Watanzania wenzangu poleni na hofu inayotawala mioyo yenu kwa sasa. Nimesoma humu ndani thread nyingi za jana zinaripoti drills za jeshi la polisi. Jeshi la polisi linadai kuwa ni mazoezi yao ya utayari. Nimejaribu kutafakali nimeshindwa kuelewa kama ni lazima hayo mazoezi wafanyie mjini tena kweupe, mbele ya raia ambao wanaendelea kupambana kwa kutoka jasho kuona watapataje mkate wa kila siku. Napata mashaka. Sidhani kama hiyo ni njia sahihi ya kuwaweka polisi hao katika utayari wa kupambana na uharifu. Mazoezi ya utayari hayawezi kuwa ya hadharani tena mjini na kwa siku moja. Ukinambia kwamba mazoezi hayo yanalenga kuwatia hofu wananchi hapo nitaelewa vizuri. Lakini kwanini kuwatia hofu raia? Hofu humpata mtu kwa sababu mbalimbali. Kwanza kumekuwa na tabia ya jeshi la polisi, kupiga yeyote anayekuwa karibu pindi wanapodai wanatuliza ghasia. Lakini pia tumeshuhudi polisi hao hao wakifyatua risasi za moto moja kwa moja mahali ambapo kunaweza kuwa na watu wengi. Hakika silaha ya moto siyo ya kuchezea hovyo. Polisi wana marungu, na hata kama ni rungu unampigaje mtu pasipo kujali kwamba mtu huyo ama ni mpita njia au anashiriki katika ghasia? Mara nyingi tunapohoji, utasikia kwamba wanatumia weledi. Ndugu zangu hakuna weledi wa hivyo.
Hii peke yake inaleta hofu, kwani mambo mengi yanatendeka na lawama tunabaki kutupiana. Hiii ndio sababu mojawapo inayowatia hofu raia wema. Ni kwasababu ya matendo ya polisi. Hofu kwa watu ni mbaya mno, watu hujenga tabia ya kuogopa jambo lolote, liwe la heri au shari watu watakuwa waoga tu. Nakumbuka nilisimuliwa na babu yangu jinsi walivyokuwa wanaogopa wakimuona askali au polisi wa kikoloni. Naambiwa walikuwa wakijificha polini siku nzima hadi wanapelekewa chakula na wake zao. Binafsi sioni kama zama hizi zinapaswa kurejewa kabisa. Ni zama za giza, ambazo hazina tija yeyote kwa sasa. Binafsi hapo nilipo ninahofu, naelekea mpaka wa nchi jirani na kwakuwa nina visenti vyangu nitafanya shughuli ndogondogo huko. Hii dunia ni pana, hatuko ndani ya chupa.
Wasalam