Ni ipi 'short course' nzuri?

thatone

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
365
196
Habari JF,

Nina mdogo wangu alimaliza kidato cha sita akapata division 3.17 akakataa kwenda diploma akidai kuwa atajiendeleza hapo badaye.

Lakini anataka zile kozi fupi fupi kama miezi 6, mitatu. Je, ni kozi gani ambayo anagalau mtu unaweza kusoma na kujiendeleza kimaisha?

Ushauri tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aangalia interest yake, kuna dogo alimaliza six akajikita kwenye driving! Kumbe ndiyo interest yake na kwa kuwa aliipenda aliona mbali!

Kaajiriwa kama dereva kwenye mashirika ya UN, anapiga maisha yake kama kawa, hata waliosoma mpaka masters wanamuonea wivu!

Kama anautundu na computer kuna graphics design, animations!

Carpentry, anakuwa show room yake ya kufa mtu! Ufundi magari, kuna gari za kisasa ni computerized hazihitaji nguvu ni akili!
 
Mimi nashauri kitu kimoja tu

Awe kama Mimi tu baada ya kumaliza six tu

Nikafungua account jamii forum wiki tatu tu zilitosha kupata wazo la nini nifanye

Na ilo wazo nilipopeleka home nilionekana nimekuwa kiakili

Nampaka leo maisha yanaenda ndo maana napenda sana jamii forum

computer engineering
 
Mimi wakati nasoma nilichukia sana shule. Nikawa sisomi wala sihudhurii prep. Kuzurula sana nje ya shule lakini si mkorofi kivile na dini kwa sana. Nikafanya paper nikijiaminisha sihitaji kwenda chuo, ile watu wanahangaika hatua za mwisho mimi nalala. Nikapiga paper nikaingia kitaa tu nikalazimika kuhonga kupata kazi.

Matokeo yakatoka hata sikuhangaika kujua nikaja ambiwa two days later na mshkaji wangu. Lengo langu nifanye kazi mwaka mmoja nitoke na milioni 5 ( maana kuna gharama za maisha, kula, vocha, etc) nikajiajiri.

Nilifanya kazi miezi mitatu tu nikanyanyasika hapo nyumbani sitaki kuelewa mtu, baadae nikagundua mtaa ni mgumu vibaya mno. Nikaacha ujinga nikaapply vyuo nikapata sasa niko nasoma na mkopo sina. Pale kazini nilitoka na 1.2M sijui iliishaje hata, niliishi kishetani miezi mitatu siwezi sahau.
Shule muhimu mtu haniambii kitu.
 
Back
Top Bottom