Ni ipi ligi bora kati ya La Liga na EPL?

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,577
18,904
Kumekuwa na mjadala mkubwa sana kuhusu ipi ni ligi bora kati ya la liga na EPL. Niseme kitu kimoja ambacho kinawachanganya watu ni vitu viwili: ushindani na ubora, watu wameshindwa kutofautisha both things.

Ligi ya Uingereza ni ligi ya ushindani lakini si bora, ukiangalia team kama Man U na Arsenal zina wachezaji baadhi ni wa kawaida ambao hata wakienda Leicester City number hawapati. Ndo maana wakicheza na team ndogo wanapata shida.

Ukiangalia team ya Man City ambayo ndio team bora kwa sasa EPL, ukimpeleka UEFA kajitahidi sana ni robo fainali. Kiufupi hawafanyi vizuri sana UEFA; mwaka jana kidogo ndo wamefanya vizuri lakini miaka 10 iliyopita mfululizo vilabu vya Hispania vime-dominate.

Ligi ya Hispania imekuwa ikifanya vizuri kutokana na ubora wa wachezaji walionayo pamoja na soka wanaocheza ndo maana vilabu vya uingereza vikikutana na vilabu vya hispain wanapata shida Sana.

Hitimisho: ingawa me ni mshabiki wa epl lakini kuhusu ubora wa ligi naona upo hispania but tukisema ligi ya ushindani naona upo epl.
 
Kwangu mimi EPL ni ligi bora kabisa tangu ligi ya Italy ilivyo poteza umwamba wake miaka ya mwishoni mwa tisini. Kinacho nifurahisha pale timu zisizopewa nafasi ya kushinda zinapo pindua meza kibabe.
Ladha nyingine ni nguvu na kasi inayotumika na timu nyingi kucheza direct football. Vilevile Marefalii wanaitofautisha Ligi ya EPL na nyingine za Ulaya kwa kuruhusu ubabe/Nguvu kutumika bila kupigapiga hovyo filimbi. Ndio maana wachezaji lain lain hawezi kukipiga EPL watakimbilia Spain, German,au Itali.
 
EPL ni ligi inayotangazwa sana haswa kwenye makoloni yaliyokuwa ya Mwingereza hata ukienda America kusini Laliga ndo inaongozwa kuangaliwa. Katika ubora Laliga kuna Moira mzuri kuliko EPL sema EPL kuna kelele nyingi za mashabiki viwanjani
Kwangu mimi EPL ni ligi bora kabisa tangu ligi ya Italy ilivyo poteza mwamba wake miaka ya mwishoni mwa tisini. Kinacho nifurahisha pale timu zisizopewa nafasi ya kushinda zinapo pindua meza kibabe.
Ladha nyingine ni nguvu na kasi inayotumika na timu nyingi kucheza direct football. Vilevile Marefalii wanaitofautisha Ligi ya EPL na nyingine za Ulaya kwa kuruhusu ubabe/Nguvu kutumika bila kupigapiga hovyo filimbi. Ndio maana wachezaji lain lain hawezi kukipiga EPL watakimbilia Spain, German,au Itali.
 
EPL ni ligi inayotangazwa sana haswa kwenye makoloni yaliyokuwa ya Mwingereza hata ukienda America kusini Laliga ndo inaongozwa kuangaliwa. Katika ubora Laliga kuna Moira mzuri kuliko EPL sema EPL kuna kelele nyingi za mashabiki viwanjani
Kama unafikiri EPL uborawake ni matangazo pekeyake basi izo liginyingine zijitahidi kutangaza ili ziwe na mashabiki wengi kama Epl.
 
Kwangu mimi EPL ni ligi bora kabisa tangu ligi ya Italy ilivyo poteza umwamba wake miaka ya mwishoni mwa tisini. Kinacho nifurahisha pale timu zisizopewa nafasi ya kushinda zinapo pindua meza kibabe.
Ladha nyingine ni nguvu na kasi inayotumika na timu nyingi kucheza direct football. Vilevile Marefalii wanaitofautisha Ligi ya EPL na nyingine za Ulaya kwa kuruhusu ubabe/Nguvu kutumika bila kupigapiga hovyo filimbi. Ndio maana wachezaji lain lain hawezi kukipiga EPL watakimbilia Spain, German,au Itali.

PUMBA
 
Kama unafikiri EPL uborawake ni matangazo pekeyake basi izo liginyingine zijitahidi kutangaza ili ziwe na mashabiki wengi kama Epl.

Kama ni bora walishindwa nini kuchukua uefa na europa cups miaka yote!! Ukiangalia by records spain ndie wanaongoza wana 18 wakati Uingereza wana 13...ukija europa league the competition has been won 11 times by teams from Spain, more than any other country...

Ebu tuambie ubora wake ni upi??
 
EPL inaangaliwa sana South East Asia (China, Japan, S.Korea India kidogo, Indonesia, Malaysia nk) middle East wanaangalia zaidi Laliga, S. America Laliga imetawala N.America 50/50, Africa inategemea na nchi uliyopo (Hapa Vijana wa Tz wataonekana wanaangalia sana EPL)
 
Mimi si mshabiki wa mpira, lakini mpira ni kushinda. Hivyo kama uchambuzi wako ni sawa basi La Liga ni bora zaidi. Hayo mengine ni hisia zinazoletwa zaidi na historia. Uzuri wa mpira haujalishi lugha inayotumiwa na sheria ni zile zile na goli ni goli. Isiwe kama wale waliosema "ingawa wametufunga lakini chenga twawala". Unakuwa mzuri zaidi ukiwala chenga na kuwafunga.
 
EPL inaangaliwa sana South East Asia (China, Japan, S.Korea India kidogo, Indonesia, Malaysia nk) middle East wanaangalia zaidi Laliga, S. America Laliga imetawala N.America 50/50, Africa inategemea na nchi uliyopo (Hapa Vijana wa Tz wataonekana wanaangalia sana EPL)
Labda China. Japan inakuwa usiku sana au asubuhi
 
Back
Top Bottom