Ni halali kumlazimisha Dada yako akaolewe?

msnajo

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
3,066
1,136
Ndg zangu naomba kuwasilisha hii mada. Kwa kifupi ni kwamba kuna jamaa yangu ana gf wake na wamekua kwenye mahusiano kwa muda wa 3 yrs. Mwaka jana Oct yule gf ali-conceive, baada ya miezi 2 kwa bahati mbaya ikatokea miscarriage. Kaka yake yule gf akashtuka na kuanza kumlaum yule jamaa yangu kuwa wameshirikiana kufanya abortion. Ilikuwa mzozo ila daktari ndie aliokoa. Walikaa kikao wakajadili kuwa jamaa atamchukua gf kutoka kwao lini, jamaa akaomba apewe muda wa miezi 2 ili awashirikishe wazazi na ndg zake ili ikiwezekana afanye mchakato wa mipango ya vikao. Kabla ya miez 2 kuisha yule gf akamwambia jamaa yangu kuwa anataka ahamie kwake hakuna haja ya kusubiri hiyo miez 2 iishe. Yule jamaa akamkatalia na wakakwaruzana kwa swala lile. Wakiwa kwenye mkwaruzano yule gf akaja kwa nguvu na cku jamaa anarudi ucku kuhangaika anamkuta gf wake yupo nyumban anasema haondoki tena coz alikua na funguo nae pia. Yule bwana alinitext nikamuuliza, ameaga kwao? Akasema hapana na hawajui alipo. Nikachakachua nikamsihi amweleze Kakake gf ili isilete shda. Kaka akafoka sana kuwa hatambui anachotaka ni taarifa kuwa dadake keshaolewa. Yalikuwa makubwa sana coz yule gf alimkwaza jamaa kwa kitendo cha kuja kuhamia kwa nguvu, akimlazimisha amuoe na kumfokea kama mtoto. Alifikia mahali akampiga yule jamaa na cm ikamuumiza mdomo wa juu na kuvuja damu! Ilinckitisha sana. Jamaa akasema, ok, kwa kuwa ameamua kuja kwa nguvu na ujeuri akaamua kusepa na kumwacha gf nyumbani na cm imezimwa, so hapatikani ila kwa watu wachache. Nlishauri aripot police ili kaka yake gf asijesema mdogo wake ametoroshwa. Tuliripot coz yule gf alimwambia yule jamaa atajiua na kumuua yeye. Nikachunguza kwa makini sana nikagundua kuwa yule gf alilazimishwa na kakake na wifi yake kuwa aondoke home, cjui alikuwa anawakwaza nini? Mbaya zaidi aliekua anatoa shinikizo la kumwondoa nyumban ni wifi yake. Mpaka hapa ninapoandika hi mada yule jamaa ameapa hatomrudia yule bint ila nina wasiwasi kwani mapenzi ni mdudu wa ajabu sana. Yule bnt kwa kuwa aliona miez 2 ni ming sana sasa ana wakati mgumu na anamlaum kakake na wifi kwa kuwa lengo halikutimia! Kaka ke nae ana hasira coz huenda akamkosa shemeji mwenye chapaa.. Ushauri wangu ni kuwa pamoja na kwamba tunawapenda sana wake zetu, tuangalie na kupima ushauri wao, na pia mdogo wangu wa kuzaliwa inakuwaje namlazimishe kwenda kuolewa!. This is true story, naomba mchakato wa mawazo ili tumwongezee jamaa yangu ushauri. Na je akiamua kumrudia yule gf atumie taratibu zipi kuhakikisha hatopigwa tena na cm au kuropokewa kama ilivyokuwa hivi majuzi. Natanguliza shukrani zangu wakuu.
 
Duu!!hii kali.
Inaelekea wifi ndio chanzo cha kumfanya kaka kushinikiza dada kuolewa
ba huyo dada kumpiga mwenzake na simu na kumtusi ni hasira zilizosababishwa na kufukuzwa home
kwa kuwa inawezekana kaka ndo anamuweka mjini na hana pa kwenda, dada kachanganyikiwa na yeye kawa desperate anataka kuolewa kilazima iil nae awe na kwake.
Jamaa kukimbia na kumuacha binti peke yake inaweza kuleta tatizo mana keshatamka kuhusu kujiua so inabidi awe makini achkue muda wake ila asimkasirikie amueleweshe tu i.e. kama kweli alikuwa ana nia ya kuoa baad aya hiyo miezi miwili..
narudi
 
Jamaa alirudi baada ya binti kuamua kurudi kwao. Ila hawako kwenye good terms, manake walimfedhesha sana.
 
mmmh,jamani mambo ya kulazimisha ndoa mabaya,pengine penzi limeshaanza kufa,wewe unang'ang'ania tu.na huyo dada mbona yupo desperate hivyo.bora wote wawili wapeane break ya muda,kila mtu ampe mwenzie nafasi,huyo jamaa amueleweshe huyo dada
 
Jamaa hana hamu kwa sasa ameamua kuvuta subira hadi akili itakapotulia. nilimwambia aendelee na kazi zake kwa muda then afanye tathmini ya kina kuhusu yaliyotokea kabla hajachukua maamuzi yoyote
 
na huyo dada,mbona kama ana ukorofi fulani?.ndoa bado,ameshaanza kumrushia vitu,jee wakiwa ndani ya ndoa jee,huyo jamaa ndoa si atakuja kuiona chungu?
 
na huyo dada,mbona kama ana ukorofi fulani?.ndoa bado,ameshaanza kumrushia vitu,jee wakiwa ndani ya ndoa jee,huyo jamaa ndoa si atakuja kuiona chungu?

