Ni hatari Jeshi la Polisi kuzagaa mtaani

Ni hatari Jeshi la Polisi kuzagaa mtaani

Majibu ya hivyo vyote utayapata kesho ukidiriki kuandamana, hapo ndipo utajua kama polisi ni wachache au wengi, au wana miili ya kazi au hawana.
Yaap mkuu, citizen must ask government why? and government respond answer to citizen in good faith not in bad ways like this,
 
Hizo jumuiya za kimataifa hata zikiangalia hazina msaada kwenu mkithubutu kuingia barabarani. Wengi wao ni majizi tu na safari hii kichaa kapewa lungu.
SABABU ZA KUWACHAPA TUNAZO
NIA YA KUWACHAPA TUNAYO
UWEZO WA KUWACHAPA TUNAO
TUTAWACHAPA MJE BARABARANI MUONE
Peleka utahira wako huko, wananchi ndo wenye nchi yaan ndo maboss wa serikali sasa wewe uliona wapi wafanyakazi wakimpiga boss wao
 
Kuna Athari kubwa sana kwa Jeshi la Polisi kuzunguka na magari na silaha mtaani. Nimejaribu kuainisha sababu kadhaa chache;

Moja, lengo lao ni kuleta hofu kwa Wananchi lakini hali hii hujenga usugu na mazoea kuwaona kuwa si lolote si chochote. Mbinu hii ni mbaya sana.

Pili, huweza kuwajengea wananchi ujasiri wa kukabiliana nao, ni hatari sana maana kama kweli atakuepo mtu mwenye nia ovu, anaweza kuangalia the way wanavyojipambanua na mtu huyo akajenga namna ya kuwashambulia Askari. Kwa mfano, Jana nimekutana nao kigogo, wako kwenye gari kama sita! Ni rahisi sana kushambuliwa kama atakuepo mtu mwenye nia ovu.

Tatu, ili uweze kushambuliwa vizuri ni lazima umjue vizuri adui yako, yale magari yao ambayo wamejifunga mikanda ikitokea wamefanyiwa ambush watakumbuka saa ngapi kufungua seat belts na kushambulia?

Nne, askari wa Jana wengi hawana miili ya kazi, sijajua upande wa akili, lakini kwa miili ile kweli wananchi wakilianzisha hakuna atakayepona. Wajitahidi mazoezi.

Tano, ni wachache sana! Wananchi wa Kigogo peke yao wangeweza kuziba barabara na kuwaweka mtu kati tungepoteza Askari wetu kizembe sana.

Ushauri wangu, kama lengo ni kuwatisha wananchi basi tujue tumepanga mkakati wa hovyo saana maana unampa adui ABC kuhusu wewe.

Tujitafakari, umwagaji damu ni hatari kwetu sote. Tuipende nchi yetu
Police wetu hawajazoea mikiki mikki matumbo makubwa wanacho jua wao ni kula rushwa na kubambikia watu kesi
 
Nakubaliana kabisa na mtoa mada kuhusu athari za polisi kurandaranda mitaani jinsi wanavyofanya hasa ukizingatia uwezekano wa kujenga chuki na usugu.

Kuhusu usugu na chuki tukumbuke namna watoto wadogo wa shule za msingi kule Soweto Afrika Kusini 'walijitoa ufahamu' wakaamua kupambana na polisi wa makaburu waliokuwa na silaha nyingi na kali zaidi kuliko hata hawa wa kwetu.

Hatujui ndani ya akili za Watanzania sasa hivi kuna nini. Lakini kama wameshafikia usugu wa kuamua 'liwalo na liwe' hali inaweza kuwa mbaya sana. Sidhani kama kesho maandamano yatakuwepo lakini kwa hakika kuna watu wengi sana wanao uchungu mioyoni mwao. Hatujui huo uchungu wao unaweza 'ukalipuka' kwa namna gani na kuwafanya waamue 'liwalo na liwe'. Tunisia ilianza hivi hivi, na kule Syria ilianza hivi pia.

Namwomba tu kila kiongozi atafakari kwa kina sana hali iliyopo sasa na kufanya kila analoweza kurekebisha mambo. Kuendelea kufikiri hizi ni 'mbinu za wapinzani' kutaka kuharibu amani ya nchi sio sahihi. Wenye malalamiko ya kudhulumiwa ardhi zao, na kukoseshwa haki kwenye mambo mengi sio wapinzani peke yao bali hata wananchama wa ccm na wasiokuwa na vyama. Kama hakuna mwananchi aliye na uchungu wa jambo fulani ni nani atakayekubali kupoteza muda wake kujiingiza kwenye maandamano?
 
