Ni hotuba ya Rais yupi ilikuwa bora wakati ufunguzi na ufungaji wa bunge?

Pendaelli

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
8,920
23,246
Hope mpo salama,

Katika tukio la kumuapisha waziri mkuu awamu ya tano kipindi Cha pili, moja Kati ya kauli za waziri mmoja alimpongeza mh Rais kwa hotuba bora ya karne wakati akizindua bunge.

Kwa kweli mimi binafsi niliweza kuisikiliza hio hotuba, nikailinganisha na ile ya 2015, Kisha nikarudi nyuma kwa mh Kikwete wakati akifungua bunge kipindi cha pili kwake. Na pia kufunga bunge kipindi Cha Kwanza Cha Kikwete, nilionelea hotuba ya juzi bungeni ni kama ya kawaida sana pengine kuliko zote.

Labda kwa vile sina kumbu kumbu na Wala kuzisikia hotuba za mwalimu , Mzee Mwinyi na mh Mkapa bungeni ndio maana nikaja kuuliza hapa wakuu, kweli ile hotuba ya juzi ni hotuba bora ya karne?

Walao naona hii ya mh Mkapa wakati wa kipindi chake cha pili siku ya kuapa kwake ilikua Ni bora kuliko ile ya mh juzi na Jana iliojaa vijembe na mipasho.

 
Mshamba wa Chato asiyejua hata kiswahili wala kuhutubia yeye anajua kufokea fokea tu.

ILIKUWA HOTUBA MBOVU KABKSA KUWAHI KUZISIKIA.

HOTUBA YA MWALIMU NYERERE KUDUNGA NA KUFUNGA BUNGE NI HOTUBA BORA KABISA ZA MIAKA YOTE.
 
Hotuba iliyokonga mioyo na kutoa mwelekeo kitaifa ni Ile ya 2015!

Ilikuwa imejaa hoja, utatuzi na ufumbuzi wa matatizo ya moja Kwa moja ya wananchi,

Binafsi yangu, hiyo ndio ilikuwa hotuba ya Karine iliyogusa kila eneo na kutoa mwelekeo wa kitaifa
 
Hotuba iliyokonga mioyo na kutoa mwelekeo kitaifa ni Ile ya 2015!

Ilikuwa imejaa hoja, utatuzi na ufumbuzi wa matatizo ya moja Kwa moja ya wananchi,

Binafsi yangu, hiyo ndio ilikuwa hotuba ya Karine iliyogusa kila eneo na kutoa mwelekeo wa kitaifa
Tatizo matokeo ni tofauti na matarajio mkuu
 
Back
Top Bottom