Nyota njema inaonekana asubuhi.
 
Yani sio wadada tu wanaolazimisha ndoa siku hizi mpaka ndugu?Well huyo kaka ashukuru tu Mungu amemjua huyo msichana mapema kabla hajamuoa!Akijitosa ajiandae maana kuna uwezekano wa kipigo kuendelea na kuongezeka huko mbeleni!
 
Nimeshamshauri sana kuhusu swala la kurudiana na huyo gf wake. Wasiwasi wangu ni kwamba mapenz yanauma kwa muda then tunasahau yaliyotokea! Naomba tumpe ushauri akiamua kumrudia aweke terms za namna gani ili kuhakikisha kuwa haya hayatarudia tena.
 
Aangalie yeye moyo wake unamtuma vipi/
Kama bado wanapendana aendelee
But kama anataka kumchukua kwa shinikizo
Asithubutu kabisa.
Mapenzi hayalazimishwi
Ndoa hailazimishwi ni hiari ya watu wanaoenda ishi pamoja
 
Hilo ni onyo kwamba hiyo familia akae nayo mbali,akijifanya amekolea sana kwa bint basi arudi ila anajua ategemee nini baadae.
 
Namshauri huyo kaka kama ana mapenzi ya kweli na huyo msichana akae nae mbali kwa muda, badae hasira zikiisha watakaa pamoja kuongea kuona kama wanaweza kurudiana na kufata taratibu zinazotakiwa ili wafunge ndoa.nakushauri hivi sababu unaweza kukosa kuishi na mwanamke umpendae sababu tu ya hasira na yeye kukosa ushauri unaofaa.
Tatizo hamnalo nyie bali ni wale ndugu wa mwanamke wanaolazimisha ndoa. na huyo wifi mtu atakuwa tu amechoka kukaa na huyo bibie. haya nakutakia kila la kheri.nakushauri usimwache kwanza usije juta badae
 
unajua hata kama ni hasira huwa zinafichwa hadi utakpoletwa ndani na nyumba na kuwa Maza house rasmi. Yule binti katika hasira zake alimtolewa kauli chafu, nainukuu kutoka kwa jamb "usinichezee na kunizoea. Mimi sio Mama yako". Katika hali kama hii mapema yote unaehubutu kumtakia umpendae, tena mume mtarajiwa? Wadada watatusaidia hapa ikiwa kama ni halali tuambizane.
 
Huyo binti hafai kuolewa kwa tabia hiyo aliyoonyesha!!

Mh unajua huyo bwana alimfanya nini labda nayeye alimfanyia unyama kwanini asijitetee binti wa watu .
Tujaribu kupima mambo mbona hii iko onesided tu
 
na huyo dada,mbona kama ana ukorofi fulani?.ndoa bado,ameshaanza kumrushia vitu,jee wakiwa ndani ya ndoa jee,huyo jamaa ndoa si atakuja kuiona chungu?

Je huyo jamaa alimfanyia nini hadi amrushie hivyo vitu?
 
Je huyo jamaa alimfanyia nini hadi amrushie hivyo vitu?

Jamaa alikuwa anakataa asikae kwake na kumshhi arudi nyumban kwao. Katika hizo purukushani ndipo akapigwa na cm. Kwa busara hakumjibu yule gf bali alinitext na ndipo nikampigia akanipa full stor. Kimsingi huyu bwana asingefika huku kama sio papara na uelewa mdogo wa huyu gf.y.
 
Dah! Sasa huyo jamaa yako si amuoe tu huyo dada.
Dada hakuwa na pa kukimbilia zaidi ya kwa mtu wake.
Na mmeshajua huyo dada maisha anayoishi na kaka yake. Sio vizuri, mnazidi kumuongezea majonzi. Huyo jamaa yako ajirudi tu.
Dah! Pole kwa mdada.
 
unajua hata kama ni hasira huwa zinafichwa hadi utakpoletwa ndani na nyumba na kuwa Maza house rasmi. Yule binti katika hasira zake alimtolewa kauli chafu, nainukuu kutoka kwa jamb "usinichezee na kunizoea. Mimi sio Mama yako". Katika hali kama hii mapema yote unaehubutu kumtakia umpendae, tena mume mtarajiwa? Wadada watatusaidia hapa ikiwa kama ni halali tuambizane.

hiyo kauli sio nzuri ila watu wanapokuwa na hasira hufanya maamuzi ya ajabu na hata kutoa kauli chafu.
Hilo nalo mlizingatie.
 
Back
Top Bottom