Jamaa alikuwa anakataa asikae kwake na kumshhi arudi nyumban kwao. Katika hizo purukushani ndipo akapigwa na cm. Kwa busara hakumjibu yule gf bali alinitext na ndipo nikampigia akanipa full stor. Kimsingi huyu bwana asingefika huku kama sio papara na uelewa mdogo wa huyu gf.y.
Mimi nahisi, maisha anayoishi huyu binti na huyo kaka ake ndiyo yanapelekea huyu amekuwa hivi.
Naamini ukimsikiliza huyu dada naye, utaweza kupata ni jinsi gani, haya mambo yalikuwa.
Kumsikiliza huyo kaka peke yake, haitoshi kuona kwamaba huyu binti ana matatizo makubwa kiasi hicho.
Kwanza tukumbuke ni miezi miwili tu, ametoka kwenye maumivu ya kuharibikiwa mimba,
Bado kaka ake anamfanyia unyama pengine ni kwa sababu alibeba hiyo mimba.
Dah, lazima kunakuchanganyikiwa hapo. Kuwe tu na roho ya utu na upendo.
Wakati huu ni mgumu sana kwake, kaka hamtaki, boyfriend aliyembebesha mimba na kumsababishia
maumivu pia hamtaki. Jamani hili ni jaribu kubwa kwa huyu dada.
Hebu chukulia angekuwa ni dada yako, haiwezekani akampiga mtu kwa simu bila sababu, hata kama ni hasira,
hasira zina sababu, na baada ya kukugundua kaka yake ndiye anayeleta matatizo mmemsaidia je.
Hebu kaa upande wa huyo dada, halafu uone na kutafakari vizuri. Mchukulie kama mwanao, au dada yako, au mama yako
kabisa. Ooh my God, muoneeni huruma, basi atulie kwanza, muonesheni upendo, manake mmehusika katika hayo mapito yake.
Halafu baada ya muda atakapokuwa na yeye akili zimemkaa sawa, ataamua vizuri cha kufanya.
Nimehuzunika SANA!!!!!