Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?

Du hayo tena ni makubwa,hebu tujiulize kutakuwa kweli naulinganifu wa medani za kiasi kati ya CCM na vyama vingine wakati hawa wanatumia fedha na nyumba za serikali kufanya mikakati yao ya kukandamiza upinzani kweli hayo ni matatizo makubwa,ninauhakika siku watanzania watakapoamua kuikataa CCM wengi wao wataporomoka vitambi
 
CCM ni chama kiongozi nchini mwetu,Viongozi wa CCM ndo hao watawala wa serikali yetu...kwahiyo CCM ndio Serikali...Hivyo HAKUNA UBAYA VIKAO KUFANYIKA IKULU!! ni mangapi yamefanyika ya kichama ndani ya IKULU lakin hayakuwekwa hadharani....conclusion ni HALALI hata kama hutaki kukabali ndio hivyo ishakuwa..
 
nimejiuliza hili swali pia, kuwa kazi za chama ndani na may be kwa gharama za serikali, mmh sijui wenye kuelewa hii inasemaje watupe msaada ktk tuta! but sio sahihi naamini hivyo!

In fact and law, its not proper. Hata Kidogo. The whole meeting is of CCM in nature. They have their offices nearby there. I wonder why all the time they run to state house! Wanalifanya pango la wanyang'anyi maana wote wezi tuu. Ukiangalia katiba yetu inakataza mambo, pamoja na mengine, Ubaguzi. Halafu inasisitiza Usawa. Kwamba nisabaguliwe kwa ninachomini ikiwa sijavunja Sheria. Sasa kama CCM in point of law ni sawa na vyama vingine kwa maana ya haki na uhuru, the CHADEMA or CUF wanaweza kuomba kufanyia vikao ikulu. And im sure hata kujaribu hawawezi maana wanajua watanyimwa. Where is equality here?

Halafu ikulu si ya CCM, ni ya wananchi wote. CCM waende Lumumba au Dodoma? IF we put ikulu as main office for executive branch of state, it goes at par with judiciary and legislature. Sasa kama wanaweza kufanya vikao vyao katika office hizo za mihimili mingine then it wil be right to do so.
 
Du hayo tena ni makubwa,hebu tujiulize kutakuwa kweli naulinganifu wa medani za kiasi kati ya CCM na vyama vingine wakati hawa wanatumia fedha na nyumba za serikali kufanya mikakati yao ya kukandamiza upinzani kweli hayo ni matatizo makubwa,ninauhakika siku watanzania watakapoamua kuikataa CCM wengi wao wataporomoka vitambi

Watakufa gafla!!
 
CCM ni chama kiongozi nchini mwetu,Viongozi wa CCM ndo hao watawala wa serikali yetu...kwahiyo CCM ndio Serikali...Hivyo HAKUNA UBAYA VIKAO KUFANYIKA IKULU!! ni mangapi yamefanyika ya kichama ndani ya IKULU lakin hayakuwekwa hadharani....conclusion ni HALALI hata kama hutaki kukabali ndio hivyo ishakuwa..

Mkuu Senator,

kwa hiyo kwa mtizamo wako ata kwenye uchaguzi 2010 watumie mali za umma kufanya kampeni zao nalo ni halali. hapa naongelea kuanzia magari , rasilimali watu, majengo ya serikali et al? Bado kuna kitu hakiko sawa. Kusigina sheria na kanuni na taratibu za sheria za nchi hii [hata kama ni kidogo] ndio zilizotufikisha hapa tulipo. Please tusimamie utawala wa sheria bandugu
 
Watakufa gafla!!

TB, naona wewe ni mfuasi wa jamaa wa hapo mwembechai. Just kidding. in a serious note; hayo ya Sheikh Yahya ni hatari kwa mstakabari wa taifa. Yasiponyooshewa vidole yanaweza kutufikisha ndiko siko. ebu turudi nyuma, chukulia huo utabiri ungekuwa kinyume cha hayo.. yaaani kwamba mkimpinga mkulu tu Israili anamchukua...

