoma na kuandika hajui vizuri. Ni hatari sana.
Hatari kubwa zaidi ni viongozi kujaribu kuyatumia majeshi yetu kisiasa. Hii ni hatari kubwa kuliko wao wanavyofikiri. Kama hali itaendelea hivi, basi kuna Siku haya haya majeshi yetu na yenyewe yatatamani kutawala. Hakuna atakayeweza kuyazuia.
Nchi imekosa dira kabisa. Wananchi hawajui wafanye nini! Kwa mfano. Mwaka huu wakulima wamelima nyanya na mazao ya mboga mboga kwa wingi sana. Wengi walihamasika baada ya kiongozi wetu kuwaahidi kuwa ni Tanzania ya viwanda. Matokeo yake kila mkulima analia. Nyanya hazina bei na hakuna hata kiwanda kimoja cha kusindika nyanya. Zinaozea mashambani.
Wakulima wa nyanya ni kilio kila kona ya nchi hii. Sasa hivi tenga moja la nyanya ambalo lina wastani wa kilo 30 bei yake ni Tsh elfu tatu (3000) hakuna juhudi zozote za kuwaokoa hawa wakulima. Waziri anayehusika na viwanda hawezi kufanya lolote la dharura ili kuwaokoa hawa wakulima kwa sababu anaogopa bila sababu. Sasa kama hatuwezi kuhifadhi hata mazao yetu tunayolima, je ni viwanda gani tunafikiri tunaweza kumiliki?
Kila kiongozi mwenye taaluma anaogopa kufanya maamuzi kwasababu nyuma yake kuna anayemsimamia ambaye ni mwanasiasa asiye na taaluma yoyote. Yeye taaluma yake ni kutafuta sifa tu, madhara yake ni makubwa kuliko tunavyofikiri. Tusipobadilika mapema, tutakwama sana na tunastahili kukwama.
Viongozi wetu ni Kama wamechomwa sindano waka paralaizi. Hakuna wa kumstua mwingine. Wao bado wanafikiri wako kwenye kampeni wakati tayari tulishawachagua. Nasikitika sana.Na pia ukichukulia tishio la watoa maoni kwenye mitandao basi hata yale mawazo ambayo outwardly hudahiwa ni ya kijinga lakini ndio yanawasaidia wenye PhD zao kufikiri kwa usahihi yamesimama!
Hali ngumu ikiwa kwako usifikiri na kwa wengine ni hivyo hivyo. Binafsi naona mambo murua kuliko kipindi kingine chochote.
Jiongeze, Ongeza ubunifu, challenge ni kawaida pambana nazo.Hongera ndugu yangu, mimi nilikua na kibanda nilikua nauza 80,000/ kwa siku ila juzijuzi nimefunga kibanda kwani nilianza kuuza 3,000/ kwa siku.