Umenena kweli tupu, ndio Msingi WA thread yangu. Ni hatari Sana Sana. Kesho na keshokutwa tutamlaunu Nani??
 
Siamini kama ni tishio la yule dada wa marekani linasababisha wapiganaji wetu kuzurura huku mitaani...hii ni fedheha kubwa kwetu sisi.
 
Yaaani kadada kamoja tu ambako hakafiki hata kilogram 60,hajapitia mafunzo ya jeshi kawaaamuru mapolisi na mitambi yao waandamane leo,hata kama maaandamano hayatafanyika lakini yule dada kawachezesha gwaride sizonje,ma rpc bila wao kupenda
 
Maandamano Ya jeshi la polisi yanaendelea Leo siku Ya pili huku alieamulisha akiva bado yuko huko Marekani

Mimi nitoe tafadhali Kwa polisi mkitoka huko msije kutusumbua kutuomba omba bia kwenye Baar maana mmezoea Sana kuja Baar kutuomba omba bia mkimaliza maandamano mange kimambi awalipe kabisa posho ili tupumue Leo na kuombwa ombwa offa Ya bia maaana kwenye Baar mnakera Sana
Mimi nikijua we ni polisi tu hata salamu hupati.
 
Mmi Nipo Jiji Fulan Hapa,Naona Maandamano Ya Polisi Yanaleta Usumbufu Usio Wa Lazma Barabarani,Maana Cjaona Yeyote Aliyebeba Bango La Kumlaani Mange Kimambi! There For Maandamano Yao Ni Bubu,Hayana Maudhui Yeyote! Ni Kher Watupishe Sisi Raia Kwa Vile Sisi Tunaye Wa Kumlaani,Tunazo Jumbe Nyingi Tu Za Kuwasilisha..Unity 4RevEr.
Mkuu hayo sio maandamano ya polisi bali nachohisi ni mazoezi tu ya kawaida. Lakini kujua kama kweli ni maamdamano yao tusubiri mpaka ijuma asubuhi twaweza kuwa na jibu.
 
Wengine wamebeba hadi Missile Launcher sijui RPG.

Ila polisi wamefeli sana kuanzia kidato cha 4 hadi strategy zao.

Mwingine bila aibu anasema atawapiga waandamanaji kama mbwa koko. Anaropoka akisahau huyo rais ambaye yupo madarakani ana kinga. Alichosema kitatumiaka kama ushahidi mahakamani.

Polisi wanasahau kwamba wanaoandamana wanafuata haki zao za kikatiba.
 
Hizo jumuiya za kimataifa hata zikiangalia hazina msaada kwenu mkithubutu kuingia barabarani. Wengi wao ni majizi tu na safari hii kichaa kapewa lungu.
SABABU ZA KUWACHAPA TUNAZO
NIA YA KUWACHAPA TUNAYO
UWEZO WA KUWACHAPA TUNAO
TUTAWACHAPA MJE BARABARANI MUONE
Yani hawa jamaa wanakua vituko kabisa na hio jumuiya yao ya Kimataifa walianza kujipendekeza tokea kwenye ishu ya Lisu......wakapiga kelele sana alivyopelekwa huko kwa Wazungu ishu zikabuma sasa hivi tena wanatafuta lakuzugia hio jumuiya inajua yote yanayoendelea hata hawahitaji hizo kelele zao ila kama wameamua tu kujifurahisha wacha waendelee
 
Kama hatutaki kumwaga damu demokrasia iachiwe huru. Rudishe hela zetu 1.5tr. Acheni kuua watu hovyo. Rudisheni ajira kwa watu. Acheni civil society zifanye kazi.
 
Askari kuwepo mitaani ni jambo la kawaida,hofu inatoka wapi wakati tunahitaji ulinzi siku zote au mtoa post wewe kibaka nini unaona dili zako zimevurugwa kwa uwepo wa polisi?
 
Kwanini msiongeze juhudi katika kazi zenu za kujiingizia kipato?mkianzisha ugomvi na lidubwana linaloitwa serikali mnajiondolea uhuru wa kufanya mambo yenu ya kujiingizia kipato.

Jeshi la Polisi libadilike badala ya kutumia mabavu kwa kila jambo wabadilike kulingana na hali.

Kupasha kabla ya vita hiyo ni hali ya kawaida upolisi ni fani na kama hujasomea upolisi ni vigumu kuponda hasa kwa kutumia vigezo vya umbo na muonekano usichague kitabu kwa kuangalia uzuri cover lake.
 
Back
Top Bottom