Turudi kwenye mada yetu bado sijashawishiwa na wadau wanaosema hivyo vikao vya kichama huko Ikulu ni halali.
 
Rais wa Jamhuri ana uhuru wa kufanya mkutano na kikundi chochote ikulu wakati wowote atakao.

Swali kama hili linakuwa na mantiki pale mkutano ufanyike ikulu alafu Rais asiwepo... lakini maadamu yupo utaambiwa na wana-usalama kwamba waliona Lumbumba sio salama sasa utasema je? na ofisi yake na makao yake yako Ikulu.
 
Nilikimbia haraka kuona Kasheshe ameandika nini kujaribu kuspin hili ... usalama? of all things ungekuja nazo unasema usalama? ccm wana jengo lao kule idodomya (ambalo by the way linatakiwa kutumia na vyama vyote vya siasa nchini). Kwa nini Kikwete asingepeleka mkutano huko?
 
Wakati mfumo wa vyama vingi unajadiliwa, nakumbuka Mrema au Mtikila (I stand to be corrected) alishauri kwanza kabla ya yote CCM iainishe mali zipi ni za Chama na zipi ni za Serikali. Sitashangaa siku chama cha upinzani kinashinda uchaguzi, tukaambiwa ikulu na makochi yote ni ya CCM. CCM ina assets nchi nzima. Wakifanyiwa audit sijui kama wataweza ku-verify hizi mali zote!Unaweza pata psychosocial stress buree!Sijui tutaanzia wapi!
 
i will be very happy ccm itakapoacha kuvaa magwanda ya kijani manake imenifanya nishindwe kuwa na shirt la kijani! ggggr cant be associated with them hta by color tu
 
i will be very happy ccm itakapoacha kuvaa magwanda ya kijani manake imenifanya nishindwe kuwa na shirt la kijani! ggggr cant be associated with them hta by color tu
Ni kweli green should never be associated na CCM, manake green stand for life (uhai). Thanks Gaijin!lolz!
 
Nilikimbia haraka kuona Kasheshe ameandika nini kujaribu kuspin hili ... usalama? of all things ungekuja nazo unasema usalama? ccm wana jengo lao kule idodomya (ambalo by the way linatakiwa kutumia na vyama vyote vya siasa nchini). Kwa nini Kikwete asingepeleka mkutano huko?

Kwa ushabiki it make a lot of sense, kwa kuangalia objectively it is cost effective kufanya mkutano wake ikulu kwa meeting kama ya CC.

Unafahamu mzee cost ya kumpeleka Rais wa Jamhuri Dodoma na Kurudi. au unadhani Rais atalipiwa na chama... safari zote za Rais zinalipiwa na Serikali mkuu... they are the one responsible kwa usalama wake.
 
Kwa ushabiki it make a lot of sense, kwa kuangalia objectively it is cost effective kufanya mkutano wake ikulu kwa meeting kama ya CC.

Cost effective kwa CCM mkuu au kwa taifa lote?

Unafahamu mzee cost ya kumpeleka Rais wa Jamhuri Dodoma na Kurudi. au unadhani Rais atalipiwa na chama... safari zote za Rais zinalipiwa na Serikali mkuu... they are the one responsible kwa usalama wake.

Mkuu Kasheshe,

Hapa ndipo makosa yanapofanyika. Vikao vya chama vinatakiwa kulipiwa na chama na si vinginevyo. Nchi zingine (mf marekani) raisi wa nchi akienda sehemu kwa ajili ya kampeni au chama chake, inabidi chama chake au PAC ichangie gharama za safari ya raisi.

Nadhani hapa utakubaliana na wale wanaoshauri kuwa raisi wa nchi asiwe pia mwenyekiti wa chama ili kupunguza matatizo kama haya. Wewe unasemaje?
 
Nadhani hapa utakubaliana na wale wanaoshauri kuwa raisi wa nchi asiwe pia mwenyekiti wa chama ili kupunguza matatizo kama haya. Wewe unasemaje?

Yes, But until when... kwa sasa yuko ndani ya mstari mkuu, na huwezi kulaumu kabisa.

Furthermore, kwa utaratibu wa sasa alivyofanya mkutano Magogoni it is cost effective kwetu taifa na kwa CCM kuliko angeupeleka Dodoma.

Ukifuatilia kwa makini CCM pia wanaogopa mzigo wa kusafirisha wajumbe wao ndio maana mara nyingi sana NEC inakutana wakati wa Bunge sessions.
 
Yes, But until when... kwa sasa yuko ndani ya mstari mkuu, na huwezi kulaumu kabisa.

Hapana Kasheshe,

Ukitaka kuwa objective .. Kikwete hayuko ndani ya msitari kwa kutumia jengo la serikali ya watanzania wote (vyama vyote) kuendeshea mkutano wake wa chama. Hii ni makosa "objectively" kama ambavyo ulianza argument yako. Ikulu sio jengo la chama kilicho madarakani. Ni jengo la serikali na linaendeshwa kwa kodi ya watanzania wote bila kujali itikadi zao.

Furthermore, kwa utaratibu wa sasa alivyofanya mkutano Magogoni it is cost effective kwetu taifa na kwa CCM kuliko angeupeleka Dodoma.

Ukifuatilia kwa makini CCM pia wanaogopa mzigo wa kusafirisha wajumbe wao ndio maana mara nyingi sana NEC inakutana wakati wa Bunge sessions.

Kama hii ikichukuliwa kuwa ni nzuri ... ilifaa basi ccm walipie gharama za ukumbi na matumizi mengine yaliyotumika kuendeshea mkutano. Je waweza kusema kwa hakika kuwa hili limefanyika?

Najaribu kukutana nawe katikati ya msitari unaotutenga hapa, kama ni cost effective kwa serikali kufanyia mkutano wa ccm ikulu, je ccm wamegharimika nini kwa kufanyia mkutano huu ikulu?
 
Naamini hili ni jambo lililo wazi kabisa kwamba Ikulu ni mahala pa kuongoza nchi na wananchi wote regardless of their political orientation. Inaendeshwa kwa kutumia raslimali yetu wote kwa kupitia kodi zetu tukiwa kama wakulima, wafanyakazi au wafanya biashara. Kwa hiyo Ikulu kutumika kwa shughuli za chama kimoja kilichoko madarakani kwa kutumia raslimali iliyochangiwa na wanachama say wa NCCR au CUF ni makosa makubwa kabisa na kuonyesha mapungufu makubwa katika uongozi wetu. Viongozi wetu lazima wawe na dhamira zinazowasuta kwa kufanya mambo kinyume kabisa na kuyatangaza mapungufu yao kwenye picha zilizoonyeshwa mbele kwenye gazeti la CCM la Uhuru.
 
Rais wa Jamhuri ana uhuru wa kufanya mkutano na kikundi chochote ikulu wakati wowote atakao.

Swali kama hili linakuwa na mantiki pale mkutano ufanyike ikulu alafu Rais asiwepo... lakini maadamu yupo utaambiwa na wana-usalama kwamba waliona Lumbumba sio salama sasa utasema je? na ofisi yake na makao yake yako Ikulu.

Haya nayo maoni ktk JF kweli? Naona wewe kila kitu ni sawa tu.
 
npo na gazet la mwananchi naiona hii picha na habari nkashtuka, mi nahsi c harari coz pale unatumika mda na raslimali za serikali badala ya kutumia za chama.
Wataalamu mnaojua katiba na mfumo wa siasa wa nchi hii mpo mbona hamjibu au mnataka tu kutukana bila kutuelekeza katika katiba na mfumo wa kuendesha nchi? Tunafuata misingi ipi ya demokrasia.yuaani nazungumza sisi ,yaani watanzania, sio ule wa Marekani au wa Uingereza ama wa China? Duhh nimepagawa kabisa.
 
Back
Top Bottom